Menu
in , , ,

Vermaelen afikiria kuiacha Arsenal

 

Nahodha wa Arsenal, Thomas Vermaelen amesema anafikiria kuondoka klabuni hapo.

 

 

Vermaelen aliyewekwa benchi na kocha Arsene Wenger katika nusu ya pili ya msimu uliopita baada ya kupwaya sana kwenye beki ya kati, alikuja kuumia lakini kwa ujumla ana nafasi finyu.

 

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, amesema kwamba atafikiria uwezekano wa kwenda klabu nyingine ikiwa atakosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza kama ilivyo sasa.

 

Mwenendo wa Arsenal ulikuwa mbaya hivyo kwamba walikaribia kumaliza hata nje ya timu sita bora, lakini baada ya Wenger kuwapa majukumu ya ulinzi wa kati Per Metersacker na Laurent Koscielny mambo yaliimarika na kuanza ushindi.

 

Vermaelen aliwekwa benchi pamoja na kipa namba moja Wojciech Szczęsny, ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Mpoland mwenzake, Lukasz Fabianski, lakini Szczesny alirejea mwishoni mwa msimu baada ya kujifua vilivyo.

 

Mabeki wawili wa kati aliowaamini Wenger msimu uliopita wameendelea kung’ara kwenye ulinzi wa Arsenal, wakichanganyika vyema na mabeki wa pembeni, Bacary Sagna na Kierran Gibbs pamoja na viungo wa kimataifa walioifanya Arsenal ipae kwa mafanikio hadi kushika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.

 

Vermaelen anataka kutafuta klabu atakayochezea mara kwa mara ili kuweka hai ndoto zake za kuendelea kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa lake kwa ajili ya Kombe la Dunia Brazil mwakani, lakini pia ili kuonesha uwezo wake.

 

“Natakiwa kufikiria juu ya hili itakapolazimu. Bado kuna miezi kadhaa hadi kufika Januari, ni kweli si vyema kuendelea kukaa hivi bila kucheza hasa ukizingatia Kombe la Dunia linakuja … hata hivyo sijapagawa kama watu wanavyoniuliza.

 

“Nimezungumza na kocha wangu na hayo yatabaki kuwa siri baina yangu na yeye. Yaweza kutokea mambo katika sekunde tu na kubadili hali yangu, yaweza kuwa kesho au wiki ijayo na ikiwa hivyo tutakuwa na simulizi tofauti Januari kuhusu hali yangu,” anasema Vermaelen aliyechukua unahodha baada ya Robin van Persie kuhamia Manchester United msimu uliopita.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version