Algeria, Senegal waua
Mikiki ya fainali za 30 za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inaendelea nchini Guinea ya Ikweta, ambapo Algeria na Senegal wameibuka na ushindi waliopigania vilivyo.
Wakati Algeria waliwakausha Afrika Kusini 3-1, Senegal waliwashangaza Black Stars wa Ghana kwa kuwafunga 2-1. Kocha wa Algeria, Christian Gourcuff amesema timu yake imeepuka kuanzia mguu mbaya, baada ya kuanza kufungwa dakika ya 51.
Algeria wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele na hata kutwaa ubingwa, kwani kwenye fainali za Kombe la Dunia ndio walifanya vyema zaidi ya timu nyingine za Afrika, wakafika hatua ya mtoano licha ya wachezaji wake kuwa na swaumu kutokana na kufunga Ramadan.
Mchezaji wa Bafana Bafana, Thuso Phala alifunga bao la kuongoza, na wakiwa kwenye nafasi nzuri ya kupachika la pili, mchezaji wa Bournemouth ya England, Tokelo Rantie alikosa penati, kwenye wakati ambapo Algeria walishaanza kuhaha.
Kocha huyo Mfaransa alisema penati hiyo ilikuwa na athari kubwa, iwe wangeipata Afrika Kusini au kwa walivyokosa, na kutoka hapo ndipo Algeria wakarudi mchezoni, wakaja kufanikiwa kufunga mabao matatu katika dakika 23 za mwisho, Bafana Bafana wakabaki bila kuamini kilichokuwa kikitokea.
Afrika Kusini walianza kujichanganya pale Thulani Hlatshwayo alipojifunga na kuwapa washindi matumaini, kisha yakaja mabao mawili kutoka kwa Faouzi Ghoulam na Islam Slimani. Sasa wanajiandaa kuchuana na Ghana Ijumaa hii.
Gourcuff amechukua nafasi ya Vahid Halilhodzic baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia mwaka jana.
GHANA HOI KWA SENEGAL
Black Stars wamekwazwa na wenzao wa Afrika Magharibi, Senegal baada ya kufungwa 2-1, kwenye mechi ambayo washindi walifunga bao la pili katika muda wa majeruhi. Alikuwa ni Moussa Sow aliyemharibia siku Avram Grant, kocha wa Ghana aliyepata kuwafundisha Chelsea.
Akitokea benchi, Sow alifunga kwa mkwaju uliotokea kuwa wa mwisho kwenye mechi hiyo na kuwapa Simba wa Teranga pointi tatu muhimu. Mshambuliaji wa Ghana, Andrew Ayew aliwatanguliza Ghana kwa kufunga penati ya kipindi cha kwanza baada ya winga wa Everton, Christian Atsu kuangushwa na kipa Bouna Coundoul.
Hata hivyo, Senegal walikunjua makucha ambapo katika mashambulizi yao, shuti la Kara Mbodj liligonga mtambaa wa panya kabla ya Mame Biram Diouf wa Stoke kusawazisha. Ghana walipoteza nafasi kadhaa za wazi na palionekana kuwapo ombwe kwa kukosekana nahodha wao, Asamoah Gyan anayeumwa malaria.
Ghana walianza vyema hata hivyo, ambapo Andrew Ayew coolly stroked home from the spot after Atsu had been brought down by goalkeeper Bouna Coundoul.
Comments
Loading…