in , ,

Arsenal hongereni ila bado hapa…

Jana tulishuhudia Pierre-Emirick Aubameyang akicheza mechi yake ya
kwanza akiwa na jezi ya Arsenal. Mechi hii Pierre-Emirick Aubameyang
alifanikiwa kufunga goli akipokea pasi kutoka kwa Henrikh Mkhitaryan
ambaye alitoa pasi tatu za magoli kwenye mechi hii.

Mechi hii Arsenal alicheza katika mfumo wa 4-2-3-1, mfumo ambao
ulimwacha Pierre-Emirick Aubameyang kuwa mshambuliaji wa mwisho, huku
akizungukwa na Iwobi , Ozil pamoja na Henrikh Mkhitaryan.

Ozil mara nyingi alikuwa anashuka chini katikati kuchukua mipira
kutoka kwa Xhaka na Ramsey kisha kuisambaza kwa kina Iwobi ambaye
alikuwa anatokea pembeni kushoto na Henrikh Mkhitaryan aliyekuwa
anaingia katikati akitokea pembeni kulia.

Kipi kilimfanya Aaron Ramsey ang’are katika mchezo huu?

Hat-trick katika mchezo huu, hat-trick ambayo ilitokana na yeye kuwa
huru, alikuwa huru kutembea popote mpira ulipokuwepo, alikuwa anashuka
chini kukaba na kupanda juu kushambulia.

Uhuru huu wa Aaron Ramsey ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na ubovu wa
safu ya ulinzi ya Everton ambayo ilikuwa inatengeneza uwazi mkubwa
katika eneo lao la kujilinda. Goli la kwanza la Aaron Ramsey, walinzi
wa Everton waliacha uwazi , uwazi ambao aliutumia Ramsey hata wakati
anapokea mpira alijikuta yuko huru peke yake, vivo hivo hata goli la
tatu kwake ambalo lilikuwa la tano kwa timu.

Ni sehemu sahihi kwa Henrikh Mkhitaryan?

Kwa mchezo wa jana ulikuwa mchezo sahihi na salama kwa Henrikh
Mkhitaryan kwa sababu ulimpa nafasi kubwa ya yeye kuwa mbunifu.

Je Arsenal ya jana ndiyo Arsenal inayotakiwa iwe kwenye ushindani?

Hapana, kwa sababu zifuatazo. Kwanza kipimo cha Everton siyo kipimo
sahihi kwa sababu Everton walikuwa wabovu kwenye kujilinda na
kushambulia (haikuwa timu ya ushindani)

Pamoja na kwamba Everton walikuwa siyo washindani wa dhati kwa Arsenal
lakini walitusaidia kutupa pungufu la Arsenal.

Pungufu ambalo linatengeneza sababu yangu ya pili. Pungufu hilo ni
aina ambayo Arsenal inatumia kujilinda.

Arsenal inajilinda vibaya kuanzia eneo la kiungo wa kati wa kujilinda
mpaka mabeki wao.

Hawana kiungo wa kujilinda ambaye ni dhabiti kuilinda safu ya ulinzi ya Arsenal.

Xhaka anaruhusu sana presha kubwa katika eneo la mabeki wa Arsenal.

Kama wakifanikiwa kupata kiungo wa kati wa kuzuia itakuwa na faida kwao.

Pili, wanaposhambuliwa mabeki wao wa kati wanatengeneza uwazi katika
eneo la nyuma, kiasi kwamba wakikutana na timu ambayo inajua kutumia
uwazi (space) unaotengenezwa na safu hii ya ulinzi ya Arsenal inaweza
ikawa na hasara kubwa kwao.

Kwa hiyo, pamoja na kwamba wamewaongeza Henrikh Mkhitaryan pamoja na
Pierre-Emirick Aubameyang katika kikosi chao kitu ambacho kinaonesha
kuongeza uzito kwenye kikosi na morali ndani ya kikosi, lakini
wanatakiwa wapate kiungo mzuri wa kati wa kuzuia, tangu aondoke
Patrick Evra hawajawahi kuwa na kiungo mzuri eneo hili, pili
wanatakiwa waongeze beki wa kati, umri wa Laurent unaenda na
anaonekana kupunguza utulivu pamoja na umakini kadri muda unavyozidi
kwenda.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

West Ham na mgogoro wa ubaguzi

Tanzania Sports

MWILI WA CONTE UNAONESHA KESHO YAKE