Ligi kuu Tanzania imeanza leo jumapili ambapo timu mbalimbali zilioneshana umwamba.
Mechi zilizokuwa zinasubiriwa kwa hamu ni ile ya Simba na Yanga hasa kuona sajili mpya zinafanya kazi ipi.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC waliwapa raha wapenzi na mashabiki wao kwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu FC ambayo yanawapa uongozi wa ligi kwa alama tatu muhimu.
Goli la kwanza la Simba limefungwa na John Bocco dakika ya 10 ya mchezo huo baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Clatus Chama.
Ihefu FC walisawazisha dakika ya 14 mfungaji akiwa ni Omary Mponda.
Lakini kiungo mkabaji wa Simba Mzamiru Yasini amehakikisha timu hiyo inaondoka na ushindi baada ya kufunga dakika ya 42 ya mchezo huo.
Ihefu walionesha mpira safi huku goli la pili la Omary Mponda muamuzi wa pembeni alilikataa bila sababu ambapo pia alikataa goli la Meddie Kagere kama alivyofanya kwa Ihefu FC.
Kwa ujumla mechi ilikuwa nzuri sana na ilikuwa katika hadhi ya kuitwa mechji ya ligi.
Kikosi cha Simba kilikuwa kama ifuatavyo Manula, Kapombe, Mohamed Hussein, Onyango, Kenedy Juma, Mkude, Dilunga, Mzamiru, Bocco na Morrison.
Wakati huo huo Yanga ambayo ilikuwa na jopo la wachezaji wapya inaonekana kurudi katika ushindani licha ya kutoa sare ya goli 1-1 .
Yanga iliingia uwanjani ikiwa na matumaini makubwa baada ya kufanya usajili kabambe.
Mbinu za kocha Salum Mayanga zilitosha kabisa kugawa alama na Yanga katika mchezo huo.
Timu ya Wananchi ilianza na wachezaji saba wapya huku dakika 45 zilitosha kumuona Farid Mussa akifanya vizuri sana.
Nyota hao ni Mwamnyeto, Yassini, Kibwana, Sarpong, Farid, Mauya na Abdallah Shaibu.
Tumeona kazi nzuri ya Michael Sarpong kufunga goli lake la kwanza katika ufunguzi wa ligi.
Tanzania Prisons walikuwa wa kwanza kupata goli lakini kazi nzuri ya Farid Mussa ikamfanya Michael Sarpong kusawazisha goli la kuipa alama moja Yanga.
Kikosi cha Yanga kilikuwa hivi, Shikalo, Mwamnyeto, Yassini, Kibwana, Sarpong, Farid, Mauya, Abdallah Shaibu, Feisal, Nchimbi na Kaseke.
Huenda uchoyo wa Kisinda umeipa nafuu Tanzania Prisons kutopoteza mchezo huo.
Matokeo mengine Namungo Fc 1 Coastal Union 0, Biashara United 1 Gwambina 0, Dodoma FC 1 Mwadui 0 na Mtibwa Sugar 0 Ruvu Shooting 0.
Michezo mingine inapigwa jumatatu ambapo Azam FC watacheza na Polisi Tanzania huku KMC itapambana na Mbeya City.