Timu ya Yanga imejihakikishia nafasi ya pili ligi kuu Tanzania Bara baada ya kushinda goli 1-0 dhidi ya Lipuli FC katika uwanja wa Samora Iringa.
Ushindi wa Yanga inaizamisha Lipuli FC kucheza ligi daraja la kwanza ambayo imekusanya alama 44 nafasi ya 18.
Goli la Yanga limefungwa na David Molinga dakika ya 39 ambalo limeifanya Lipuli kuondolewa katika ligi kuu Tanzania Bara.
Huku Mtibwa Sugar ilipitia katika tundu la sindano baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting.
Hivyo Mtibwa Sugar inabakia katika ligi ikiwa nafasi ya 14 ikikusanya alama 45.
Mchezo mwingine mabingwa watetezi Simba wamepata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania magoli yote yakifungwa na John Bocco dakika ya 1 na 45 ya mchezo huo.
Kwa ushindi huo Simba inafikisha alama 88 ikiwa imefungwa magoli 21 na ikifunga magoli 78.
Matokeo mengine Singida United ambayo imeshuka daraja imefungwa magoli 2-0 dhidi ya Biashara United.
Mwadui FC ikiibamiza Kagera Suagar mabao 2-1 huku Tanzania Prisons ikitoa sare ya magoli 2-2 dhidi ya Azam FC.
Rasmi sasa Lipuli FC, Alliance, Ndanda FC na Singida United wao wameaga rasmi ligi kuu Bara na kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Huku Mbao FC itacheza ‘Playoff’ dhidi ya Ihefu FC ya Mbeya wakati Mbeya City ikichuana na Geita Gold.
Mshindi wa michezo hiyo atapata tiketi ya kubaki kwa Mbao FC na Mbeya City au kupanda daraja kwa Geita Gold na Ihefu FC.
Michezo hiyo itacheza Julai 29 kwa mkondo wa kwanza na Agusti mosi kwa mkondo wa pili.