WINGA Savinho amekuwa mhimili katika klabu ya Manchester City. Vinicius Junior ndiye mchezaji bora wa FIFA wa mwaka na staa wa Real Madrid. Casemiro anamalizia soka lake katika klabu ya Manchester United. Rodrygo Goes anatajwa kuwa mchezaji mzuri zadiai kiufundi na mashabiki wanamwita ‘mzee wa matukio’ kwenye dimba la Santiago Bernabeu.
Rafinha amekuwa nyota na nahodha wa Barcelona. Bruno Guimares anatamba kwenye kiungo cha Newcastle akiwa na Jeolington klabuni hapo. Endrick ni kinda toka Palmeirs anayetengeneza jina lake katika klabu ya Real Madrid. Estevao atajiunga na Chelsea msimu ujao. Nyota hao wote ni raia wa Brazil na ambao wanajitahidi kurudisha thamani yao kwneye Ligi kubwa barani Ulaya. Licha ya kuwepo kwa nyota wengine, lakini klabu ya Palmeiras imekuwa kama mgodi wa kuzalisha vipaji vya soka. Na sasa limeibuka juina lingine la Vitor Reis ambaye anawindwa na vilabu mbalimbali vya England.
Vitor Reis ni nani?
Klabu ya Brighton imeweka mezani ofa ya pauni milioni 23 kama mtaji wake wa kumnununua Vitor Reis. Brighton wametoa ofa hiyo kwa ajili ya kumnunua mchezaji huyo ambaye anacheza nafasi ya beki wa kati. Brighton wametupia jicho lao kwa Vitor Reis ili kuimarisha kikosi chao kuelekea ngwe ya mwisho ya kumaliza Ligi ya EPL.
Vito Reis ana umri wa miaka 18 anasfika kuwa miongoni mwa nyota mahiri katika soka la Amerika kusini huku akiwa anazifutia timu mbalimbali za Ulaya zinazolenga kupata huduma yake. Brighton wamecheza kwa mafanikio katika ngwe ya kwanza ya Ligi ya EPL chini ya kocha Fabian Hurzeler ambapo klabu hiyo sasa inashikilia nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi hiyo. Kushika nafasi ya 10 si kwamba wameridhia lakini wana mipango ya kuvuka vihunzi na kufikia nafasi ya juu zaidi ufikapo mwisho wa Ligi kwahiyo njia pekee ni kuimarisha kikosi chao. Malengo ambaye amekuwa nyota katika klabu ya Palmeiras na amepenya kikosi cha kwanza kutokana na kipaji kikubwa alichonacho. Anatajwa kuwa nyota anayetamba kwenye ligi ya Brazil.
Palmeiras na Brighton kwa pamoja zinafanya uchambuzi kuhusu thamani ya fedha ya kulipa kama ada, ambapo mezani imetengwa kiasi kinachoelezwa ni pauni milioni 23 ambacho ni punfu ya milioni 2 kwani Palmeiras wanataka kulipwa pauni milioni 25 kwa kinda huyo. Palmeiras inasadikiwa kuzikataa ofa mbili za klabu zilizotaka kumsajili Vitor Reis, ambaye anahusishwa nha kwenda Arsenal, Real Madrid na Chelsea.
Nyota huyo wa miaka 18 anaweza kucheza kama beki wa kati, beki wa kulia, na beki wa kushoto, kwhaiyo anazimudu nafasi zote za beki. Palmeiras wamekuwa klabu inayozalisha wachezaji wenye vipaji katika bara la Amerika kusini huku nyota wake wakinunuliwa na vilabu mbalimbali vya Ulaya.
Hata hivyo Palmeiras huenda wakazuia uhamisho wa Vitor Reis kwa sababu wanatarajiwa kushiriki michuano ya Klabu bingwa wa Dunia itakayofanyika baadaye mwaka huu, lakini Brighton wanadaiwa kumtaka nyota huyo kujiunga na klabu yao mapema mwezi huu Januari ili kuimarisha kukosi chao.
Taarifa zinasema kuwa huenda klabu hizo zinaweza kukubaliana dili la usajili la Januari kisha Palmeiras wakapewa mchezaji huyo kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huu. Nyota huyo anapita katika nyayo za mabeki mahiri waliowahi kutoka Brazil kama vile Thiago Silva, Junior Baiano, Aldair Santos, Marquinhos, Marcelo na wengineo.