Menu
in , , , ,

YANGA YAKUTANA NA UCHUNGU WA VAR

Tanzania Sports

Mechi za mzunguko wa hatua ya robo fainali ya klabu bingwa ya soka barani afrika zimeisha huku zikiwa zimeacha hisia tofauti kwa wadau wengi wa soka na michezo kwa ujumla barani Afrika. Wafuatiliaji wengi walishangazwa na mechi nyingi za awali kuisha huku zikiwa na matokeo ya kutokufangana na hata zilipochezwa mechi za marudiano matokeo hayakuwa makubwa sana. Tanzania kwa mara ya kwanza ilikuwa ina vilabu 2 katika hatua hiyo na kwa mara ya kwanza vilabu viwili vinayotoka katika kitongoji kimoja vilijikuta vinacheza hatua hiyo. Vilabu vya Yanga na Simba vilijikuta katika hatua hiyo. Kwa mara ya kwanza Yanga imefanikiwa kuingia katika hatua hiyo baada ya miaka mingi kupita bila ya kuweza kuingia katika hatua hiyo.

Mechi iliyosisimua zaidi ni kati ya Yanga na klabu ya Mamelodi Sundowns katika mechi hiyo hususani ya pili klabu ya Yanga ambapo katika kipindi cha pili mchezaji wao Aziz Ki alifunga goli na goli hilo lilikataliwa na refa kwa madai ya teknolojia ya VAR. uamuzi huo umegusa mashabiki wengi wa soka katika bara la afrika hadi kufikia kuweka dhana kwa kuwa rais wa chama cha soka barani Afrika ndiye mmiliki wa klabu ya Mamelodi Sundown basi yawezekana maamuzi ya refa yakawa yamechangiwa kiasi fulani na msukumo kutoka juu. Baada ya mechi hiyo refa amejaribu kujitetea lakini bado Imani ya  mashabiki wanaona kama maamuzi yake aliyafanya kwa makusudi kabisa. Hata kocha mkuu wa Yanga baada ya mechi hiyo wakati akiwa katika mkutano wake na waandishi wa habari alilaumu maamuzi hayo ya refa.

VAR kama teknolojia ya maamuzi ya kuchezesha mechi za soka kwa kupitia teknolojia ni jambo ambalo limekuja katika miaka ya hivi karibuni. Lengo kubwa ambalo lililengwa katika kuanzishwa kwa VAR ni kujaribu kupunguza makossa ya kibinadamu ambayo hupatikana na marefa katika kuchezesha mechi za soka. Teknolojia hii awali ililetwa na shirikisho la soka duniani katika mashindano ya kombe la dunia na mwanzoni ilionekana kama tu ingetumika katika mashindano ya kimataifa lakini kwa sasa teknolojia hiyo imesambaa maeneo mbalimbali duniani na ligi nyingi duniani zimeanza kutumia teknolojia. VAR hata kabla haijaanza kutumika ilikuwa inalaumiwa kwamba haitaleta ladha nzuri katika soka n ahata ilipoanza kutumika nayo imekuwa inalaumiwa tu sana.

VAR kwa sasa imekuwa inalaumiwa kwamba maamuzi yamekuwa yanachukua mda mrefu nab ado yapo kwa mujibu wa mwamuzi atakavyoamua. Halikadhalika VAR imekuwa inalalamikiwa kwamba inapunguza ladha za mechi kwani maamuzi yamekuwa yanachukua mda mrefu kuchukuliwa na hivyo kuna utamu Fulani wa asili wa soka ambao unapungua. Tatu VAR imekuwa inalalamikiwa kwamba kwa mara nyingi tu makossa yamekuwa yanafanyika kwa kuitumia na hivyo kufanya maamuzi ambayo sio sahihi kufanyika. Pia tokea imeanza kutumika bado maamuzi mengi 

Nchini Uhispania klabu ya Atletico Madrid ilikuwa ndio klabu ya kwanza kuzungumza hadharani kwamba hairidhishwi na matumizi ya VAR baada ya timu yao kushindwa kupewa penati katika mechi dhidi ya wapinzani wao Real Madrid na hiyo ilikuwa ni baada ya Casemiro kuushika mpira. Real Madrid ndio waliofuatia baada ya kushindwa kupewa penati baada ya mchezaji wao Vinicius Junior kuangushwa katika eneo la 18 lakini hawakupewa penati. Kocha wa Real Madrid aliwahi kusema kwamba moja ya matatizo ya soka kwa sasa ni kwamba VAR inaweza kutoa maamuzi ambayo sio sahihi. Hiyo ilikuwa mnamo disemba 21 mwaka 2023 wakati akizungumzia kadi nyekundu ambayo mchezaji wa timu yake alipewa ambapo alikuwa haridhiki nayo. Mchezaji ambaye alikuwa amepewa kadi hiyo nyekundu alikuwa ni Nacho.

Katika ligi kuu ya Ufaransa kocha wa Bordeaux alilaumu VAR na kuita ni utapeli baada ya timu pinzani ya NICE kupewa penati na hivyo kupelekea kushindwa mchezo huo. Maoni hayo klabu ya Bordeaux waliyatoa katika ukurasa wao rasmi wa Twitter na baadaye kocha wao mkuu kuyaongea tena wakati akiongea na waandishi wa habari.

Nchini Ujerumani nako VAR imekuwa inalaumiwa sana tu na vilabu tofauti kuanzia makocha mpaka kwa viongozi wa vilabu mfano mzuri ni Mnamo Agosti 2018 raisi wa klabu ya Bayern Munich alilaumu matumizi ya VAR katika ligi hiyo na akasema kwamba imetoa maamuzi ya hovyo katika msimu uliotangulia.

Nchini England nako VAR halikadhalika imekuwa inashutumiwa mara kwa mara kutoa maamuzi ambayo yanatia shaka Katika ligi kuu hiyo ya England mfano mnamo disemba 22 mwaka 2023 kocha wa Arsenal bwana Mikael Arteta alilaumu VAR kwamba inaharibu soka kauli yake ilikuja kufutwa na klabu yake.Kocha wa Liverpool bwana Jurgen Klopp aliwahi kulaumu VAR kwamba haifai.

Sio tu barani ulaya ambako VAR imelalamikiwa hata katika bara la Amerika ambako VAR inatumika katika baadhi ya ligi nako kumekuwa kunalalamikiwa vilevile. Mfano nchini Mexico kocha wa klabu ya Toluca Herman Crisante alilaumu sana matumizi ya teknolojia katika michezo. Na alisema kwamba ni kifaa kizuri lakini kinatumika vibaya.

Mwisho nitoe pole kwa mashabiki wa Yanga baada ya kutolewa katika hatua hiyo ya robo fainali kwa namna ambayo kwa namna moja ama nyingine haikuwa vizuri lakini uhalisia matumizi ya VAR hayajakuwa rafiki kwa timu nyingi ila hali hiyo isiwakatishe tamaa wajipange zaidi wana kikosi kizuri wakiboreshe ili walete ushindani zaidi mwakani.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version