*Man City na Barca, kisha Arsenal na Bayern
Kivumbi cha hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) kimeanza baada ya 16 nyingine kutupwa nje.
Manchester City ambao wamekuwa na nguvu kubwa ya kufunga mabao wanakabiliana na Barcelona, moja ya timu kubwa duniani.
Badala ya kuzungumzia timu yake, Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ambaye hivi karibuni amekuwa akiwananga makocha wenzake, amedai kwamba City wanakabiliana na Barca mbovu kabisa kuliko ilivyopata kuwa miaka mingi iliyopita.
Mchuano baina ya Manchester City na Barcelona Jumanne hii unaonekana kuwa wa kuvutia sana, ambapo Manuel Pellegrini atakabiliana nao kwa mara ya kwanza akiwa City lakini anawajua vyema Barca kwani alikutana nao wakati akiifundisha Malaga. Ni wazi haitakuwa kazi rahisi sana.
Hii ni hatua yenye mvutano mkali, ambapo mabingwa watetezi, Bayern Munich, kama ilivyokuwa msimu uliopita wanakabiliana na Arsenal.
Wanaanza pia jijini London Jumatano hii kama mwaka jana na watamalizia huko Bavaria, wenyewe Wajerumani wakieleza kwamba wanahofia Arsenal watawapelekesha.
Manchester United wamepangwa kupepetana na Olympiakos ambao kocha David Moyes alikwenda kwao kutazama moja ya mechi zao za ligi.
AC Milan ambao hawaendi vyema sana wanakabiliana na timu inayochukuliwa kuwa ya tatu kwa ubora nchini Hispania, Atletico Madrid.
Bayer 04 Leverkusen watakabiliana na muziki wa Paris Saint-Germain wakati Galatasaray watakuwa wakipepetana na Chelsea.
Schalke 04 wanakipiga na Real Madrid wakati
Zenit St. Petersburg wakikabiliana na wagumu wa Ujerumani, Borussia Dortmund.
Schalke 04 wanakipiga na Real Madrid wakati
Zenit St. Petersburg wakikabiliana na wagumu wa Ujerumani, Borussia Dortmund.
Baada ya mechi za Jumanne na Jumatano wiki hii na nyingine Februari 25 na 26, marudiano yatakuwa kati ya Machi 11 na 12 na Machi 18 na 19.