Menu
in , , , ,

YUPI NI MWAKILISHI BORA WA AFRICA KOMBE LA DUNIA?

Tanzania Sports

Bara la Africa tayari limeshapata wawakilishi wa kombe la dunia nchini
Russia mwaka 2018.

Nchi tano tayari zimeshapata tiketi ya kwenda Russia ambazo ni
Nigeria, Misri, Morocco, Tunisia na Senegal.

Timu tatu kutoka Afrika ya kaskazini na timu mbili kutoka Afrika Magharibi.

Maendeleo ya soka la Afrika Kaskazini siyo ya kushangaza. Hata kwenye
michuano ya vilabu barani Afrika vilabu vya Afrika Kaskazini vilikuwa
vingi kwenye hatua ya nusu fainali.

Mataifa haya matano ndiyo yamebeba matumaini ya Afrika, swali la
kujiuliza ni yupi aliyebora wa kutufikisha mbali?

*NIGERIA*

Hii ndiyo nchi ya kwanza kukata ticketi kwenda Russia na ikimaliza
safari yake bila kupoteza hata mchezo mmoja.

Ikiwa imeshinda mechi 4 na kutoka sare mbili.

Nigeria katika harakati za kufuzu imefunga magoli 14 na ndiyo timu
ambayo imefinga goli nyingi.

Hii ikitoa tafasri ya kwamba Nigeria ndiyo timu ambayo ilikuwa na safu
Kali ya ushambuliaji kuzidi timu yoyote.

Ubora wao uko kwenye safu yao ya ushambuliaji na jinsi timu
inavyotumika katika upatikanaji wa magoli.

Lakini imefungwa magoli manne. Na kuwa moja ya timu ambazo zimefungwa
goli nyingi kati ya timu ambazo zimefuzu kwenda Russia.

Hii inatoa tafasri ya kwamba Nigeria anauwezo mkubwa wa kufunga goli
pia anaruhusu magoli pia.

Nigeria siyo mara ya kwanza kwao kufuzu kombe la dunia.

Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1994 ambapo walifika hatua ya 16 bora
ambapo ilitolewa na Italy kwa goli 2-1

Mwaka 1998, 2002, 2010 na 2014 walifuzu pia.

Ukiangalia Nigeria wameenda kombe la dunia kwa Mara ya tano na
kufanikiwa kuingia hatua ya 16 bora Mara mbili.

Hii inaonesha Nigeria wana nafasi kubwa ya wao kupita hatua ya makundi
kutokana na historia inavyombeba.

*MISRI*

Hii ndiyo timu pekee ambayo imefungwa mechi katika mechi za kufuzu
kombe la dunia.

Mpaka sasa kwa timu kutoka Afrika timu pekee iliyofungwa kwenye mechi
za kufuzu ni Misri.

Imefanikiwa kufunga magoli 8 na kufungwa 4 , hii inamaanisha ina safu
ya kawaida ya ushambuliaji, na INA safu ya ulinzi ambayo inafungika.

Misri imefuzu kabla Mara mbili, Mara ya kwanza ilifuzu mwaka 1934 na
Mara ya pili ilifuzu mwaka 1990 na mar a zote iliishia katika hatua ya
makundi.

Haijawahi kuvuka hatua ya makundi na huu ndiyo mtihani mkubwa kwao
kuhakikisha wanavunja mwiko wa kutofuzu

*TUNISIA*

Hawa ndiyo walikuwa timu ya kwanza barani Afrika kufunga goli katika
kombe la dunia.

Walifanya hivo katika michuano ya mwaka 1978, ambapo Tunisia iliifunga
Mexico goli 3-1 na kuwa timu ya kwanza kufunga goli katika kombe la
dunia.

Kabla ya hapa Tunisia imefuzu mwaka 1978, 1998, 2002 na mwaka 2006 na
mara zote wanaishia katika hatua ya makundi.

Katika kampeni za kwenda Russia, Tunisia hawajafungwa hata mechi moja.

Ila wamefanikiwa kufunga magoli 11 na kufungwa magoli ya manne (4).

*SENEGAL*

Hii ni Mara ya pili kwao kufuzu kombe la dunia. Mara ya kwanza ilifuzu
mwaka 2002 ambapo ilifanikiwa kufika robo fainali ya kombe la dunia
ambapo walitolewa na uturuki.

Senegal imefungwa goli chache kwenye harakati za kwenda Russia ,
ambapo mpaka sasa wamefungwa magoli 2 tu.

Hii inaonesha wana safu imara ya ulinzi ambayo hairuhusu magoli mengi .

Wamefanikiwa kufunga magoli manane (8) magoli ambayo yanaonesha safu
yao ya ushambuliaji ni ya kawaida.

*MOROCCO*

Hawa ndiyo ambao hawajafungwa goli lolote kwenye harakati za kufuzu
kombe la dunia.

Hii ni mara yao ya tano kufuzu kombe la dunia.

Wamewahi kufanya hivo mwaka 1970, 1986, 1994 na 1998 na mara zote hizi
wakaishia hatua ya makundi kasoro mwaka 1986.

Mwaka 2018 wanaenda na kikosi ambacho ni bora.

Maendeleo ya soka barani Afrika kwa sasa ni ya kiwango cha juu, hata
Bingwa wa klabu bingwa Afrika anatokea nchini kwao.

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Exit mobile version