Menu
in ,

Yanga, Simba, Arsenal Ndani Ya Tukio Moja

Mwezi wa nane siku zote unakuwa ni mwezi wa michezo duniani, isingekuwa COVID-19 ligi mbalimbali zingeanza mapema mwezi huu.

Baada ya Korona kila kitu kimebadilika na sasa wiki ya michezo inaelekea mwishoni mwa mwezi huu.

Huku ligi mbalimbali zikianza mwezi Septemba, Bongo itaanza tarehe 6 na EPL ikianza Sepetemba 12.

Haya hapa ni matukio matatu makubwa kabisa ya kimichezo duniani kote hasa hapa Tanzania.

Baada ya kuona tukio la kwanza la Simba Day lililofanyika Agusti 22 ambapo Simba walicheza na Vital O ya Burundi sasa kuna mengine yanakuja.

1. La kwanza ni siku ya Mwananchi ambayo wiki yake imeshaanza na kilele chake kitakuwa tarehe 30 mwezi huu pale uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Wiki hii mara nyingi inakuwa na mamabo mengi wakianzia kuhudumia jamii kuingia katika Hospitali, Shule pamoja na sehemu mbalimbali za jamii kuweza kutoa huduma.

Baada ya hapo kinachofuata uwanjani ambapo kilele ndio kama nilivyokieleza hapo juu.

Siku ya kuingia uwanjani kunakuwa na mbwembwe nyingi moja wapo kutambulisha wachezaji wapya na wazamani watakao hudumu kwa msimu mzima.

Yanga wamemchukua Harmonize kutumbwiza siku ya kilele cha timu hiyo huku akitoa wimbo kwa ajiri ya timu ya Yanga.

Pili kuangalia viwango vyao baada ya mechi kuchezeka kila mmoja atakuwa anatoa maoni yake juu ya sajili hizo.

Yanga wameialika Aigle Noir Makamba ya nchini Burundi ambayo ilishikanafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu nchini humo.

Wakati huo huo wanaenda kumaliziai usajili wa nyota wao wapya na kuanza msimu mpya baada ya kuwafyagia wachezaji 16 msimu huu.

Swali ni kwamba viwango vya nyota wao wapya vita akisi uwezo ambao wanachama wa Yanga wanahitaji .

Hayo yote tuyaache hadi pale tutakapoona wanacheza uwanjani na kuonesha kiwango au kutoonesha kiwango.

2. Tukio la pili lile la ngao ya jamii, hii ilikuwa ifanyike Agusti 29 mwaka huu lakini imebadilishwa na kufanyika Agusti 30 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha.

Hapa sasa watakutana bingwa wa kombe la FA na aliyeshika nafasi ya pili kombe la FA ambapo Simba itaumana na Namungo.

Ina maana tukio hilo litakuwa na ufunguzi wa pazia la ligi kuu Tanzania Bara.

Timu zote hizi zimetesti mitambo kwa mechi za kirafiki, Simba walicheza na Vital O wakati Namungo walipepetana na Azam.

Tukio kubwa lingine lile la ngumi kati ya Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ dhidi ya Twaha Kiduku litakalopigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Hili ni pambano la kufa au kupona ‘Do or die’ kutokana na mechi ya kwanza hakupatikana mshindi  na sasa inatakiwa apatikane.

Wengi wao hawakuridhika na mchezo wa awali waliotoa sare sasa wanataka kurudiana na wahakikishe nani atatoboa.

Kila mmoja ana mashabiki wake na uwezo wake unafahamika kikubwa kujaa uwanja wa Uhuru na kuangalia mpambano huo.

Ngumi zimerudi kuwa na thamani kubwa sana hivi sasa, niseme wazi kuwa Hassan Mwakinyo ameirudisha ngumi katika ramani.

Ukubali au ukatae huo ndio ukweli wa mambo na sasa kila mmoja ukimueleza juu ya ngumi atakuwa anachakuhadhithia ubora wa Mwakinyo pamoja na mabondia wengine .

Hii yote ni mitoko yaani wale wala bata ndio sehemu zetu sahihi sahihi za kuelekea kuanzia Simba Day ambayo imepita Siku ya Mwananchi, Dulla Mbabe dhidi ya Twaha Kiduku nakupa ‘code’ za kufurahia siku hizo zote.

Mabingwa wa Kombe la FA
Mabingwa wa Kombe la FA

Huko duniani Arsenal watapepetuana na Liverpool katika kuwania ngao ya hisani ama ngao ya jamii kama wengi wanavyoita.

Hii inatumika kurudisha hisani kwa jamii wanakusanya fedha zitakazopatikana zinaenda katika mfuko wa kusaidia jamii.

Ndio maana ya mpira au michezo imejaa kila mahali na kusaidia kila kitu kuanzia kupata ajiria kuhudumia jamii pamoja na harakati nyingine.

Bila kusahau tukio la usajili hii ya mwisho kabisa Arsenal wameramba dume kwa Gabriel dos Santos Magalhães, beki kitasa kabisa mwenye miaka 22, Manchester United nao walitaka huduma ila ameichagua Arsenal.

Nawaona watu wa Manchester United wakianza kuguna na kusema huyu mtu anaishabikia Arsenal.

Kunatukio lingine kubwa nimelisahau basi liweke hapo katika maoni yako chini ili tuendelee kuhesabu siku ya mitoko.

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version