Collection

Ajibu aweka alama kwa Mkapa

Ni Ibrahimu Ajibu mchezaji nyota wa timu ya Simba ambaye naye ameweka historia yake uwanja wa Mkapa siku ya jumamosi ya tarehe 8 katika mchezo wa hisani wa mastaa Ali Kiba na Mbwana Samatta.

 Ajibu ndiye mchezaji wa kwanza kufunga goli tangu jina la uwanja wa taifa lilipo badilishwa na kuitwa uwanja wa Mkapa tuanzie kuhifadhi historia hii kwanza.

‘Yes’  ni mashindano yasiyokuwa rasmi kwa maana sio ya mashindano ila ndio mechi ya kwanza pia kupigwa katika uwanja huo tangu jinalifanyiwe mabadiliko hivyo tunaanza kuandika historia yake.

Ilikuwa hivi nyota huyo ambaye kwa sasa hana nafasi  ndani ya timu ya Simba alifunga goli hilo dakika ya 25 ya mchezo huo wa hisani kuchangia  watu wenye mahitaji maalumu .

Goli lake litaandikwa na linatakiwa liandikwe na tuanze kutunza takwimu sasa ili tusivurugane huko baadae.

Tena amemfunga goli kwa kumtungua  kipa mahiri kabisa Tanzania Juma Kaseja kwa kutumia akili nyingi. Huku chini nataka niongee na Ajibu amefeli wapi?

Mchezo huo uliisha kwa timu ya Ali Kiba kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 huku mchezo ukiibuka na shangwe nyingi kwa mashabiki hasa wa Simba baada ya kumuona Morrison ambaye picha zimesambaa na uthibitisho wake kuwa amehamia Simba akitokea Yanga kwa mkataba huru.

Pia tusisahau kuwaandika kina Mudathiri Yahya na Hassan Dilunga ambao nao walifunga goli la pili na la tatu.

Lakini hisotria huwa inabakia kwa yule aliyeanza kufanya wengine watafuataia.

Mchoro mzima wa tamasha hilo liko hivi nyota wa Muziki Tanzania Ali Saleh Kiba na mwanandinga namba moja Tanzania anayekichafua kule England Mbwana Samatta walibuni namna ya kutumia umaarufu wao ili kurudisha fadhila kwa jamii.

Ndipo wakaunda SamaKiba  sasa ni msimu wa tatu na mara zote kiasi kinachopatikana kinapelekwa sehemu maalumu.

Uzuri zaidi Kiba na Samatta wanatafuta wachezaji maarufu na watu maarufu pia kushiriki hisani hiyo.

Kwa upande wa Kiba kikosi chake kilikuwa hivi, Shaban Kado, Kibwana Shomary, David Luhende, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Lamine Moro, Mudathiri Yahya, Issa Abushehe, Said Ndemla, Ali Kiba, Japhary Kibaya na Ibrahim Ajibu.

Wakati upande wa Samatta, Juma Kaseja, Mohamed Hussein, Issa Rashid, Shomary Kapombe, Henry Joseph, Mohamed Samatta, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba, John Bocco, Haruna Moshi na Farid Mussa.

Katika misimu mitatu Samatta na timu yake ilishinda mara mbili wakati Ali Kiba ndio imeanza mara moja.

Maneno ya Ali Kiba kabla ya mchezo yaliashiria hiki tulichokiona kuwa alijinasibu Samatta hatomfunga tena.

Kablaya mchezo Ali Kiba amesema kuwa, safari hii hatakubali kufungwa na timu Samatta hata kama atatumia njia zake za kuwahonga waamuzi kama ilivyokuwa awali.

Hiyo ya kuhonga waamuzi aliongea kama utani tu wala sio kweli katika utani ili kuvutia mashabki.

 “Safari hii tumejipanga kuwafunga timu Samatta, hapo awali walitumia njia za kuwahonga waamuzi ili wapate ushindi ndio maana walifunga magoli ya kuvizia,sasa safari hii tutawafunga mabao mengi,” amesema Kiba.

Hivi vitu huwa vinafanyika sana Ulaya wanatumia kufanya wachezaji wa zamani mfano wale waliowahi kuwika Arsenal na wale wa Madrid wanaandaa tamasha na wanacheza kinachopatikana wanawapa watu wenye uhitaji maalumu.

Hivyo unapoingia uwanjani unakuwa umechangia moja kwa moja katika upatikanaji wa fedha kwa ajiri ya lengo lao.

Kwa mwaka huu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana maana mashabiki walifika wengi na wameweza kupata burudani.

Juu ya Ajibu alichemka wapi hiyo nitakuja nayo makala yake tofuati ili tuweze kumchambua kwa karibu kabisa.

Mchezaji ambaye alitoa’assist’ 15 namagoli 8 kwa msimu mmoja kweli msimu unaofuata anaenda kukaa benchi na kupata nafasi chache za kucheza.

Je wapi amekosea chaguo lipi lilikuwa sahihi kwake au mapenzi ndio yamemfanya asiende sehemu sahihi tutakuja nayo katika makala nyingine.

Nikukumbushe tu Abdi Kassimu ndiye mchezaji wa kwanza kufunga goli wakati uwanja umezinduliwa 2007 wakati huo unaitwa Uwanja wa Taifa tena ilikuwa dhidi ya timu ya taifa ya Uganda, sasa naye Ajibu kaja kumjibu katika hisani ya Ali Kiba na Mbwana Samatta.