MARA mbili hivi mwandishi mmoja wa michezo kutoka nchini Ghana amewahi kuelezea namna Kocha wa Wydad Casablanca, Rhulani Mokwena anavyomhusudu Stephan Aziz Ki pamoja na Clement Mzize. Mojawapo ya matamanio yake ni kufanya kazi na nyota hawa wawili. Hata hivyo shauku hiyo alianza nayo alipokuwa klabu ya Mamelodi Sundowns na kisha Wydad. Hata hivyo mar azote hajafanikiwa kuwanunua wachezaji hao kutokana na Yanga kukataa ofa zozote zilizoletwa kwenye klabu hiyo kwa ajili ya huduma ya wachezaji hao. Uongozi wa Yanga chini ya Injinia Hersi Said umeweka wazi kuwa hauna mpango wa kuwauza nyota wake.
Kilio cha Mokwema Wyad
Ukiangalia mwenendo wa Wydad kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya safu ya ulinzi na safu ya ushambuliaji. Kocha Mokwema alifahamu kuwanunua wachezaji hao wawili ilikuwa ni kuongoza ufanisi wa timu yake. Timu za Afrika kaskazini zinakabiliwa na changamoto ya wachezaji wenye vipaji na makocha.
Ni sababu hii makocha kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara wakiwemo Fadlu Davids na Rhulani Mokwema wamefanikiwa kupenya katika soka la Afrika kusini kwa kufanya kazi na vilabu vikubwa. Wyad inafahamu kuwa endapo itafanikiwa kuwanunua wachezaji hao basi itakuwa hatua nzuri kwenye kikosi chao. Kwenye moja ya mechi Wydad walipigwa mabao matano na wapinzani hao, hali ambayo ilikiweka katika mazingira magumu kikosi chao. Kuwakosa Clement Mzize na Stephan Aziz Ki ni kitu ambahco bado kinamsikitisha kocha Rhulani Mokwema.
Mashuti ya Lampard, Rooney EPL
Mabao mawili kutoka kwa mshambuliaji Clement Mzize na moja la Stephan Aziz Ki yaliwapa ushindi Yanga wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe kwenye mfululizo wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa ushindi huo Yanga wamepata pointi nne na mabao matano. Lakini namna magoli yalivyofungwa ndivyo inakuwa gumzo. Katika ulimwengu wa kandanda mashabiki wanamfahamu kiungo mshambuliaji wa Chelsea,
Frank Lampard pamoja na aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.wachezaji hawa wawili walikuwa wanasifika kwa uwezo mkubwa wa kupiga mashuti makali kwenye lango la adui. Magoli mengi waliyofunga yalitokana na mashuti makali mno. Shuti la Clement Mzize dhidi ya TP Mazembe lina hadhi ileile ya Frank Lampard na Wayne Rooney.
Kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Clement Mzize aliwapunguzia presha mashabiki wao baada ya kufunga bao la kwanza kwa Yanga na kufanya matokeo yawe 1-1.
Namna alivyofunga bao lenyewe, kasi aliyotumia, namna alivyomwangalia golikipa wa TP Mazembe na kuachia mkwaju mkali uliokwenda moja kwa moja kimyani. Ufungaji wa bao hilo bila shaka yoyote utaendelea kuwalinza viongozi wa Wydad Casablanca pamoja na kocha Rhulani Mokwema.
Yanga watadumu kukaa fedha za Waarabu?
Katika bao la kwanza alilofunga kwenye mazingira magumu na yasiyotarajiwa, yanaonesha kuwa Clement Mzize ni hazina ambayo Yanga wanatambua ndiko mahali penye mafanikio yao. Yaani miguu ya mshambuliaji huyo ndiyo kitu ambacho kinapendwa na mashabiki wa Yanga ambao watashangazwa siku watakapouzwa.
Ni miguu ambayo imeongezewa uimara wa kimwili na kupevuka kwa maarifa yake kiwnajani. Lakini vilevile inaonesha Mzize ni hazina ambayo wakubwa wanaitazama kwa jicho la matamanio na huenda ukafika wakati Yanga wakashindwa kujizuia kama walivyofanya wenzao Simba kwa kuwauza Luis Miquissone kwenda Al Ahly ya Misri na Cletous Chama aliyesajiliwa na Berkane ya Morocco. Mwisho wa siku swali linabakia, Yanga wataendelea kuzigomea fedha za Waarabu au watafika bei? Hilo ni suala la muda kwani wanaye mshambuliaji mwenye mashuti kama Old Traford kule Manchester na Stamford Bridge hapa London. Mzize anatukumbusha mbali sana.