*Ni kocha maarufu, ametangulia mbele ya haki
*Taifa lamlilia, Xabi Alonso asema ni kila kitu
Kocha maarufu aliyepata kuifundisha Timu ya Taifa ya Hispania, Luis Aragones ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 75.
Aragones alipata sifa kubwa alipokuwa akiwafundisha La Roja na kulipatia taifa hilo kubwa Kombe la Ulaya 2008.
Amepata pia kufundisha klabu kadhaa kubwa za Hispania, ikiwa ni pamoja na Barcelona na Atletico Madrid ambako alitwaa Kombe la La Liga mwaka 1977.
Aragones aliyejulikana kwa tambo na maelekezo yake uwanjani, alianzia kwenye uchezaji ambapo alifunga mabao 172 katika mechi 372 akiwa na Atletico na alichezea timu ya taifa mara 13.
The Spanish Football Federation issued a statement that “expressed its grief and shock at the death of Luis Aragones”.
Timu ya Taifa ya Hispania imetoa tamko, ikisema kwamba inamchukulia kwa uzito kocha huyo ambaye alifurahiwa mno na wachezaji wake baada ya kutwaa kombe hilo la Euro 2008.
Aragones honours alitwaa Kombe la La Liga akiwa mchezaji katika miaka ya 1966, 1970 na 1973 na Copa del Generalisimo 1965 na 1972 akiwa na Atletico Madrid.
Akiwa kocha alitwaa ubingwa wan chi 1977, Copa del Rey 1976, 1985 na 1992, Intercontinental Cup mwaka 1974 akiwa na Atletico Madrid na Copa del Rey mwaka 1988 alipowaongoza Barcelona.
Alichukua uamuzi wa kijasiri kwa kuwaondosha kikosini wachezaji mahiri kama Raul na Michel Salgado kisha akaanzisha mfumo mpya wa soka wa pasi fupi fupi ulioleta mafanikio makubwa.
Miaka minne baada ya mabadiliko hayo, timu ilifanikiwa Ulaya kwa kuwapiga Ujerumani 1-0 kwenye fainali kisha muda mfupi baada ya hapo akang’atuka akiwa ameshaweka misingi muhimu iliyotumiwa 2010 La Roja wakatwaa Kombe la Dunia na la Ulaya 2012.
Mchezaji mahiri wa Hispani, Xabi Alonso anasema kwamba Aragones ndiye chanzo cha mafanikio yao na kutwaa makombe kwa sababu aliwajengea kujiamini na wanaendelea hivyo sasa chini ya Vincente Del Bosque.
Hayati Aragones alipoondoka alikwenda kufundisha klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, akitaka kubadili mazingira. Apumzike kwa amani.
Comments
Loading…