Menu
in

Wachezaji Yanga walia njaa

Timu ya Yanga

Ikiwa inakabiliwa na ushindani mkali katika kampeni yake ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na pia mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, programu za mazoezi ya Yanga inashindwa kutekelezeka kikamilifu kutokana na wachezaji wake kutopata mishahara yao ya miezi miwili.

Mishahara hiyo ambayo wachezaji wanadai ni ya mwezi Novemba na Desemba, ambao umeambatana na sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili imezipata ni kwamba mbali na wachezaji hao, pia wafanyakazi wengine walioajiriwa na klabu hiyo hawajalipwa kwa muda wa miezi mitatu sasa.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa hali hiyo ya ukata imechangia mambo mengi kutofanyika kama ilivyotarajiwa ikiwemo kuvurugika kwa programu ya mazoezi.
“Hali ni mbaya, klabu haina pesa, mambo mengi hayafanyiki kama ilivyokusudiwa, tunajaribu kufanya kila linalowezekana ili kutatua tatizo hili linalotukabili,” alisema mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Aliongeza kuwa kukosekana kwa fedha kutoka kwa aliyekuwa mfadhili wao na mapato madogo ya mlangoni yaliyokuwa yakipatikana katika mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi ndio sababu nyingine iliyofanya klabu yao ikose fedha za kujiendesha.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version