England watakuwa wenyeji wa fainali zijazo za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) na mechi itapigwa kwenye Uwanja wa Wembley.
Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) limetangaza rasmi kwamba Chama cha Soka cha England (FA) kimeshinda kwenye maombi yaliyowasilishwa ya kuwa mwenyeji. Tayari mechi za mkondo wa kwanza kwenye makundi zimechezwa.
Wembley ndio uwanja unaotumiwa kama wa taifa kwa England, ambapo huchezewa mechi za kimataifa na nyingine kwa kadiri FA inavyopanga, kama fainali za Kombe la FA na mechi nyingine kubwa.
Uefa imesema kwamba viwanja vya Hampden Park uliopo Uskochi na Aviva uliopo Dublin nchini Ireland vitatumika kwa ajili ya mechi 16 za mwisho na tatu za hatua ya makundi.
FA ya England imeishinda ile ya Ujerumani (DFB) waliotaka kuwa wenyeji, na badala yake watafanya hivyo katika moja ya hatua za robo fainali na mechi tatu za makundi kadhalika.
Mechi za robo fainali na mechi tatu za makundi zitachezwa Munich (Ujerumani), Baku (Azerbaijan), Roma (Italia) and St Petersburg nchini Urusi.
Majiji wenyeji yatakayoandaa mechi tatu za makundi katika hatua ya 16 bora ni Copenhagen (Denmark), Bucharest (Romania), Amsterdam (Uholanzi), Bilbao (Hispania), Budapest (Hungary) na Brussels nchini Ubelgiji.