KAMPUNI ya Simu za Mkononi Tanzania Vodacom imetoa Shilingi 45 milioni kwa ajili ya udhamini wa Michuano ya Kombe la Muungano itakayoanza kutimua vumbi Aprili 26 katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Zanzibar.
Meneja udhamini wa Vodacom, Emiliani Rwejuna alisema udhamini huo utahusisha pia na vifaa vya michezo, gharama za usafiri kwa wachezaji, posho na gharama za maandalizi na zawadi kwa washindi wa kombe hilo.
Alisema mshindi ataondoka kombe na Sh12milioni wakati mshindi wa pili atazawadiwa atazawadiwa kombe na Sh1milioni na wakati mchezaji bora wa michuano hiyo atapata 300,000.
Alisema kwa kawaida mashindano hayo huwa yanaanza katikati ya Aprili na kufikia mwisho Aprili 26 ambayo ni siku ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar lakini mwaka huu yataanza Aprili 26 na kumalizika katikati ya Mei.
Alisema mashindano hayo hujumuhisha timu kutoka Tanzania bara na visiwani na timu hushindana kwa mtindo wa ligi na mwaka huu ztimu zimegawanywa katika vituo viwili bara na kimoja visiwani.
Rwejuna alisema kwa kituo cha Mbeya kitakuwa na timu za Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Ruvuma wakati kituo cha mafinga kitakuwa na timu za mkoa wa Iringa na Zanzibar kitakuwa na timu za Zanzibar.
Alisema ilikumpata bingwa mshindi wa mkoa wa Mbeya atacheza na mshindi wa mkoa wa Mfindi na mchezo ni nyumbani na ugenini na mshindi wa hapo atacheza fainali na wa Zanzibar na utakuwa ni nyumbani na ugenini.