in , , ,

AMORIM NA RASHFORD NI KAMA PAKA NA PANYA

MARA ya mwisho kocha wa Manchester United, Ruben Amorim kumwelekeza mambo ya kiufundi Marcus Rashford ilikuwa wakati wa mchezo dhidi ya Bodo/Glimt mwezi  Novemba mwaka 2024 kwenye mashindano ya Kombe la Europa League. Maisha ya kisoka kati ya kocha Ruben Amorim na staa wake Marcus Rashford yamekuwa magumu kwa sababu za kiufundi na shauku ya mafanikio. Rashford ni mchezaji anayelipwa kitita kikubwa lakini uchezaji wake kwenye dimba la Old Trafford hauridhishi na sasa Amorim amemtolea uvivu kwa kumweka benchi mfululizo na zaidi anakuwa nje ha mipango ya kikosi cha mchezo. 

TANZANIA SPORTS inakuletea uchambuzi Makini juu ya mwenendo wa mambo kati ya kocha na mchezaji wake. 

HAWAZUNGUMZI TENA

Uhusiano wa kocha wa Manchester United

Amorim na Rashford ni mgumu na hawazungumzi tena. Hili si jambo la Siri Kwa sababu Kila upande unashikilia sababu zake za msingi. Kocha anamuona mchezaji wake kama mtu mvivu ambaye haoneshi kiwango wala thamani ya mshahara mnono anapokea. 

Kabla ya uamuzi wa kumweka benchi na nje ya kikosi cha Manchester United, kocha huyo amewahi kukiri kuzungumza na makocha wa zamani wa klabu hiyo kupata maoni yao juu ya mchezaji huyo pamoja na wengine. 

Kuanzia hapo ndipo Amorim alipokuwa mkali kwa Alejandro Garnacho na Marcus Rashford. Angalau Garnacho alikuwa mtulivu na kuonesha nidhamu ya kujituma, hivyo akapata nafasi ya kupangwa kikosini. Lakini hali ya Rashford imekuwa ngumu kuliko ilivyodhaniwa. 

Inaelezwa kuwa Ruben Amorim anazungumza na Rashford wakati anaokuwa na kikao na kikosi kizima cha Manchester United. Ni sababu hiyo Manchester United wapo kwenye mbio za kumsajili nyota wa Lecce, Patrick Dorgu kwa pauni Milioni  35.

Hakuna aliye tayari kukubali yaishe kati ya Ruben Amorim na Marcus Rashford kiasi Kwamba hawatazamani tena usoni.

KUKAA BENCHI AU JUKWAANI

Marcus Rashford alicheza mchezo wa mwisho mwezi Desemba mwaka 2024 na tangu hapo amewahi kuchaguliwa kwenye kikosi mchezo mara moja wakati ambao hakutumika. Kama ingekuwa vijana wa Kitanzania wangesema Rashford alitajwa kwenye kikosi lakini akaishia “kukoboa mahindi” wakiwa na maana ya kukaa benchi.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 anaendelea na mazoezi katika kikosi cha kwanza, lakini kocha wake Ruben Amorim hajawahi kuzungumza naye binafsi kuhusu mchezo, mbinu au masuala yote muhimu ya maandalizi ya mchezo. Kwahiyo Rashford amekuwa mchezaji wa kukaa benchi kama sehemu ya kuitwa kikosi cha kwanza lakini mara nyingi amekuwa nje ya benchi maana kwa maana kocha wake ahamweka kando ya kikosi chake hivyo kuishi a jukwaani.

HALI NI NGUMU

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fulham jumapili iliyopita, kocha Ruben  Amorim akizingumza na vyombo vya Habari alisema itakuwa rahisi kwake kumchagua kocha wa makipa Jorge Vital mwenye umri wa miaka 63 kucheza mchezo wowote kuliko kumpanga mchezaji ambaye haoneshi wala kuongeza na kutoa mchango katika kikosi chake. Hilo ni sawa na kusema kocha huyo haoni mchango wa Marcus Rashford na kwamba timu yake inaweza kuendelea kucheza bila staa huyo. 

Rubun alisema hayo wakati alijibu maswali ya Waandishi wa Habari za michezo ambao walitaka kujua hatima ya Marcus Rashford katika kikosi cha kwanza ambapo amekuwa akitengwa zaidi. Kimsingi majibu ya kocha huyo yalikuwa yanatoa maelekezo Kwamba uwezekano wa Marcus Rashford kupangwa kikosini katika mchezo wowote inabidi aanze kujitambua na kuonesha nidhamu na kiwango bora kinachoendana na hadhi yake. Na kwamba Rubun ameamua kutorudi nyuma katika mipango yake ya kukirudisha mchezoni kikosi hicho. 

“Ni suala lilelile na ambalo linamhusu Kila mchezaji. Endapo mchezaji utaonesha kitu cha ziada na cha kiwango cha juu katika uchezaji, pamoja na kufanya mambo sahihi uwanjani kutokana na mbinu zilizopangwa bila shaka utakuwa kwenye kikosi changu, na tunaweza kumtumia Kila mchezaji. Nadhani umeona leo, kuna kitu kilikosekana uwanjani, Ile hali ya Kasi ya mchezo na kuwadhibiti wapinzani kwa uwezo wa Ubunifu na mikimbio. Hata ukiangalia benchi unaona kuna upungufu wa wachezaji ambao wanaweza kubadili mwelekeo wa mchezo dhidi ya wapinzani, lakini ninapotakiwa kufanya mabadiliko ya wachezaji, kutoa na kuingiza, basi sitapepesa macho hata Jorge Vital anaweza kuingia kikosini kucheza nafasi yoyote .

CHANGAMOTO MPYA 

Mwanzoni mwa msuguano kati ya kocha Ruben Amorim na Rashford kulikuwa na kelele nyingi ikiwemo Kambi ya Rashford kubainisha kuwa yuko tayari kwa changamoto mpya. Alisema anahitaji changamoto mpya ikiwa na maana alikuwa tayari kuondoka katika kikosi cha Manchester United kwenye dirisha la dogo la usajili la Januari. Hata hivyo mshambuliaji huyo ameshindwa kupata timu ya kumsajili hivyo kukosa mwelekeo sahihi wa kucheza Soka lake.

 Pia sakata hilo limebaki hewani na kumfanya awe mchezaji anayeongeza idadi ya watu badala ya kutoa mchango katika kikosi cha kwanza cha Manchester United.

Haijulikani ni lini staa huyo ataondoka klabuni hapo, mahali alipoanza kusakata kandanda na inatarajiwa ataondoka kabla ya tarehe ya mwisho ya kufungwa mwa dirisha la dogo la usajili barani Ulaya. 

KUCHEZA KWA MKOPO

Licha ya kutamani kuondoka katika kikosi cha Manchester United, lakini mipango yake ilivurugika siku chache zilizopita. Rashford alikuwa miongoni mwa nyota wanaotarajia kusajiliwa na klabu ha AC Milan, lakini kanuni na Sheria zilizuia usajili huo. Kikanuni AC Milan ilikuwa na nafasi moja pekee Kwa mchezaji anayetoka katika nchi ya nje ya Jumuiya ya Ulaya. Tayari AC Milan walimsajili Kyle Walker toka Manchester City kwa Mkopo. Kutokana na kushindwa madili kadhaa, klabu ya Manchester United italazimika kumtoa nyota huyo Kwa Mkopo lakini hakuna timu iliyopatikana. Hivyo basi upo uwezekano nyota huyo akasalia kikosini hapo hadi mwishoni msimu huu kisha atakuwa huru kutafuta klabu nyingine ya kucheza.

AKIONDOKA, MWENZAKE ANAINGIA

Ingawaje Rashford anatafuta kila njia kutaka kuihama klabu ya Manchester United upo uwezekano wa mchezaji mwingine mpya kusajiliwa klabuni hapo. Hadi jumanne usiku wiki hii klabu ya Manchester United iliripotiwa kumfukuzia nyota wa kushoto wa Lecce,  Patrick Dorgu mwenye umri wa miaka 20 na raia wa Denmark Kwa kiasi cha pauni Milioni 35. 

MPANGO KABAMBE WA UWANJA MPYA 

Wakati huo huo, Jumanne wiki hii, Baraza la  Trafford liliunga mkono mpango wa klabu ya Manchester United wa upanuzi wa uwanja wa Old Trafford pamoja na maeneo yanayozunguka uwanja huo. Mpango uliopo ni kuwa na uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki  100,000 wakiwa wamekaa kwenye viti vyao. 

Liz Patel, mwanachama mwandamizi wa Baraza la Trafford  aliusifia mpango wa Man United akisema, ” Mpango madhubuti wa Klabu ya Manchester United kupanua uwanja wake wa Old Trafford unatoa dira ya umuhimu  wa maneno yanayozunguka uwanja huo. Mpango unaonesha kuwa utakuwa uwanja maarufu zaidi duniani, hifadhi ya Makumbusho ya Vita na Mfereji wa Manchester ambao ulitumika kupitisha meli. Kwa sasa tunataka kampuni ya ushauri ya Kimataifa kuhusiana na mradi huu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Hawamuoni Rodrygo, lakini anawaonyesha

Tanzania Sports

WYDAD CASABLANCA NA HESHIMA LIGI KUU TANZANIA