Arsene Wenger amewajibu wapinzani wake kwa ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Newcastle, idadi ambayo Arsenal pia waliwafunga Galatasaray kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwa wamefungwa na Stoke 2-0 mechi iliyopita ya ligi kuu.
Arsenal walionesha maelewano makubwa, Wenger akasema ushindi huo ni majibu tosha kwa shinikizo lililokuwapo, huku washabiki wakimshangilia kwa kusema; “kuna Arsene Wenger mmoja tu’ wakati mechi ikielekea kumalizika.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na mshambuliaji wa kati aliyetoka kwenye majeraha ya kuvunjika mguu majuzi, Olivier Giroud mawili na kiungo Santi Cazorla aliyetokea kung’ara katika mechi za karibuni.
Newcastle waliingia uwanjani wakiwa wanajiamini, kwani vijana hao wa Alan Pardew walitoka kuwafunga Chelsea mechi iliyopita na kuvunja rekodi yao ya kutofungwa msimu huu. Pardew alisema wameadhibiwa kwa makosa yao.
Beki wa kulia wa zamani wa Newcastle aliyekuwa nje muda mrefu kwa kuumia, Mathieu Debuchy naye alikuwa dimbani kwa Arsenal akicheza dhidi ya timu yake ya zamani. Wenger alikuwa na wasiwasi iwapo amchezeshe, akisema huenda hajawa timamu vyema, lakini hakuwa na jinsi kwani wachezaji wengine muhimu ni ama majeruhi au wana kadi.
CHELSEA NAO BADO WAZURI
Chelsea wameendelea kutanua kileleni mwa ligi baada ya kuwafunga Hull 2-0, lakini wachezaji wao wawili, Willian na Diego Costa walilambwa kadi za njano kwa makosa ya kujirusha wakijidai wamechezewa rafu.
Mabao ya washindi yalifungwa na Eden Hazard na Costa, na kwa dakika 30 Hull walicheza wakiwa 10 uwanjani baada ya Tom Huddlestone kupewa kadi nyekundu kwa kosa la
Beki wa Chelsea na England, Gary Cahill alikuwa na bahati ya kutotolewa nje, akaoneshwa kadi ya njano tu baada ya kumchezea vibaya Sone Aluko, ambapo kocha wa Hull, Steve Bruce alilmlalamikia mwamuzi Chris Foy kwa kutompa kadi nyekundu, akisema ulikuwa mchezo hatari sana.
CITY USHINDI KIDOGO, MAJERUHI WAPYA
Manchester City wameendelea kuwafukuzia Chelsea wakiwa nyuma kwa pointi tatu, baada ya kuwafunga kwa tabu Leicester 1-0, bao hilo likitiwa kimiani na kiungo wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard.
Hilo ni bao la 175 katika ligi kuu nchini England kwa Lampard lakini City wamepata maumivu baada ya wachezaji wao muhimu, Eden Dzeko ambaye ni mshambuliaji na nahodha Vincent Kompany kuumia. Mshambuliaji mwingine, Sergio Aguero yupo nje kwa maumivu pia.
Katika matokeo mengine, Bunrley wameshangaza kwa kuwafunga Southampton 1-0, Crystal Palace wakaenda sare ya 1-1 na Stoke kama ilivyokuwa kwa sunderland na West Ham wakati West Bromwich Albion waliwatungua Aston Villa 1-0.
Jumapili hii ni kivumbi baina ya Manchester United na Liverpool wakati Swansea watawakaribisha Tottenham Hotspur.
Comments
Loading…