Menu
in

Yanga yapita njia za Simba kivingine

Sifa ya kikosi bora Simba,Yanga na Azam

Ni busara kumkaribisha mgeni pale anapoingia katika kaya yako, na huu ndio utamaduni ambao Waafrika tumeutengeneza na una maana kubwa sana katika kutengeneza urafiki na undugu imara.

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania bara, Young Afrika (Yanga) wamefika mjini tangu mwaka 1935 miaka 85 hivi sasa, ila ni vyema tukawakaribisha kwa kuanza mchakato mpya wa mabadiliko ya timu yao kuelekea mfumo mwingine ambao utaleta manufaa ndani yake.

Karibuni Yanga niwakumbushe tu mchakato wa mabadiliko unahitaji uvumilivu na hekma sana ili kila kitu kiende vile mnavyotarajia, hapa mjini nafiriki mmeona pacha wako alipopita hadi kufikia hapo alipo hivi sasa, basi kuweni makini na manchokifanya huu sio muda wa kurumbana tena muwe kitu kimoja ili mfanikiwe.

Mchakato huo unahitajika gharama na bahati nzuri mnao wadhamini wenu ambao mnaenda sawa na wameahidi kuwa saidia katika mchakato wote hadi timu inakuwa katika muonekano mzuri.

Salamu za kuwakarbisha mjini inaishia hapo sasa tuangalie mbinu ambazo Yanga wamezichukua katika hatua za awali ambazo zinaonekana zinatija ndani yake.

Niwakumbushe Yanga mchakato wa mabadiliko haukuanza leo, zamani kulikuwa na Yanga kampuni na Yanga asili yote hayo yalikuwa katika harakati za mabadiliko ila mlichemka kwakuwa lengo halikuwa moja kwa navyoona hivi sasa mnaenda vizuri.

Yanga wanapita katika njia za Simba kivingine, baada ya kuona nini wamefanya mapacha wao Simba katika mchakato wa mabadiliko, sasa wameamua kuja kivingine kabisa.

Watoto wa Jangwani walianza kumleta mtaalamu Carraca Antonio Domingos Pinto kutoka Ureno, katika hatua za mwanzo kabisa ilia je achore mchoro wa mabadiliko, alifika bongo na akaahidi kurudi japo hadi leo hazungunziw tena , ila hatua nzuri ambayo inaonekana timu hiyo kupita njia nyingine ya aina yake toufauti na ile ya Simba.

Huenda mchakato huo ukaleta faida ndani ya timu hiyo huku wakipewa nguvu na GSM katika kulisongesha gurudumu la maendeleo la mabadiliko.

Baada ya hapo sasa hivi wameanza tena mchakato huo kwa kuungana na wataalamu kutoka Hispania (La Liga) ambapo pia ni njia nyingine inayotofautisha na ile waliyopita Simba wakati wa mchakato wao.

Hii inaweza kuwa na faida kubwa kwa soka la Tanzania hasa timu ikiwa na utegemezi yenyewe , maana halisi ya mabadiliko timu ipate kujitegemea hata kama hakuna mdhamini, hisa zake zitajiendesha na kuleta uhai wa kupambana na timu nyingine kubwa barani humo.

Huu mchakato utakuwa na maana kubwa sana kwa wanachama na wapenzi wa Yanga lakini utakuwa na maana zaidi kwa Mwenyekiti wa timu hiyo Mshindo Msolla ambapo katika kampeni yake wakati anahitaji kupigiwa kura ya kushika nyazifa hiyo kubwa alisema kuwa lazima atahakikisha mabadiliko yatafanyika, huenda Korona imekuja kutibua mipango yake maana alitaka mwezi huu wa tano tayari mambo yamekaa sawa.

Kamaa atatekeleza na kukamilisha mchakato huu basi Msolla atakuwa shujaa kwa ahadi na mipango yake ambapo kikifika kipindi cha kutoa maelezo kwa kipindi chake cha uongozi basi ataweza kujinadi na kujitutumua kuwa amefanikisha hilo.

Faida kubwa ambayo wataipata Yanga kama watafanikisha mchakato huo utembezaji wa bakuli utakuwa umeisha maana watakuwa na watu halisi watakao simamia timu.

Kwa katiba ya Tanzania katika michezo inasema endapo timu inahitaji kufanya mabadiliko basi iwe hivi, wawekezaji wanatakiwa wapate 49%, klabu inatakiwa iwe na 51%.

Wawekezaji wanatakiwa wawe wawili au zaidi katika kugawana zile hisa 49%, zile nyingine zitabakia kwa klabu ambapo nao watazigawanya kwa wanachama wao.

Kwa kanuni hii inambana muwekezaji kutokuwa na sauti sana ila atakuwa na faida yake ndani yake kwa wafanya biashara wanajua namna gani faidia inapatikana.

Yanga ni miongoni mwa timu zilizopata mafanikio makubwa kwa soka la Tanzania bara, hata ligi ya Muungano pia na Kagame .
Ilifika wakati timu hiyo imetungiwa wimbo na mwanamuziki Pepe Kale ‘Young Africa’ hayo yote ni miongoni mwa mafanikio waliyowahi kuyapata.

Sasa ni muda wa mabadiliko ili Tanzania nayo iwe kama nchi nyingine za Afrika zinazotoa wawakilishi wengi katika kombe la Shirikisho na Klabu bingwa wa Afrika.

Simba inapokuwa nzuri inategemea Yanga iliyokuwa bora, hivyo kila mmoja anamtegemeamwenzake katika kusukuma gurudumu mbele.
Ningependa kuwakumbusha tena kuwa katika harakati za kuweka mambo sawa kuna kuwa na ugumu wake kama mmeamua kuleta sura mpya ya klabu basi inatakiwa mshirikiane katika kutetea maslahi ya timu yenu.

Timu ya Simba kwa sasa iko mbali sana japo mfumo haujakaa sawa ila inaonekana iko katika kuelekea katika mambo mazuri, kama yale ambayo tumeyaoa kupata uwanja wake kule Bunju huku kukiwa na hosteli ambazo zitawasaidia wachezaji kupunzika humo.
Kupata uwanja wao kuna wezakupunguza gharama za timu hiyo kukodi uwanja na sehemu ya kuweka kambi ambayo ni moja ya sehemu ya kujitegemea.

Baada ya kuweka mfumo vizuri huenda tukaona wachezaji walio na hadhi kubwa kutua Ligi kuu Tanzania Bara kwani kila timu itakuwa na uwezo wa kuwaleta walio bora ule ujanja wa 10% hautokuwepo tena.

Kulipa mishahara kwa wakati hii inaweza kuwa na maana kubwa sana hasa kwa Yanga ambayo msimu uliopita ilikuwa katika matatizo makubwa ya ulipaji wa mishahara tatizo lilikuwa ukata.

Yanga hebu tulieni nendeni katika mstari ulionyooka,mkifika safari yenu mtarejea nyuma na kuangalia mlipopita mtaona namna gani mlipita na kuleta furaha kwa watu zaidi ya milioni 18 wanaowafuatailia.

Mpira wa Tanzania unatakiwa kubadilika sio kuishi kama ilivyokuwa miaka ya tisini kweusi.

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Exit mobile version