Timu ya Yanga inatajwa kuwa ni mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa kuchukua mara 27 huku mpinzani wake Simba ikichukua mara 21.
Hayati Benjamini William Mkapa alichaguliwa kuhudumu kama Rais wa Tanzania mwaka 1995 baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi.
Kwa wakati huo Simba ndio wa kwanza kufungua pazia kwa kulichukua msimu wa mwaka 1995.
Baada ya hapo Yanga wakachukua mara tatu mfululizo yaani kuanzia msimu wa 1996-98.
Ikarejea tena kulichukua mwaka 2002 na mwisho mwaka 2005 ikawa ndio mwisho wake.
Simba ambao ndio wapinzani wa jadi wa Yanga katika soka la nchi hii imechukua mara nne yaani 1995, 2001, 2003 na 2004.
Mtibwa Sugar ambayo imeweka historia ya kuchukua ubingwa wakati wa mwisho wa karne na kufungua mwanzo wa karne.
yaani Mtibwa nao walichukua mara mbili msimu wa 1999 na 2000.
Kuna watu watakuwa wamechanganyikiwa kuona katika kipindi hiko mbona mara 11 na sio mara kumi ?
Ule msimu wa 1995 yaani ulikuwa msimu wa kutokea 1994-95 na mwaka huo ndio Mkapa ameingia madarakani yaani Oktoba 1995.
Tunafahamu msimu unaisha wakati unaingia msimu mwingine mwaka ule ule.
Mfano mwaka huu msimu umeisha mwezi Julai na unaofuata utakuwa Septemba mwaka huo huo.
Kwa utaratibu huo Yanga imechukua mara tano, Simba mara nne na Mtibwa mara mbili.
Yanga na Simba ndio timu kubwa Afrika Mashariki na kati huku zikipendwa na watu wa rika mbalimbali.
Hayati Mkapa ambaye alitengeneza uwanja mkubwa wa taifa habari zinasema kuwa alikuwa anaishabikia Yanga.
Baada ya harakati zote Mwanahabari huyo Mungu amemuita na kupitia michezo tunamkumbuka kwa aina hiyo.
Wakati zama zinaendelea alipokea kijiti Rais mstaafu Jakaya Kikwete naye alikuwa na mambo yake na alionesha wazi anapenda sana michezo.
Kule England anashabikia Newcastle United ila hapa bongo yeye ni mfuasi waYanga na katika kipindi chake bado timu hiyo imetawala kuchukua ubingwa wa ligi kuu Bara mara nyingi ikichukua 6 wakati Azam imechukua mara moja na Simba ikichukua mara tatu.
Yaani iko hivi 2005-06, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13, 2014-15.
Huku Simba ikichukua 2006-07, 2009-10 na 2011-12 wakati Azam FC ikichukua mara moja msimu wa 2013-14.
Katika utawala wa Magufuli ambapo tayari miaka mitano imeshakatika Simba inaongoza kwani imechukua mara tatu huku Yanga ikichukua mara mbili.
Iko hivi Yanga imechukua msimu wa 2015-16 na 2016-17 huku Simba ikichukua 2017-2020.
Nyongeza Yanga iliwahi kuchukua mara tano mfululizo kipindi cha baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuanzia 1968-1972.
Wakati Simba walilipa mwaka 1976-1980 kitu pekee ambacho Yanga anadaiwa kwa Simba kufungwa goli 6 mwaka 1977.
Lakini pia tangu ligi ya Tanzania ianze kutambuliwa kama ligi kuu na kipindi hiko ilikuwa katika utawala wa Nyerere Yanga imechukua mara nane.
Simba ikiizidi Yanga kwa kuchukua mara tisa kwa mwaka mmoja mmoja wamechukua Pan Africa, Cosmopolitan na Mseto.
Wakati wa Rais Mstafu Mwinyi Yanga ilitawala tena kwani imechukua mara sita yaani 1985, 1987, 1989, 1991,1992 na 1993 , Tukuyu Stars ya Mbeya nayo ilichukua mwaka 1986, Costal Union ya Tanga ilichukua mwaka 1988 wakati Simba ikichukua 1990 na 1994.
Historia za timu hizi zinavutia kweli, siku mgogoro waviongozi ukiwa upande waJangwani msimu unaofuata unahamia kwa Simba.