Menu
in , , ,

VODACOM KUTOA ZAWADI ZA VPL KESHO

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, kesho siku ya alhamis tarehe 11/06/2015 wanatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa Vodacom Premier League msimu wa 2014/2015.

Hafla ya utoaji wa zawadi hizo itafanyika katika ukumbi wa JB Belmonte (Kilimanjaro) uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower (PSPF), mtaa wa Ohio eneo la Posta Mpya jijini Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni.

Mgeni rasmi katika halfa hiyo ya utoaji zawadi kwa wachezaji, makocha, na timu washindi atakua ni Juma Nkamia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Vodacom watatoa zawadi kwa Bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na mshindi wa nne, baadhi ya vipengele vitakavyotolewa zawadi pia na wadhamini hao wa Ligi Kuu ni :

1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mohamed Hussein (Simba SC)
Mrisho Ngasa (Young Africans)
Saimon Msuva (Young Africans)

Vodacom Premier League (Tanzania)
Vodacom Premier League (Tanzania)

2. Mlinda mlango bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons)
Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
Shaban Hassan (Coastal union)

3. Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Goran Kopunovic (Simba SC)
Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
Mbwana Makata – (Tanzania Prisons)

4. Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Israel Mjuni Nkongo
Jonesia Rukyaa
Samwel Mpenzu

5. Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mgambo JKT
Mtibwa Sugar
Simba SC

MAHUNDI MCHEZAJI BORA MWEZI MEI
Wakati huo huo mchezaji John Mahundi wa timu ya Coastal Union amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei, 2015 na jopo la makocha kufuatia kuwazidi wachezaji wengine 14 aliokuwa anananiwa nao nafasi hiyo.

Kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi mei, Mahundi atazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version