Menu
in , , , ,

Ange Postecoglou safari imewadia?

Tanzania Sports

MSIMU wa pili unaelekea ukingoni kwa kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs. Spurs wapo katika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi kuu England wakiwa wamejikusanyia pointi 37 kutokana na mechi 31. Kwa maana hiyo ikiwa itashinda mechi zote 7 zilizobaki Spurs watakuwa na uwezo wa kufikisha pointi 52 na kubaki kati ya nafasi ya 6, 7 na 8, wakati huo wanatakiwa kuomba timu kama Chelsea, Newcastle United, Aston Villa, Chelsea na MAN City zifungwe katika michezo yake yote iliyobakia. Kwenye Ligi Kuu England ni dhahiri safari ya Tottenham Hotspurs kunyakua taji la EPL haipo. Kwa sasa wapo kwenye mashindano ya Europa League ambapo wataingai kwenye mchezo wa marudiano huko nchini Ujerumani dhidi ya Frankfurt. Mchezo wa kwanza kwenye dimba la White Lane ulimalizika kwa sare ya 1-1 na kuwaweka katika mazingira magumu kwneye mashindnao hayo. 

Maisha ya ukocha wa  Ange mar azote zymetawaliwa na msimu wa pili wenye mafanikio. Mara kadhaa kwenye mahojiano na vyombo vya habari amekuwa akibainisha kuwa msimu wa pili huwa anachukua kombe fulani. Katika Ligi Kuu EPL Spurs hawana nafasi yoyote kutwaa taji hilo kwani wanazidiwa pointi 36 na vinara wa Ligi hiyo Liverpool. Katika imani yake ya kutwaa taji kwenye msimu wa pili ni wazi haiwezekani akanyakua taji hilo kwani anashikilia itamsaidia kubaki Ligi Kuu pekee na kushindania vikombe.

Pili, katika imani yake hiyo kocha huyo ameendelea kubainisha kuwa uwezo w akutwaa taji bado upo, kwani kwenye mchezo wa marudiano anaamini wachezaji wake wataamua namna ya kushinda mchezo dhidi ya Eitratch Frankfurt. Endapo watashinda mchezo huo basi itakuwa ahueni kwa kocha Ange Postecoglou.

Daniel Levy atakubali msimu mtupu?

Hadi sasa inaonekana nafasi ya kocha Ange Postecoglou kuendelea na kibarua cha kuinoa Spurs huenda ikawa finyu kwa sababu matokeo ya timu hiyo hayaridhishi na amekuwa amekizufunga timu kubwa lakini anakuja kufungwa na timu ndogo. Kwa mfano kwenye mchezo mmoja dhidi ya Man City waliwahi kuichapanga mabao ya kutosha lakini ikawa kupoteza mechi dhidi yua timu ndogo. Daniel Levy anajulikana kama mmiliki wa timu menye mkono wa chuma. Linapofika suala la makocha kushindwa kufanya vizuri huwa anawafukuza haraka sana. Levy amewahi kuwafukuza makocha wakubwa kama vile Maurizio Pochettino na Jose Mourinho. Hivyo suala la kumfukuza Ange Postecoglou huenda likaw ajambo jepesi lakini sehemu pekee ambayo itaokoa kibarua chake ni kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Frankfurt.

Nini hasa kinachomkabili?

Ange Postecoglou ni kocha ambaye ameingia England akiwa na sifa za kutwaa mataji huko Scotland. Katika Ligi ya Uskochi kocha huyo alikuwa miongoni mwa miamba ya soka. Sifa zake za kiufundi ndizo zilizomfanya apate ajira ya kuifundisha Spurs, lakini tangu alipowasili huu ni msimu wa pili ambao unaelekea ukingoni huku akiwa hana uhakika wa kunyakua taji lolote. Kikosi chake kimekuwa kikicheza mpira wa kuvutia, lakini anaonekana kukosa kikosi cha kwanza thabiti ambacho kinaweza kupigania hadhi ya timu hiyo. 

Spurs wamefungwa katika mechi 16 na kushinda michezo 11 na kutoka sare 4 katika michezo 31 waliyocheza hadi sasa. Hii inadhihirisha mwenendo wa Spurs msimu huu si mzuri. Katika mechi 31 kisha kufungwa 16 ni jambo la hatari ambalo mwalimu anatakiwa kuhojiwa nini kinachotokea katikati ya uwekezaji huo. 

Uvumilivu walionao viongozi wa Spurs huenda ukafika mwisho kwa mwalimu huyo kwani haionekani kama anaweza kuendelea na kibarua hicho msimu ujao. Spurs imekuwa timu ambayo vijana wa mjini wanaweza ina homa ya vipindi, wanaweza kucheza vizuri mechi moja kisha wanakwenda kuvurunda nyingine. Mfano unapambana na timu kama Man City na kuionesha kuwa wewe ni mwamba lakini unakuja kufungwa na timu kama West Ham au  Everton lazima kuwe na hali ya sintofahamu.

Hofu ya usaliti?

Uvumi umeenea kwamba huenda kuna wasaliti wa kimbinu katika kikosi chao. Inasemekana kocha Ange Postecoglou anahisia na kubaini kuwa wapo wasaliti ndani ya Totteham Hotspurs ambao wanahujumu jitihada za timu hiyo. Kocha huyo amekaririwa na gazeti la Mirror kuwa ndani ya klabu yake kuna watu wanatumia mbinu chachu kukwamisha juhudi zake. Inaelezwa kuwa kocha huyo anaamini wapo wasaliti kwenye timu hiyo ambao wanafanya kila njia kuhakikisha haifanyi vizuri. 

Kocha huyo amekuwa akitoa matamshi yanayoashiria hali ya mambo ndani ya klabu hiyo si shwari na amekuwa akiwinda huku na huko kumkamata msaliti wake. kwa mujibu wa Mirror, kocha huyo amesema muda si mrefu atagundua nani hasa anafanya usaliti. Wakati huo klabu yenyewe imeanza uchunguzi wa kina kuhusiana na tuhuma usaliti ambazo zinadaiwa kufanyika kwenye klabu hiyo. Spurs inachunguza kujua nini sababu, nani na kwanini kumekuwa na shutuma za kusalitiwa klabuni hapo.

Nyota watakimbia?

Kila mchezaji anatamani kucheza Ligi ya Mabingwa ama kutwaa taji lolote. Spurs ya Ange Postecoglou haionekani kuwa kwenye mbio za ubingwa wa EPL. Sehemu pekee ambao Spurs inapambana kuonesha umahiri wao ni kwenye mashindano ya Europa League. Endapo watalikosa taji la Europa League, safari yao msimu huu itakuwa imefika tamati. Hii inaleta madhara kwa wachezaji nyota klabu hapo ambao wataona hakuna mwanga wa kupigia mataji bali kucheza kwa ajili ya kukamilisha taratibu tu. Katika misingi hiyo mbali ya ushawishi wa kifedha uwezekano wa kukimbiwa na nyota wake ni mkubwa kuliko inavyodhaniwa.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version