Sakata ambalo linaendelea hivi sasa juu ya usajili wa Bernard Morrison ambaye anaitumikia timu Yanga huku watani wao wa jadi Simba ikimvutia kasi.
Sauti ambayo inatembea katika mitandao ya kijamii ya mchezaji huyo juu ya kupewa dola mia tano na timu ya Simba SC lengo atie saini msimu ujao atoe huduma yake huko wakati huo Yanga wanaonekana wamempa mkataba wa miaka miwili.
Huenda likawa jibu la pamoja juu ya maswali yanayoendelea wengi wakiamini Simba wanaweza kuadhibiwa juu ya sintofahamu hiyo na imekuwa mjadala mkubwa sana.
Iko hivi Yanga walimsaini mkataba wa miezi sita katika dirisha dogo la usajili bahati nzuri ameweza kufikia kiwango kizuri na hakuna mchezaji mwenye kiwango kikubwa kama yeye.
Baada ya kuona mazuri yake kampuni ya GSM ambao ndio wadhamini wa Yanga wamempa mkataba wa miaka 2 ili aitumikie timu hiyo ushahidi wa mkataba tuliona akitambulishwa huku akishika mkatba lakini pia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni hiyo alisema kuwa wamemsajili kwa miaka miwili.
Tamthiliya iliyo sasa juu ya kinachoendelea ni kwamba kuna wakala mmoja ambaye amejinasibu kuwa anatoka Simba na lengo kumshawishi ajiunge na timu hiyo.
Bila shaka ninayanukuu maelezo ya Benard Morrison, huku akidai kuwa alitaka kurejea Afrika Kusini kucheza huko.
“Kuna majadiliano yalikua baina yangu na Orlando Pirates na Cape Town City kwa kua niliamua kurudi Afrika ya Kusini”
“Kuna mtu alikuaja akasema yeye ni wakala na ametumwa na Rais wa Simba na akaniletea ofa mie nikamjibu acha niangalie baadhi ya vitu kisha nitawarudia”
“Anataka kunishawishi zaidi, kuna siku akaja na dola 10,000 kisha akanipa mimi dola 5,000 na yeye akachukua 5,000 Kama sehemu ya kazi yake ya ushawishi”
“Sikuwaomba hiyo pesa na kama wanaitaka nitairejesha kwa sasa mimi ni mchezaji wa Yanga kwa miaka miwili”
“Ananipigia simu sana na kuniuliza kama bado nitasaini Simba”
Hiyo ni sauti ambayo inaendelea katika mitandao ya kijamii pamoja na Waandishi maarufu wa habari inamambo mengi hasa ukiangalia maoni yao chini ya akaunti zao za Instagram.
Maswali ya kujiuliza yapo mengi, je timu ya Simba itaweza kuadhibiwa endapo Yanga wakipeleka vielelezo ndani ya Shirikisho la mpira wa miguuu Tanzania (TFF) ?
Vipengele vinakuaje kama timu ikiongea na mchezaji akiwa katika mkataba na timu nyingine.
Ni muda gani wa mkataba timu inaruhusiwa kuongea na mchezaji .
Tuanze kujibu maswali matatu kisha tuendelee kama nafasi ipo ya kuyaelezea.
Mosi, kipengele cha mkataba kinasema mchezaji haruhusiwi kuongea na timu nyingine kama amebakisha mkataba wa mwaka mmoja au zaidi.
Endapo mchezaji anahitajika timu B na timu A ana mkataba unaozidi miezi sita timu B inaruhusiwa kuongea na timu A ili ivunje mkataba na mchezaji na aitumikie huko.
Ila kwa bongo sijawahi kuona timu inavunja mkataba kwa kuogopa gharama kubwa ya uvunjwaji wa mikataba.
Mfano Simba wakimuhitaji Papy Tshishimbi wanatakiwa wakae meza moja na uongozi wa Yanga ili waangalie namna ya kuvunja mkataba huo.
Pili mchezaji anaruhusiwa kuongea na timu nyingine endapo mkataba wake una miezi sita.
Tatu endapo timu itaongea na mchezaji moja kwa moja bila ya kufuata utaratibu wa yaliyoelezwa hapo juu inaweza kuchukuliwa hatua.
Ndio maana Makamo Mwenyeikti wa Yanga Fredrick Mwakalebela aliomba radhi baada ya kusikika anamtaka Clatus Chama wa Simba.
Turudi katika ‘point’ yetu Simba haiwezi kuadhibiwa inawezekana wakati ushawishi huo unafanyika ilikuwa ndani ya miezi sita yaani kabla hajasaini mkataba mwingine na Yanga.
Lakini pia endapo Simba wakimkana huyo anayejiita wakala wa kumshawishi Morrison wataadhibiwa vipi? Huyo anayejiita wakala naye akikana kuwa hajawahi kutumika na Simba ili ajilipue na msala ukabaki kwake inakuaje hapo ?
Tambo ambazo zinaendelea kwa mabosi wa timu zote mbili wanasema kuwa wanaweza kumsajili mchezaji yoyote je ni wataweza kweli kama wanashindwa kukaa meza moja na kuvunja mkataba wa mchezaji?
David Morrison amefunga magoli 3 ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara pamoja na goli moja katika kombe la Shirikisho au kombe la FA.
Nyota huyo alisajiliwa katika dirisha dogo la usajili na alianza kufunga January 26 mwaka huu dhidi ya Tanzania Prisons katika kombe la ‘Azam Sports Federation Cup’ (ASFC).
Mechi ya pili ilikuwa dhidi ya Lipuli FC kutoka Iringa na akafunga katika mchezo huo ambao ulikuwa wa ligi kuu Tanzania Bara hii sasa ilikuwa Februari 5.
Goli lake la pili katika mchezo wa VPL akafunga dhidi ya Mbeya City Februari 11.
Goli lake la tatu alilifunga dhidi ya Simba Machi 8 uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Una swali lolote juu ya hili unaweza kuacha maoni yako hapo chini utajibiwa.