in , , ,

Man United wachanganywa Ukraine

*Manchester City waaibishwa nyumbani

*Mancini ameanza kwa sare Galatasaray

 

Kazi bado ni nzito kwa klabu za Manchester, baada ya usiku wa kuamkia Alhamisi kupata matokeo yasiyoridhisha kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Manchester United walikabiliana na Shakhtar Donetsk nchini Ukraine, ambapo licha ya kupata bao la kuongoza mapema, waliishia kwa sare ya 1-1.

Alikuwa mshambuliaji wa Brazil, Taison aliyewanyima vijana wa David Moyes ushindi wa pili kwenye UCL, baada ya kupachika bao dakika 14 tu kabla ya kipenga cha mwisho.

Bao la United lilifungwa na mchezaji wa timu ya taifa ya England, Danny Welbeck aliyenasa mpira wa chini chini wa Mbelgiji Marouane Fellaini.

Bao la kusawazisha lilipatikana baada ya nahodha wa Mashetani Wekundu, Nemanja Vidic kushindwa kufagia majalo ya Yaroslav Rakitskiy hivyo kunpa nafasi Taison kucheka na nyavu.
Kipa wa United, David De Gea alifanya kazi ya ziada dakika za mwisho kumzuia Taison kufunga bao la ushindi.

Matokeo hayo yamewafikisha United katika pointi nne, wakiongoza kundi lao kwa tofauti ya bao tu, maana wanalingana na Shakhtar.

Bayer Leverkusen wanafuatia kwa pungufu ya pointi moja tu, kutokana na ushindi wao wa bao 2-1 dhidi ya wanaoonekana kuwa wanyonge wa kundi, Real Sociedad.

United hawakuwa wazuri uwanjani, ambapo katika mechi nzima ni shuti moja tu lililenga goli na kupatikana kwa bao hilo, ikiwa ni mara ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa tangu 2006.

PELLEGRINI BADO HOMA IPO JUU

20131003-092038.jpg

Manchester City wamepokea kichapo cha pili mfululizo katika mashindano yote, baada ya kudhalilishwa nyumbani na mabingwa watetezi, Bayern Munich kwa mabao 3-1.

Kiwango cha kipa wao, Joe Hart hakina uendelevu, kwani amekuwa akipanda na kushuka, na katika mechi hii ya nyumbani, amewasababishia hofu washabiki.

Kocha Manuel Pellegrini atatakiwa kufikiria sana na kuamua iwapo aendelee kumtumia wakati huu au ampe nafasi papili wake, Costel Pantilimon.

Kocha wa zamani wa City, Roberto Mancini alipata kuanza kupoteza imani na Hart na kumsema hadharani kabla Mancini hajafutwa kazi.

Washabiki waliotarajia mchezo mzuri walimshuhudia Hart akisukumiza wavuni mpira mrefu wa Franck Ribery mapema. Bao la pili lilifungwa na Thomas Muller na la tatu aliliruhusu kirahisi baada Arjen Robben kupiga katika engo ya karibu naye.

City walijifuta machozi kwa bao zuri la Alvaro Negredo aliyeingia kipindi cha pili badala ya Edin Dzeko.

Mchezaji wa zamani wa City, Jerome Boateng alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya kiungo Yaya Toure.
Kichapo hicho kimewafanya City kushika

MANCINI AANZI SARE, REAL MADRID SAFI

Zemanta Related Posts Thumbnail

Wakati Manchester City wakilia, kocha wao wa zamani Mancini alikuwa na afadhali katika mechi yake ya kwanza katika klabu mpya ya Galatasaray.

Mtaliano huyo alipambana na wenzake Juventus na kupata sare ya 2-2, akimtumia zaidi Didier Drogba aliyefunga bao la kwanza kabla ya Arturo Vidal kusawazisha kwa panati.

Juventus waliwabadilikia Galatasaray kwa kupata bao la pili kupitia kwa Fabio Quagiarella lakini Waturuki walijitutumua na kusawazisha dakika moja tu baadaye kupitia kwa Umut Bulut.

Katika mechi nyingine, Cristiano Ronaldo aliwafungia Real Madrid mabao mawili na hivyo kutoka kifua mbele kwa FC Copenhagen kwa mabao 4-0.

Ronaldo amefikisha mabao 26 katika jumla ya mechi 21. Winga mwenzake, Angel Di Maria naye alifunga mabao mawili katika mechi ambayo Gareth Bale hakucheza.

Madrid sasa wapo juu ya kundi hilo kimsimamo, wakiwazidi Juventus pointi nne, huku Juve wakiwazidi Copenhagen na Galatasaray kwa pointi moja tu.

Matokeo mengine yalishuhudia Paris Saint Germain wakiwafunga Benfica 3-0; RSC wakichapwa nyumbani na Olympiakos 3-0 pia wakati CSKA Moscow wakiibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Viktoria Plzen.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

*WATATU KUSHIRIKI KOZI YA FUTURO ADDIS ABABA*

Uzembe Afrika waisononesha Fifa