Kwa magoli aliyofunga David Molinga msimu huu ulioisha kama angekuwepo Ibrahimu Ajibu angefunga magoli mengi zaidi ya hayo.
Nasema hivi nikiwa na maana kubwa sana Yanga imekosa watengeneza nafasi ambao wangeweza kuwalisha washambuliaji.
Hebu tuachane na hayo kwanza turudi katika mzizi wa makala hii baada ya kumalizkia kwa ligi kuu Tanzania Bara.
Ligi kuu Tanzania Bara ilishaisha akilini mwa wengi wanafikiria maneno ya aliyekuwa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera juu ya kauli yake kwa David Molinga.
Zahera aliwahi kusema kuwa endapo Molinga asipofunga magoli 15 msimu huu ulioisha basi akatwe mkono.
Hadi kufikia leo hii ligi imeisha Molinga hakuweza kufikisha idadi ya magoli hayo aliyoyataja Zahera je tukamkate mkono ?
Molinga alifunga bao lake la 11 kwa kuifunga Lipuli lililoishusha jumla timu hiyo Uwanja wa Samora lililowapa pointi tatu Yanga ambao wapo nafasi ya pili na pointi 72.
Vipi Zahera atakuwa na jibu ya swali letu au tumsamehe basi mie naanza kumchambua kisha tujue tumsamehe au tukamchinje ?
Kwa namna alivyocheza na uchache wa mechi naanza kuamini kuwa Zahera alikuwa anaongea kitu sahihi.
Molinga alicheza mechi chache zaidi na ameweza kufunga magoli 11 huenda angecheza mechi nyingi angefikisha magoli zaidi ya hayo.
Alipokuja alikuwa katika uzito mkubwa mno ila baadae akabadilika na kuwa wa saizi ya kawaida na kuanza kufanya mambo yake uwanjani.
Aina ya wachezaji waliopo Yanga hakuna walishaji ambao wangeweza kumpatia ‘assist’ za kufunga magoli.
Pata picha walishaji wa Simba wangekuwepo Yanga Molinga angefunga magoli mangapi ?
Tena sio Ajibu hata angekuwa na mtu kama Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ basi angefunga zaidi ya hapa.
Ukiiwa mtu wa mpira unaweza kuona zile ‘Movement’ za Molinga anapohitaji mpira, ‘Yes’ sio wa daraja la juu sana ila wakati Yanga inatafuta watu wa kuisaidia timu Molinga anatakiwa abaki.
Wakati dirisha dogo la usjaili linatangazwa David Molinga ni miongoni mwa wachezaji waliokatwa na amshukuru kocha chiba Luc Aymael kwa kuhitaji arejee kikosini.
Ni kweli Yanga wanahitaji watu zaidi ili waweze kutengeneza ushindani lakini wataweza kushindana kama watawaacha wachezji wengi.
Ili tukubali tumsamehe hebu turejee namaneno yaZahrea baada ya ligi kuishakisha tufunge mjadala.
Hayo chini ni maneno ya Zahera baada ya kumalizika kwa msimu namavuno yaMolinga tumeyaona hebu tumsome.
Zahera ametamani Molinga abakie ili cheche zake azionyeshe msimu ujao nab ado anaimani naye.
Zahera anamfananisha Molinga kama Meddie Kagere na John Bocco wa Simba wachezaji mahiri ambao wanacheka na nyavu muda wowote.
Akizungumza jijini Dar es salaam Zahera amesema kuwa Molinga ni miongoni mwa wachezaji wenye kiwango cha juu klabuni hapo, ambaye anatakiwa kupewa nafasi ili aweze kufunga mabao zaidi kama vile Kagere wa Simba.
“Watu wengi walisema Molinga hafai huyu ni mchezaji mzuri na anaweza kuisadia Yanga, Kocha anatakiwa amuelewe Molinga ni mchezaji wa aina gani anacheza vipi, ufungaji wke hautoautiani na Kagere na Bocco” Zahera alisema.
“Nilisema atafunga mabao mengi akipewa nafasi atafanya vizuri zaidi, takwimu ya mchezaji ndiyo inayoonesha kama mchezaji ni mzuri au mbaya” Aliongeza.
Anatakiwa amjue ni mchezaji wa aina ani afanyishwe mazoezi ya kufika ndani ya boksi ili aweze kufunga mabao mengi, alikuwa anawekwa benchi hapati nafasi ya kucheza ndio maana alishindwa kuonyesha kiwango chake hapo nyuma” alimalizia Zahera.
Wajumbe mnasemaje tukamkate au tumvumilie kidogo tumpe muda msimu huu ?