kama hiyo haitoshi wazalendo hawa waliendelea kujikusanya kwa pamoja na kuanza mishemishe za kusaka uhuru wa nchi hii, na ndipo tarehe 9 disemba mwaka 1961 tanganyika ikapata uhuru, hivyo kama tutazungumzia uhuru wa taifa hili basi hatusiti kwa namna moja au nyingine kuitaja yanga, na kwa heshima yake inatakiwa unapoitaja yanga kama umekaa basi unatakiwa usimame.
MAFANIKIO.
yanga ndio timu iliyochukua ubingwa wa ligi ya bara mara nyingi zaidi, na ndio klabu inayofahamika zaidi kitaifa na kimataifa kwa sababu ndiyo klabu iliyopeperusha vizuri bendela ya taifa hili la tanzania nje ya mipaka.
na kama hiyo haitoshi yanga ndiyo klabu yenye washabiki wengi zaidi ndani na nje ya nchi, ndani ya africa na dunia kwa ujumla.
na pia yanga ndiyo klabu ya mwanzo hapa nchini au hata afrika mashariki kwa ujumla kwa kuwa na makao makuu sambamba na uwanja wa mazoezi ambao unajulikana kwa jina la Kaunda, jina la muasisi na mpigania uhuru mwengine wa taifa la zambia muheshimiwa keneth kaunda.
mfumo huu wa kuwa na makao makuu pamoja na uwanja wa mazoezi ni wa timu kubwa barani ulaya na dunia kwa ujumla.
yanga pia ndio timu ya kwanza kuwa na gazeti hapa nchini. gazeti hili linajulikana kama “Yanga imara”. lilipotoka katika wiki ya kwanza liliuzwa takriban nakala 50,000 nchi nzima na baadhi ya nchi za jirani.
mfumo wa kuwa na gazeti la klabu pia umeigwa na baadhi ya klabu hapa nchini lakini unaonekana kusua sua katika mauzo na hata ukisoma nakala ya gazeti lao utakuta limejaa matangazo ya waganga tu.
yanga ndo timu pekee iliyowahi kuuza mchezaji nje ya nchi na kung’aa katika vilabu mbali mbali barani ulaya, mchezaji huyu alijulikana kama Nonda Shaaban al maarufu kama “papii”.
nonda ambaye aliwahi kutamba na mashujaa hawa wa jangwani amepata kuchezea vilabu kama val profesional ya south africa, FC zuurich ya uswis, stade rennes na AS monaco zote za ufaransa, AS roma ya italia akicheza pamoja na francesco totti, blackburn ya uingereza na sasa anakipiga katika klabu ya galatasaray yenye maskani yake katika uwanja wa ali sami yen nchini uturuki.
na hapa ndipo tunapoitofautisha yanga na vilabu vingine vya soka hapa nchini ambavyo wachezaji wake huuzwa burundi, rwanda na uarabuni ambako hakuna soka la ushindani.
pia yanga ndo timu ya kwanza hapa nchini kuongozwa na rais.
pia yanga ndo timu ya kwanza kuwa na mfumo wa wanachama kuwa wana hisa wa klabu kama timu nyingi za ulaya, hivyo kumfanya kila mwanachama kuhusika kikamilifu katika mipango na malengo ya klabu, tofauti na majirani zetu ambao mfumo wao wa uongozi haueleweki na hata mishahara ya wachezaji wanalipwa kimkanda mkanda na inafika kipindi mchezaji anakaa miezi minne hajalipwa mshahara mwisho wanatimkia kucheza ligi za mchangani.
MAFANIKIO NJE YA MIPAKA.
Yanga kama yanga ndo timu pekee iliyowahi kuchukua kombe linalotambuliwa na shirikisho la soka barani afrika CAF na shirikisho la soka duniani FIFA. itakumbukwa tu yanga waliwafunga express ya uganda kwa goli 3-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la klabu bingwa afrika mashariki na kati na mechi ya fainali walitakiwa wakipige na SC villa.
yanga waliwacharaza bila huruma SC Villa goli 2-1 katika uwanja wa nakivubo kwenye mechi ya fainali ya kombe lililokuwa na msisimko kipindi hicho la klabu bingwa afrika mashariki na kati na kupelekea serikali ya tanzania kutuma ndege mpaka katika uwanja wa ndege wa entebe kwenda kuwachukua waheshimiwa waliolitoa taifa kimasomaso yaani yanga.
hivyo kuweka adabu kwa waganda ambao hawawezi kuisahau yanga maishani mwao.
yanga katika mechi hiyo iliwakilishwa na:
1) steven nemes
2) mwanamtwa kihwelu
3) keneth mkapa
4) willy mtendamema
5) issa athuman
6) method mogella
7) steven mussa
8) hamis thobias gagarino
9) said mwamba kizota
10) mohamed husein chinga one
11) edibily jonas lunyamila
pia yanga walikuwa na bunduki nje kwenye benchi kama willy martin, rifat said, aboubakar salum “sure boy” david mwakalebela “MP” na wengine wengi ambao walikuwa ni miiba kwa waganda.
katika mechi hiyo mnamo dakika ya 81 beki mahili wa villa na timu ya taifa ya uganda marehemu Paul Hasule alivua jezi na kutoka nje kwa kile ambacho mwenyewe alikiri kuwa ameshindwa kumkaba winga wa yanga edibily lunyamila, lakini alilazimishwa na kocha wake kumaliza mechi kutokana na aibu iliyokuwa inawakabili.
kutokea hapo waganda walitekwa akili kutokana na kabumbu safi lililoonyeshwa na yanga na kupelekea daladala nyingi nchini humo kuandikwa majina kama “lunyamila trans” “kizota trans” au hata wengine walifuta majina ya salon zao na kuandika “gagarino hair salon” na mpaka leo hii waganda wakisikia timu kutoka tanzania inakwenda huko wanauliza “je ni yanga?”.
na baada ya ushindi huo mwanamuziki nguli wa afrika marehemu kabasele yampanya al maarufu kama peppe kalle alitunga wimbo wa kuisifia timu hiyo baada ya kuonyesha dhahili kiwango cha juu na kuvutia washabiki wengi wa soka kitu ambacho hakijawahi kufanywa na klabu yoyote nyingine hapa nchini.
HISTORIA ISIYO SAHAULIKA.
mwaka 1972 katika pambano la watani wa jadi lililokuwa lifanyike katika uwanja wa taifa, watanzania walishuhudia kituko cha mwaka pale kilabu ya simba ya dar es salaam ilipoishia chang’ombe na kugeuza basi na kurudi katika mtaa wa msimbazi na kufanya timu ya yanga ya tanzania kupewa ushindi baada ya mpinzani kufyata mkia na kutokomea vichakani.
mnamo pia tarehe 13 mwezi novemba mwaka 1991 katika uwanja huo huo wa taifa timu ya yanga ya tanzania waliingia uwanjani na basi la sharuksi lililokuwa likimilikiwa na mfadhili wa yanga wa kipindi hicho marehemu abbas gulamali, timu ya soka ya simba ya dar es salaam iliweka mpira kwapani wakati wa mapumziko na kutokomea kusiko julikana.
na kauli hii ya kuweka mpira kwapani iltolewa na mtangazaji aliyekuwa anatangaza soka redio tanzania siku hiyo ndugu Charles Hillary, na magazeti kama motomoto, mfanyakazi, uhuru na mzalendo ya kipindi hicho yalipambwa na kichwa kikubwa cha habari “mgonjwa atema dawa”.
na kuweka mpira huko kwapani kulifuatia vipigo mfululizo vya august 31, october 9 lakini hii iltanguliwa na kipigo cha Said Sued “Scud” cha mei 18.
baadhi ya mashujaa waliowahi kukipiga yanga miongoni mwao ni rifat said, joseph katuba, peter manyika, anwar awadh, salum kabunda “ninja”, godwin aswile “baba subi” au scania, said zimbwe, thomas kipese, joseph lazaro, omar husein, costantino kimanda, sanifu lazaro “tingisha” na wengine wengi.
hili nililokupa hapo ni tone tu la maji, ila bahari ntakupa siku nyingine.
na hii ndo yanga, klabu bora kabisa hapa nchini, isiyotishwa na kelele, adhabu wala faini yoyote.