Katika hali ya maelewano wajumbe wa mkutano mkuu na Baraza la Michezo
Tanzania BMT walikubaliana kuendesha mkutano mkuu na uchaguzi wa chama
hicho.
Mkutano mkuu kikatiba ndio chombo pekee chenye mamlaka ya kufanya
maamuzi ya kuendesha chama hicho kilitoa ridhaa ya uchaguzi na kuwapa
mandate viongozi waliochaguliwa kuitazama katiba ya chama hicho upya
na kuleta mapendekezo katika mkutano ujao kwa maslahi ya mchezo wa
mpira wa wavu nchini.
Wajumbe waliochaguliwa ni Israel Agapa Mwenyekiti, Muharam Mchume
Makamu wa Kwanza Mwenyekiti anaeshughulikia Mipango na Maendeleo,
George John Makamu Mwenyekiti wa pili Fedha na Utawala.
Katibu Mkuu Allen Alex.
Wengine ni Somo Kimwaga, Coaches commission, Amon Safiel. School
Development, Emanuel Majengo Regional Development Nkane Ali Beach
Volleyball.
Comments
Loading…