Baada ya ushindi wa mabao 4-0 walioupata Kinondoni Municipal Council (KMC) dhidi ya Mbeya City wamepanda hadi nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara .
Awali Simba ndio ilikuwa inaongoza msimamo huo baada ya kuitandika Ihefu FC mabao 2-1 katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa ligi katika mzuko wa kwanza.
Sabiyanka bado anashikilia rekodi ya kufunga goli la mapema zaidi kwani iliibutua Yanga dakika ya 8 ya mchezo wao ulioishia kwa goli 1-1.
Katika michezo tisa iliyochezwa mzunguko wa kwanza yamefungwa magoli 14, huku KMC wakiongoza kwa kuchangia magoli 4 ikifuatiwa na Simba iliyovuna magoli 2.
Katika hatua hiyo ya kwanza magoli 9 yamefungwa katika kipindi cha kwanza cha michezo hiyo huku KMC na Simba bado zimechangia magoli mengi katika kipindi cha kwanza zimefunga magoli 2 kila mmoja.
Simba imefunga magoli yake dakika ya 10 na 42 wafungaji wakiwa John Bocco na Mzamiru Yassini wakati KMC yakifungwa dakika ya 22 na na 39, wafungaji wakiwa Emanuel Mvuyekure na Hasaan Kabunda.
Wengine waliofunga kipindi cha kwanza ni pamoja na Michael Sarpong dakika ya 19 wa Yanga pamoja na Omary Mponda wa Ihefu FC dakika ya 14.
Obrey Chirwa wa Azam FC, Lambert Sabiyanka wa Tanzania Prisons na Adam Adam kutoka JKT Tanzania wote wamefunga kipindi cha kwanza.
Sabiyanka bado anashikilia rekodi ya kufunga goli la mapema zaidi kwani iliibutua Yanga dakika ya 8 ya mchezo wao ulioishia kwa goli 1-1.
Magoli matano yamefungwa kipindi cha pili katika raundi ya kwanza.
Hakuna mchezaji aliyefunga goli zaidi ya moja katika raundi ya kwanza ya ligi kuu Tanzania Bara.