USHINDI wa bao moja kwa nunge waliopata Yanga umepeleka shanngwe, nderemo na vifijo kwa vijana hao wa Jangwani na Twiga. Maelfu ya mashabiki wa Yanga na Simba waliufanya uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam ukose nafasi ya kuketi kutokana na uwingi wao. Shangwe za mashabiki wa timu hizo bado hazikuleta matunda haraka kwani walipaswa kuwa kuwa na subira hadi pale mmoja alipibuka kidedea. Katika mchezo huo ulitawaliwa na rafu za hapa pale pamoja na kasi ya mchezo vilikuwa vitu vilivyowaburudisha mashabiki wengi.
YANGA WANASHUKA AU WAMEGUNDULIKA?
Hilo ndilo unaloweza kujiuliza lakini ukweli wa mambo kikosi cha Yanga ni kama vile ortodha ya makombora ya masafa marefu kwenye uwanja wa vita. Kikosi chao kinapofanyiwa mabadiliko ni sawa na w asemavyo mtaani “ametoka nafuu, ameingia fadhali,”.
Kimsingi kuanzia safu ya ulinzi hadi ushambuliaji Yanga wanao wachezaji mahiri na wenye kumpa ahueni kocha wao Miguel Gamondi. Ahueni anayopata kocha huyo ni ule uzoefu wao na kufahamiana kiuchezaji kiasi kwamba inamfanya awe na kazi rahisi ya kuwapa maelekezo nini wanachotakiwa kufanya. Hata hivyo Yanga wanapaswa kujiuliza swlai hili kama wanashuka au wanapanda. Yanga imeonesha ubabe mfululizo lakini katika ushindi unaozua swali.
Yanga ni watemi wa simu misimu minne mfululizo na ushindi wake mnono ni ule wa mabao 5-1. Ni ushindi ambao kwa hakika mashabiki wa Yanga wanapenda kudumu nao na kuwatania wapinzani wao. Hata hivyo Yanga katika mchezo wa pili mfululizo dhidi ya Simba wanashinda kwa 1-0. Katika mechi iliyopita waliibuka kwa ushindi wa bao 1-0, hali kadhalika Derby ya Oktoba 19 nayo wamepata ushindi mwembamba. Kwahiyo kutoka kushinda ushindi mnono wa mabao matano hadi moja ni jambo ambalo linapaswa kujadiliana ukali wa kikosi chao bado upo au wapinzani wao wamegundua mbinu za kupunguza magoli ya Yanga?
Tumeona kwenye mchezo mkali wa Ligi Kuu dhidi ya Kengold jijini Mbeya Yanga walipata ushindi mwembemba kwa bao lililofungwa na beki wake wa kati Ibrahim Bacca. Vile mechi kadhaa wamekuwa wakipata ushindi mwembamba, ingawa Pamba Jiji ndiyo waliokumbana na kipigo kikali cha Wanajangwani hao.
SIMBA WA KUPANDA AU KUSHUKA?
Kutoka kufungwa mabao 5-1 hadi kufungwa mabao mawili katika mechi mbili dhidi ya Yanga yenye wakali na umahiri unaotikisa barani Afrika ni dhahiri Simba watakuwa na jambo la kutafakari kama wanapanda au wanashuka? Kwanini tunaweza kusema wanashuka, sababu wameshindwa kulipiza kisasi cha kufungwa mabao 5-1, kisha katikia mchezo wa Oktoba 19 unakuwa wa pili mfululizo kuchapwa na wapinzani wao. Hii pia ni mara ya nne mfululizo Simba kufungwa na Yanga.
Endapo Simba wanapanda maana yake wamegundua mbinu zinaztumiwa na Yanga hivyo wapo tayari kmwa mapambano mengine. Hili hililikuwa jaribio la pili kwa Simba angalau kufuta uteja kwa Yanga katika michezo ya karibuni lakini wameshindwa kufurukuta na kujikuta wachapwa 1-0 huku likiwa limetengenezwa na nyota wake wa zamani Cletous Chama. Katika mtindo wao ‘total football’ kila safu inafanya kazi kwa mfumo wa kutgemeana. Ndani ya Simba hakuna mchezaji wa kutegemewa pekee hivyo kila anayepewa nafasi au kupangwa anakuja kutekeleza majukumu ya pamoja. Upo wakati walicheza kujazana katikati ya dimba yapata yadi 30 kutoka eneo lao la 18 kuelekea lango la adui. Ni dhahiri kikosi hiki kinahitaji muda zaidi pamoja na kutumia nafasi nzuri.
KOMBINENGA MATATA
Simba wana kombinesheni kule nyuma, yupo Che Malone na Hamza. Wawili hawa wanaunda safu kali ya mabeki na kuimarisha timu yao. Uwezo wao wa kucheza kwa kubadilishana nafasi au double centerhalf umewafanya wawe wanashirikiana muda wote wa mchezo na kufuta makosa ya kila mmoja. Yanga wana kombinenga mbili matata;- safu ya ulinzi wanaye Ibrahim Bacca na Dickson Job ambao makali yao pia wamehamishia katika kikosi cha Taifa Starsa.
Vijana wanapiga kazi si kitoto. Hali kadhalika safu ya ushambuliaji ina kombinenga ya Aziz Ki,Pacome na Dube, wakati nyingine ni Clement Mzize,Chama na Kennedy Musonda. Katika kombinenga hizi wachezaji wao wana ujuzi na ufundi mzuri endapo mwalimu anawapanga kama watatu mbele. Simba wana wanatafuta kombinenga yao katika safu ya ushambuliaji kwani Leonel Ateba ameonesha wazi yupo tayari kwa mapambano na bila shaka kocha Fadlu David hajutii kumpanga mshambuliaji huyo. Lakini nyuma yake acheze na nani kati ya Ahoua, Kibu Dennis na Edwin Balua. Hiki ni kibarua cha Fadlu David kuhakikisha anakuwa na kombinenga matata ya kutetekeza timu pinzani.
KIBARUA CHA FADLU DAVID, MIGUEL GAMONDI
Kocha wa Simba amepoteza mchezo wa pili dhidi ya Miguel Gamondi. Wakati Simba wakichapwa 5-1 yeye hakuwa kocha wao. Lakini wakati Simba walipokubali vipigo vya 1-0 mara sasa yeye ndiye kocha mkuu. Fadlu David anatakiwa kukuna kichwa na kuongeza makali katika mbinu anazotumia dhidi ya Yanga. Naye kocha wa Yanga Migeul Gamondi anacho kibarua kikubwa kwani ni mchezo wa pili anashindwa kupachika mabao mengi dhidi ya Simba ya Fadlu David. Gamondi amemfunga Fadlu mara mbili kwa 1-0, lakini namna ushindi wake unavyopatikana ni dhahiri mbinu zake zimegunduliwa ama wanajua namna ya kupasuana vichwa.