Menu
in

Yanga Na Simba Hazichezi Ugenini

Hivi kuna anayeamini kuwa Yanga na Simba zinakuwa ugenini zikicheza ligi kuu Tanzania Bara.

Huenda ukajibu kimyakimya vile unavyohisi moyoni juu ya swala hili lakini cha kufahamu kuwa Yanga na Simba kwa Tanzania hazichezi ugenini.

Timu hizi zinacheza ugenini pindi zinapoenda kimataifa tu ila sio ligi ya ndani au katika kombe la Mapinduzi ambalo huchezwa kule Zanzibar.

Ninayofuraha kubwa kusema kuwa hizi timu kwa taifa la Tanzania kama utamaduni tu, mtoto anapozaliwa huko Songwe au Ilula anakuwa na machaguo mawili tu Yanga au Simba baada ya kupata fahamu.

Ndio maana Yanga au Simba ikienda kucheza Lindi dhidi ya Namungo 99% ya uwanja inajaa jezi za timu husika na mashabiki wanazishabikia timu hizo.

Hivyo itabakia kuwa nadhalia Yanga inaenda kucheza ugenini katika makaratasi ila uhalisia zinaenda kucheza nyumbani popote pale Tanzania.

Afisa Habari Wa Azam FC Thabiti Zakaria ‘Zakazakazi’ amelithibitisha hili na kusema kuwa timu hizo hazina ugenini kwa soka la Tanzania.

Zakazakazi ameitolea ufafanuzi alipoulizwa swali juu ya timu ya Azam FC kupoteza mechi 6 ugenini huku mbili wakizipoteza katika uwanja wao wa nyumbani katika msimu uliopita.

” Yanga na Simba hazina mechi za ugenini kwa Tanzania pindi zinapocheza na timu nyingine hivyo hazina presha kama ilivyo Azam inapocheza nje ya uwanja wake,”alisema.

Tanzania Sports
VPL

Yanga na Simba zimejijengea ufalme ambao inahitajika nguvu ya ziada kuweza kuvunja utawala huo, ambao umewekwa kwa zaidi ya miaka 85.

Yanga imeundwa mwaka 1935 lengo lao lilikuwa kujifurahisha na kutoa burudani, wakati inaanzishwa walichanganyika wazawa na wageni.

Baada ya kuvurugana mwaka 1936 wale waliokuwa wanaunda Yanga walienda kuunda timu nyingine iliyoitwa Sunderland ambayo kwa sasa Simba SC, hiyo ilikuwa mwaka 1936 na ndipo ilipoundwa Simba .

Mizizi waliyoiweka tangu wakati huo hadi sasa hakuna atakayeweza kuibomoa hadi viongozi waliopo katika timu nyingine waupende mpira kuliko mapenzi ya timu hizo.

Angalia mchezo uliochezwa katika uwanj a wa Jamhuri mkoani Morogoro Simba ilipocheza na Mtibwa Sugar, 98% ya mashabiki walikuwa Simba huku waliobaki walikuwa wa timu pinzani.

Kwa pale uwanjani unasema asilimia mbili zilkuwa za Mtibwa Sugar ila uhalisia waliokuwa wanafurahi walikuwa wa Yanga.

Hii ndio Tanzania na huu ndio utamaduni tuliouweka kwa miamba ya Yanga na Simba.

Wenzetu Ulaya mtu anapozaliwa katika kitongoji chake huwa anaishabikia timu iliyopo hapo, mfano  ukizaliwa Tukuyu wewe utakuwa Tukuyu Stars.

Ila huku kidogo tunaenda na mifumo yetu ambayo inaraha yake kwakweli.

Sio kila jambo liigwe kuna mengine yanabakia kama yalivyo na itakuwa historia kwa wengine.

Kujaa kwa mashabiki katika majukwaa uwanjani ni kiashiria tosha kabisa kuwa soka letu linapendwa lakini pia Simba na Yanga zinapendwa kweli.

Zinapoenda mikoani hizi timu ndio utashangaa mwenyewe namna wanavyomiminika. 

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version