Jumatatu ndiyo siku ambayo inasubiriwa kukamilisha ndoto ya Phillipe Countinho.
Ndoto ambayo aliipigania kuanzia dirisha la majira ya joto la usajili
lililopita lakini Liverpool alipigana kumbakisha.
Walifanikiwa kumbakisha, wakaamini wataendelea kufanya chochote
wanachoweza kufanya ili abaki Liverpool.
Lakini jitihada zao zilikuwa bure kwa sababu mwili wa Phillipe
Countinho ulibaki Liverpool lakini akili yake ilikuwa Barcelona.
Kila alichokuwa anakifanya, alikifanya huku akiwa ni lini ataenda Barcelona.
Ndiyo maana hakuona hatari kwenda katika kipindi hiki cha usajili wa
majira ya baridi.
Hakuona hatari ya yeye kutocheza klabu bingwa ulaya ( UEFA champions
League) ili mradi ndoto yake itimie ya kwenda kucheza Barcelona.
Hadithi sasa ishabadirika, Phillipe Countinho yupo katika jiji la
Barcelona akisubiri jumatatu afanyiwe vipimo kuona kama atafuzu vipimo
awe mchezaji rasmi wa Barcelona.
Ameleta furaha kwa mashabiki wa Barcelona na kuacha huzuni na
masikitiko ƙwa watu kwa mashabiki wa Liverpool.
Ameondoka Liverpool , nafasi yake nani anaenda kuiziba?
Hili ndilo swali ambalo tunatakiwa kujiuliza na kutakiwa kulijibu.
Hawa ndiyo wachezaji ambao wanafaa kuchukua nafasi ya Phillipe
Countinho pale Liverpool.
Henrikh Mkhitaryan. Mwaka 2009 aliyewahi kuwa nyota wa timu ya
Liverpool, Michel Owen alienda Manchester United akitokea Newcastle
United.
Baada ya kujiunga na Galacticos ya kina Luis Figo, David Beckham,
Roberto Carlos na Ronaldo, maisha yake aliamua kuyahamishia Newcastale
ndipo akaenda Manchester United.
Lilikuwa tusi kubwa sana alilowatukana mashabiki wa Liverpool, akawa
amewasiliti na kujiunga na mahasimu wao wakubwa.
Vilabu hivi mara ya mwisho kuuzia wachezaji moja kwa moja ilikuwa
mwaka 1964,mwaka ambao Phil Chisnall alitoka Manchester United kwenda
Liverpool.
Tangia hapo hizi timu hazijawahi kuuziana mchezaji moja kwa moja.
Huu ndiyo utakuwa ugumu wa kwanza wa kumpata Henrikh Mkhitaryan ,
mchezaji ambaye anaonekana hana nafasi katika kikosi cha Manchester
United.
Henrikh Mkhitaryan aliwahi kuwa na Jurgen Klopp katika kikosi cha
Borrusia Dortmund, wanajuana vizuri hawa wawili.
Jurgen Klopp anajua namna sahihi ya kumtumia.
Henrikh Mkhitaryan anauwezo wa kucheza nyuma ya mshambuliaji, katikati
na akitokea pembeni kwenda kwenye box la mpinzani kama alivyo Phillipe
Countinho.
Pia ana uwezo mkubwa wa kufunga na kutoa pasi za mwisho za magoli.
Ryad Mahrez. Ukizungumzia wachezaji ambao walikuwa mhimili wa
Leicester City kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England msimu wa
2015/2016 huwezi acha kumtaja Ryad Mahrez.
Mchezaji bora wa ligi kuu ya England msimu huo wa mwaka 2015/2016.
Anauwezo wa kucheza kama Middle Right ( katikati ya uwanja akiwa
kulia). Pia anaweza akacheza kama Attacking Middle Right.
Msimu huu amehusika kwenye magoli 14 katika michezo 21, akiwa ametoa
pasi za mwisho za magoli 7 na kufunga goli 7.
Kasi yake, uwezo wake wa kufunga na kutoa pasi za mwisho vinaendana na
mfumo wa Jurgen Klopp.
Thomas Lemar. Kwenye dirisha la majira ya joto Monaco hawakutaka kumwachia.
Lakini hii haimanishi Thomas Lemar ana maisha marefu pale Monaco. Muda
wowote anaweza akaondoka.
Na huyu ni moja ya wachezaji ambao wanaweza kuja kuziba nafasi ya
Phillipe Countinho.
Ana uwezo wa kucheza kama Attacking Middlefielder kama Phillipe
Countinho. Anacheza pia kama Attacking Middlefielder left na Middle
Left. Kama nafasi za Phillipe Countinho ambazo huwa anacheza.
Msimu huu kacheza michezo 15 na kahusika katika magoli 6 mpaka sasa.
Manuel Lanzini, ni mzoefu wa ligi kuu ya England kama alivyo Ryad Mahrez.
Ana uwezo wa kucheza nyuma ya mshambuliaji, anauwezo wa kucheza pia
kama kiungo wa katikati ( Central Middfielder) na akacheza pia kama
Attacking Central Middfielder.
Pamoja na kwamba alikuwa anasumbuliwa na majeraha mpaka sasa
amefanikiwa kuhusika katika magoli 6 kwenye mechi 15 alizocheza.
Juan Draxler. Hana nafasi katika kikosi cha PSG kwa sasa.
Ukiangalia kacheza michezo 13 na kaanza michezo 9 tu msimu huu.
Nafasi yake ni finyu kulingana na kikosi cha PSG kilivyo na nyota
wengi kwa sasa.
Kutokuwa na nafasi pana kwake katika kikosi cha PSG kutawapa nafasi
kubwa Liverpool ya kumchukua kama wakiamua kumfuatilia kwa ukaribu