Menu
in , ,

Yanga inataka ubingwa bila usajili makini?

Tanzania Sports

USAJILI wa dirisha dogo la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lilifungwa jumanne wiki hii, baada ya klabu kuongeza wachezaji wapya kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao.

Dirisha hilo lililofunguliwa Novemba 15 mwaka huu, kila klabu ilitumia nafasi ya kusajili wachezaji wapya kutokana na ufungufu uliojitokeza katika vikosi vyao kwa michezo 10, waliyocheza duru la ligi hiyo.

Miongoni mwa timu zilizozama kufanya usajili ni Simba kwa ajili ya kukiboresha kikosi chao, kilichoonekana kulegalega katika idara ya ushambuliaji.

Simba ilionekana kutokuwa na washambuliaji wenye uchu wa kufunga mabao, licha ya kwamba ilifanya usajili ulionekana kama ungekuja kuisaidia timu hiyo, kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara.

Washambuliaji wa timu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’ Pape N’daw, Simon Sserunkuma na Hamis Kiiza walionekana kushindwa kuleta mashambulizi na ilikuwa lazima Simba kuwaongezea nguvu kwa kufanya usajili katika kipindi cha dirisha dogo.

Safu ya ushambuliaji wa timu hiyo ilikuwa na upungufu mwingi kwa haikuwa na uwezo wa kusumbulia beki iliyoshiba kama ile ya Azam na Yanga na wa timu nyingine.

Ilipoteza michezo miwili baada ya kufungwa na Yanga mabao 2-0 kisha bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, kabla ya kufikia dirisha dogo la usajili.

Kutokana na upungufu ulionekana katika safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho ni lazima walihitajika kufanya usajili ili kuimarisha idara hiyo.

Kwa upande wa kiungo, walikuwa vizuri kiasi, kwani Jastice Majabvi na Jonas Mkude ambaye hakupata nafasi ya kucheza kutokana na majeruhi haikuwa na upungufu mkubwa hali kadhalika sehemu ya ulinzi.

Timu nyingine, ambayo ilihitaji kufanye usajili ni Majimaji ya Songea, ambayo ilionekana kuruhusu mabao mengi katika michezo yao, tena kwa kufungwa idadi kubwa ya mabao.

Majimaji alitakiwa kuvunja benki ili kuhakikisha wanafanya usajili kwa umakini katika idara ya ulinzi na ushambuliaji kutokana na waliokuwa hawafungi mabao.

Inawezekana ndicho, ambacho Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mika Lonnstorm, amekifanya katika usajili wake wa nyongeza katika kuhakikisha anafuta makosa yaliyojikeza awali.

Mbeya City nayo ilihitaji kutumia dirisha dogo la usajili kwa ajili kurekebisha kikosi chao, kwani wachezaji waliosajiliwa mwanzoni wa msimu huo, hawakuonyesha kucheza soka ya ushindani, kama ambavyo ilivyokuwa katika misimu miwili iliyopita, .

Kulikuwa na upungufu katika idara ya ulinzi, kiungo hasa baada ya kuondoka kwa wachezaji wao Deus Kaseke na Peter Mwalyanzi waliojiunga Simba na Yanga.

Lakini Mbeya City ilihitaji kufanya usajili kwa ajili ya kuboresha safu ya ulinzi, baada ya Juma Nyosso kufungiwa miaka miwili kutojihusika na soka kutokana na kumdhalalisha mshambuliaji wa Azam, John Bocco.

Ukiiangalia Kagera Sugar ni kama usajili wa dirisha dogo ulikuwa unahitajika zaidi kwa timu hiyo kutokana na kupoteza mwelekeo kwa kushindwa kuonyesha soka ya ushindani.

Katika kikosi cha Kagera Sugar, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Rishard Moahamed Aldof alikuwa na sababu ya kufanya usajili usajili kwa umakini kutokana na upungufu ulionekana karibu kila idara.

Haikuwa kwa Kagera Sugar pekee, hata Kocha Mkuu JKT Ruvu, Abdallah Kibaden alihitaji kufanya marekebisho makubwa katika kikosi chake baada kupoteza michezo mingi.

JKT Ruvu ilipoteza mwelekeo kwenye ligi hiyo, baada ya kuonekana kulikuwa na upungufu katika safu ya ushambuliaji na ulinzi, kwani walikuwa hafungi mabao, lakini walikubali kufungwa katika kila mchezo.

Tatizo kama hilo, lilionekana kwa, Mgambo Shooting, African Sports, Coastal Union, ambaye kocha mkuu wake, Jackson Mayanja alikuwa lazima afanye usajili katika idara ya ushambuliaji ili kuiwezesha timu ya kufunga mabao mengi zaidi.

Ukiangalia Mtibwa Sugar na Azam ambao wataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani, wenyewe walikamilika katika idara zote.

Mtibwa Sugar na Azam hawakuwa na sababu ya kutumia dirisha dogo kuongoza wachezaji wapya kutokana na idara zao hazikuwa na upungufu mkubwa kiasi cha kutumia fedha kusajili.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu na wawakilishi wetu katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika mwakani, hawakuwa na upungufu mkubwa katika kikosi chao.

Kikosi cha Wanajangwani hao, kilionekana kimetimia kila idara, lakini kila nikiangalia kikosi hicho naona kwamba, walihitaji kusajili kiungo mkabaji kutokana na Thaban Kamusoko anaonekana kucheza zaidi chini ya mabeki.

Kamusoko anaonekana ni kiungo mzuri, lakini ni mzito wa kuunganisha viungo wa chini na mbele hali ambayo anaweza kuigharimu Yanga kwenye michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pamoja na kwamba Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm anaweza kupingana na hiki nilichokieleza, lakini huu ndio ukweli na uwezo wa Kamusoko utaonekana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Binafsi sioni kwamba Yanga walikuwa na sababu kumsajili winga kutoka Niger, Issoufou Boubar Garba, ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi za mbele, badala ya kuimarisha nafasi ya kiungo mkabaji kwa kuwa wanashiriki michuano mikubwa Afrika.

Yanga hawakuwa na mahitaji ya Garba kutokana na nafasi yake, inaweza kuchezwa na Malimi Busungu, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima ambaye, wakati mwingine anatokea pembeni.

Kama ndivyo hivyo, hawakuwa na sababu ya kumtema Mbrazil , Andrey Coutinho katika kipindi hiki cha dirisha dogo la ligi hiyo.

Sikupata kuona mahitaji ya Stand United, Toto Africans, Ndanda na Mwadui kwa kuwa sikupata muda wa kuziangalia zikicheza uwanjani.

Hata hivyo tukiitazama Yanga ambayo ineonakana kuwa na kikosi imara cha kuweza kutwaa ubingwa, ni dhahiri inayo kazi ya kufanya huko mbele. Yanga kama inataka kutwaa ubingwa lazima ikubali kujiimarisha kiungo mkabaji maana ndilo eneo lenye matatizo makubwa.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version