Menu
in , , ,

WATOTO WA KARIAKOO KATIKA KLABU BINGWA AFRIKA

Tanzania Sports

WATOTO WA KARIAKOO WAHESHIMISHA NCHI KATIKA KLABU BINGWA AFRIKA

Kariakoo ni maarufu sana kwa Tanzania kama ndio soko kubwa la kibiashara kwa nchi yetu na kwa namna Fulani soko hilo limekuwa linahudumia hadi nchi jirani kwani wafanyabiashara wa nchi jirani nao wamekuwa wanakuja katika soko hilo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali hususani kununua bidhaa ambazo nao wanazichukua na kuzipeleka kuziuza katika nchi za kwao. Katika sekta ya michezo kariakoo ndiko chimbuko la michezo ya kulipwa kwani vilabu ambavyo vimewakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya kulipwa ya ndani na nje ya nchi viliibukia hapa. Mnamo tarehe 5 mwezi wa 4 vilabu vya kariakoo yaani watoto wa Jangwani na Msimbazi vilikuwa nje ya nchi vikicheza mechi za ushindani katika shindano la klabu bingwa afrika katika hatua ya robo fainali. Vilabu hivyo vimecheza na vilabu vikubwa kwa sasa barani afrika ambapo Yanga ilikuwa nchini Afrika kusini ikicheza dhidi ya Mamelodi Sundowns na Simba ilikuwa jijini Cairo nchini Misri ambapo ilikuwa inacheza dhidi ya Al ahly.

Vilabu hivi vimeheshimisha nchi na kitongoji cha kariakoo kwani vimekuwa ni vilabu pekee ambavyo vinatoka nchi mmoja ambavyo vimefika hatua hiyo na pia licha ya kwamba vimefungwa na kutolewa lakini vimetolewa huku vikionyesha soka la ushindani, Yanga licha ya kutumia soka la staili ya kocha wa Atletico Madrid la kujilinda Zaidi lakini walionyesha upinzani ambao hata wapinzani wao wameheshimu kwani waliweza kuzuia klabu ya Mamelodi kuweza kushinda licha ya kwamba klabu hiyo ilijaza mastaa wake wote na ilicheza soka la kasi la kushambulia kwa asana lakini haikuweza kupata goli dhidi ya ukuta wa chuma wa klabu ya Yanga. Staa kama Peter Shalulile ambayo anasifika kwa uwezo wake wa kucheka na nyavu lakini hakuonekana kabisa katika mechi zote mbili dhidi ya watoto wa Jangwani. Teboho Mokoena hakuweza kuvuka ukuta ule na kuingia katika 18 za Yanga na katika mechi zote mbili amekuwa ni mtu ambaye anajaribu tu kupiga mashuti akiwa nje ya 18 ya goli la Yanga.  

Simba imetolewa halikadhalika kwa jumla ya magoli  kwa bila lakini licha ya kufungwa hivyo ila ilionyesha soka lenye kuvutia. Huwezi kulaumu kwani imetolewa na klabu bora ya mda wote ya barani Afrika. Al ahly sio klabu ya kawaida kwani imeshazoea kulibeba kombe la klabu bingwa na imekuwa ni mwiba sana kwa timu pinzani pindi inapokuwa kwenye hatua za mtoano na inajua mbinu za kuweza kusonga mbele. 

Vilabu hivi vimeweka historia kwani sio kawaida kwa vilabu viwili ambavyo vinatoka kitongoji kimoja kuweza kufika hatua kubwa za mashindano ya kimataifa ndani ya mda mmoja. Hii  inaonyesha wazi kwamba ipo siku katika miaka ya hivi karibuni tutashuhudia fainali ya klabu bingwa Afrika baina ya watoto hao wa Kariakoo. Ukiangalia uwekezaji wa Simba na Yanga na uwekezaji wa Al Ahly na Mamelodi sundowns ni vitu viwili tofauti kwani ukiangalia kuna wachezaji kama Percy Tau ambaye ada yake ya usajili unaweza ukakuta ni sawa na kununua wachezaji wote wawili wa timu hizo mbili. Licha ya hivyo ila bado wachezaji wa watoto wa kariakoo walionyesha soka maridadi na lenye ushindani ambao ulifanya mastaa hao ambao walisajiliwa kwa bei kubwa wasionekane sana pindi walipokutana uwanjani. Al Ahly imekuwa na uwezo wa kifedha mkubwa ambao umekuwa unawazuia wachezaji wake wasiweze kusajiliwa katika vilabu vya ulaya. Kocha maarufu wa kireno Jose Mourinho anasema kwamba wakati yuko katika klabu ya Chelsea ya England alijaribu mara kadhaa kutuma ofa ya kumshawishi staa wa kimisri ambaye alikuwa anachezea klabu ya Al Ahly bwana Mohammed Aboutrika aende kujinga na klabu hiyo ya jijini London lakini alikuwa anashindwa kumshawishi kutokana na huduma nzuri ambazo staa huyo alikuwa anapata kutoka katika klabu hiyo. Kama klabu hiyo ina ubavu wa kuweza kumzuia mchezaji asiende kucheza Ulaya basi ina uwezo mkuwa wa kifedha na pia inaweza ikashindana na hivi vilabu vingine vya Afrika.

Ulaya na mabara mengine ni kawaida kukuta vilabu viwili vya mji ama jiji moja kukutana katika hatua ya mashindano ya kimataifa ila sio kwa vilabu ambavyo vinatoka katika kitongoji kimoja mfano klabu ya Atletico Madrid na Real Madrid vimewahi kukutana katika hatua ya fainali ya klabu bingwa ya Ulaya lakini vilabu hivyo havitoki kitongoji kimoja kama ilivyo Simba na Yanga. AC MILAN na Juventus wameshawahi kukutana fainali ya klabu bingwa ila hawatoko jiji moja wala kitongoji kimoja. Manchester City na Tottenham Hotspur wameshawahi kukutana nusu fainali ya klabu bingwa ulaya ila hawatoki jiji moja. Kwa hiyo kama Simba na Yanga wangefanikiwa kuvuka nusu na hatimaye fainali basi wangekuwa wameweka rekodi yao ya kiulimwengu kuwa ni vilabu vya kwanza kutoka kitongoji kimoja kukutana katika mashindano ya kimataifa katika hatua hiyo.

Uongozi wa vilabu hivi viwili unatakiwa usibweteke na kufika hatua ya robo fainali mwaka huu ila wanatakiwa wajipange Zaidi kwani mahitaji ya mashabiki ni makubwa sana na wanatakiwa washibishe kiu ya mashabiki wao. Kwa sasa vilabu hivi vimeshaonjesha raha mashabiki wao kwa kufika hatua kubwa kimataifa na mashabiki wao wameanza kuamini kwamba zama za kichwa cha mwendawazimu zimepita na sasa ni zama za mafanikio katika soka na michezo kwa ujumla kwa hiyo vinatakiwa vijipambanue Zaidi na kufanya maboresho katika maeneo kadhaa;

Mosi vinatakiwa viboreshe vikosi vyao. Vikosi vyao vinatakiwa viwe vipana Zaidi na viwe vyenye kuweza kuleta ushindani Zaidi kuliko sasa. Kwa sasa vikosi vyao vimeshaonekana kimataifa na wapinzani wa kimataifa tayari wameshawasoma kwa hiyo wanatakiwa wafanye maboresho na kuwa na wachezaji ambao wanaweza kuleta ushindani kimataifa mwanzo mwisho. Ukiangalia mfano Yanga kwa kumkosa Aucho kuna mahala ilipwaya kidogo.

Pili wanatakiwa watafute udhamini Zaidi vilabu hivyo vinatakiwa vipambane na kutafuta wadhamini wakubwa Zaidi ndani na nje ya nchi. Udhamini huo utaweza kusaidia vilabu hivyo kuweza kununua wachezaji wakubwa Zaidi na ambao wataweza kuleta ushindani Zaidi.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version