Klabu tano kati ya kumi na mbili zitakazoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao wa 2009 – 2010 tayari zimewasilisha majina ya makatibu,wekahazina na maofisa wa habari ambao wameajiriwa katika klabu zao hadi sasa.
Katibu Mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF,Fredrick Mwakalebela amezionya klabu zitakazoshindwa kutimuza kanuni za ligi kuu msimu unaokuja ikiwemo kujiri maofisa hao klabu hizo hazitashiriki ligi hiyo maana hilo ni azimio lao toka mwaka uliopita.
Katibu mkuu huyo wa wa TFF amesema klabu zote zitakazoshiriki ligi kuu ya Vodakom mwaka huu zimetakiwa kukamilisha zoezi la kuajiri watumishi hao hadi ifikapo AGOST 23 mwaka huu siku ambayo ligi kuu Tanzania bara itaanza kwenye msimu huu wa 2009 – 2010.
Klabu AMBAZO zilishatimiza wajibu wao ni pamoja na Azam FC,African Lyon , Manyema Rangers (Mkuki wa Sumu) zote za Dar es salaama ,Maji maji ya Songea (wanalizombe) kusini wa Tanzania , JKT Ruvu.
Miongoni mwa timu ambazo hazijatimiza wajibu huo wa TFF ni miamba ya soka hapa nchini Tanzania za Simba na Yanga lakini pia timu zinazofuata kw aukubwa ambapo ni Mtibwa Sugar ya Morogoro na Tanzania Prisons ya Mbeya pamoja, Toto Africa (Wanakishamapanda) ya Mwanza pamoja na Moro United bado hajatiza wajibu wa TFF ilamuda bado upo.