Menu
in , , ,

Yanga yamsajili “Dida” kutoka AzamFC

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga wamezidi kuimalisha kikosi chao baada ya kumsajili tena aliyekuwa golikipa wa Azam Deogratius Munishi ‘Dida’ hiyo kwa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.

Dida ambaye alianguka saini ya miaka miwili jana alisema kuwa kwa upande wake amefurahi kuona mchango wake watu wanauona japo kuna wengine hawausanimi.

Alisema kwa sasa ni mchezaji huyu baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya Azam.

Kipa huyo ambaye amekwisha idakia Simba, Azam amesema kuwa anaenda kufanya kazi yake kama kawaida Yanga na wanachama wanatakiwa kumpokea kwa mikono miwili na kumpa ushirikiano.

Alisema amefurahi kusajiliwa Yanga kwa kuwa wanashiriki michuano ya kimataifa na ana amini inaweza ikawa Yanga ndio njia yake ya kwenda kucheza nje ya nchi na kutimiza kiu yake ya siku nyingi ya kutoka nje ya Tanzania.

Dida ni moja ya wachezaji ambao walifungiwa na Azam katikati ya msimu uliopita kwa madai ya kula rushwa katika mchezo wao dhidi ya Simba katika raundi ya kwanza ambapo walifungwa bao 3-1.

Wachezaji ambao waliingia katika kashfa hiyo ni pamoja na mabeki wa timu ya Taifa Aggrey Morris , Erasto Nyoni na Said Morrad .
Hata hivyo Taasisi ya kuzuia Rushwa wilaya ya Ilala iliwaachia huru wachezaji hao ambao walikaa nisu msimu bila kucheza kwa madai kuwa hakuna ushahisi wa kutosha wa kuwa hukumu wachezaji hao.

Kwa upande wa Yanga Mwenyekiti wa kamati ya usajili Abdallah Bin Kleb alisibitisha kumsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa miaka miwili na kuongeza kuwa atakuwa kipa namba mbili wa klabu hiyo.

Alisema wameamua kuachana na Said Mohamed ambaye alikuwa kipa namba mbili na hawatamuongezea mkataba mwingine baada ya kumaliza mkataba wa miaka miwili kutokana na kutofanya vizuri msimu uliopita.

Kipa huyo alisajiliwa kutoka timu ya Majimaji ya Songea iliyoshuka daraja msimu wa mwaka 2010/11 akiwa kama golikipa namba moja wa timu hiyo.

Alisema Ally Mustapha ‘Barthez’ ambaye alisajiliwa dirisha dogo la msimu uliopita akitokea Simba atabaki kuwa kipa namba moja wa klabu hiyo akisaidiana na Dida.

Aliongeza kuwa timu yao inaitaji kupata wachezaji wenye uwezo na wazoefu kwa kuwa wanashiriki michuano ya klabu Bingwa mwakani na wanakutana na timu ngumu na zenye wachezaji wazoefu.

Mbali na Dida pia Yanga imemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Simba Mrisho Ngassa na kumuongezea mkataba kiungo wao ambaye alimaliza mkataba wake Haruna Niyonzima raia wa Rwanda.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version