Miaka kumi na tano imepita tangu kocha Arsene Wenger achukue kombe la
ligi kuu ya England.
Kombe ambalo amelichukua mara tatu kwa miaka yote 21 aliyokaa pale England.
Ni uwiano mbaya na unaotia aibu hata kuuandika, lakini ndivyo hivo kwa
Arsene Wenger kwake ni kitu cha kawaida.
Haumii kuona mikono yake ina miaka mingi bila kubeba ligi kuu ya England
Moyoni mwake ashakubaliana na hali, hana cha kufanya zaidi ya kukubali
kuwa Arsenal anaifanya timu ya kawaida
Timu ya kawaida ambayo haiwezi kukaa na kushindana katika makombe
makubwa kama Klabu bingwa ulaya na Kombe la ligi kuu ya England.
Kwake yeye kumaliza akiwa ndani ya nafasi nne za juu ni faraja kubwa sana.
Atamaliza ndani ya nafasi nne za juu na atapata nafasi ya kushiriki
ligi ya mabingwa barani ulaya, atatolewa kwenye hatua ya kumi na sita
bora na kusubiri msimu mpya ambao atafanya kile kile alichokifanya
msimu jana.
Hakuna kipya ambacho unaweza kukisubiri kwa sasa kutoka kwa mzee
Wenger na ukakipata.
Maisha ya Arsene Wenger ni rahisi kuyatabiri kwa sababu ramani yake
anayotumia ni moja kila mwaka.
Habadiriki, hataki kujiingiza katika mabadiriko ya mpira, ana chukia
mabadiriko kwa kuamini yeye alivyo ndivyo mpira unavyotakiwa kuwa.
Yuko kwenye dunia ambayo anaamini Director of football siyo mtu
anayetakiwa kwenye mpira.
Ndiyo maana kila jukumu analibeba yeye, huwezi kushangaa Arsene Wenger
kuwa ndiye mkaguzi mkuu wa nyasi za mazoezi.
Yeye ndiye anayepigana kumfuatilia mchezaji kwa ajili ya kumsajili.
Sera zake za usajili bado ni zile zile ndani ya miaka nenda rudi.
Habadiriki, ndiyo maana anakuaminisha Sanogo alimleta Arsenal ili
kumjenga awe Thierry Henry mpya.
Ana muda wa kukuza vipaji kuliko muda wa kukuza na kusuka kikosi imara
cha kupigania ubingwa.
Mpira kwa sasa ni biashara, kama huwezi tumia pesa huwezi fanya biashara nzuri.
Pesa haileti makombe ila inakuletea wachezaji imara ambayo watakuja
kukupigania makombe.
Arsene Wenger haamini kupitia hilo, hataki kutumia pesa nyingi kwa
ajili ya usajili.
Hata mishahara ya wachezaji pamoja na malupulupu yao ni finyu
ukilinganisha na timu zingine.
Dunia ya sasa wachezaji bora huenda sehemu ambayo kuna vitu viwili,
cha kwanza sehemu ambayo atapata pesa nzuri na malupulupu mazuri au
sehemu ambayo ina uhakika wa kupata makombe upo, au vyote viwili kwa
pamoja.
Kwa Arsene Wenger vitu vyote viwili havipo, hakuna malupulupu,
mshahara mzuri na makombe.
Huwezi kukaa na mchezaji mkubwa ambaye anawaza mafanikio yake binafsi
kiuchumi pamoja na mafanikio ya mataji.
Mchezaji anafikiria kipi atawaonesha wajukuu zake na watoto wake
kipindi ambacho atakachostaafu.
Kizazi chake kitajivunia medali zake kubwa alizozipata na fedha alizochuma.
Lakini kwa Arsenal ni tofauti ndiyo maana wachezaji nyota huondoka na
kwenda kusaka mafanikio na kuyapata kila walipoenda.
Tulimshuhudia Henry akienda Barcelona kwa ajili ya kupata kombe la
ligi ya mabingwa barani ulaya na akafanikiwa kupata.
Ilimbidi Cesc Fabregas anunue mkataba wake ili tu apate nafasi ya
kwenda Barcelona ili apate nafasi ya kuchukua kombe la klabu bingwa
ulaya, alifanikiwa kupata alichokitafuta.
Ilikuwa maumivu kwa mashabiki wa Arsenal kuondokewa na wachezaji wao
pendwa, lakini ukweli ni kwamba timu yao haikuwa na uwezo wa kuwapa
wachezaji wale kitu ambacho walikuwa wanakitaka.
Kabla ya kuhama Robbin Van Persie aliandika barua kwa uongozi wa Arsenal.
Aliwaambia kama wanataka abaki wanatakiwa walete wachezaji nyota ndani
ya kikosi na kuachana na utamaduni wa kutumia wachezaji wa kawaida.
Walimdharau, wakampuuza mwisho wa siku akaondoka.
Akaenda Manchester United, sehemu anbayo makombe yalizaliwa. Na
akafanikiwa kuchukua kombe la ligi kuu ambalo hakuwa nalo awali.
Muda unazidi kwenda , mambo yako vile vile, hali ambayo inampa wakati
mgumu Alexie Sanchez kuendelea kubaki.
Miaka 28 sasa, anaelekea katika siku za mwishoni katika soka la ushindani.
Anahitaji makombe makubwa, Arsenal haina uwezo. Na anachotakiwa
kukifanya ni kutosubiri mafanikio yamfuate ni muhimu kwa sasa
mafanikio ayafuate ili apate hadhithi nzuri ya kuwasimulia wajukuu
zake