Menu
in

VAR ilivyobadilisha soka

VAR

VAR

Itafika mahali sasa kwapa limeotea, au vidole na hata beji ya jezi ya mchezaji.. 

Manchester City walipofunga bao zuri la ushindi kwenye sekunde za mwisho mwisho za mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) dhidi ya Tottenham Hotspur msimu wa machipukizi wa 2019, walau washabiki wawili waliokuwa kwenye mechi ile waliacha kutazama.

Mmoja alikuwa jukwaani, shabiki wa Man City aliyekuwa kavaa koti refu alinyanyuka na kuharakisha kutoka nje ya uwanja, akiwa amejawa raha kutokana na bao hilo la muda wa mwisho, akitaka kuwahi nyumbani baada ya ushindi.

Wakati huo huo, kwenye benchi la wachezaji wa akiba wa Spurs, alikuwa kaka Moussa Sissoko aliyetolewa uwanjani kwa kuwa majeruhi; alihuzunika hivyo kwamba alinyanyuka na kwenda akichechemea kwenye vyumba vya kubadilisha nguo peke yake.

Mie nilikuwa natazama TV na rafiki zangu, wote washabiki wa Spurs (ila mie siyo shabiki wa Spurs! na sote tuliharibikiwa. Nilikuwa nimechukua kiti cha jikoni, baada tu ya bao hilo kutinga nyavuni. Sivyo, nawaza, kwa lengo la kukirusha kwenye ile TV ili kuficha kitisho kilichokuwa mbele yangu dhidi ya macho yangu.

City walishangilia kwa sekunde 50 au 60 hivi. Baadhi ya wacheazaj walikuwa wakiteleza kwa magoti, wengine wakisali kushukuru na baadhi wakikumbatiana kujipongeza. Mara mwamuzi akapuliza kipenga, tukajua kwamba ni cha kumaliza mechi.

Kumbe haikuwa hivyo, marudio kwa taratibu ya video ya bao lile yalikuwa yamefanyika na ikawa imeamuliwa kwamba City walikuwa wameotea kidogo. Bao lile likafutwa. Ule ukweli wa msingi wa soka – wameshinda, kwa hiyo tumepoteza – ukageuzwa kichwa chini. Sekunde zile za taabu na mateso zikafutwa kadhalika.

Watu walikuwa kama wamechanganyikiwa. VAR hiyo – yaani video kwa ajili ya usaidizi kwa waamuzi ilikuwa imefanya mambo yake. Imekuwa kwenye ulimwengu wa soka tangu 2017. Pamekuwapo maamuzi muhimu na makubwa yaliyosaidiwa na VAR kwenye mashindano tofauti, lakini sikupata kuona uamuzi wa kushitua na kuchanganya kama wa bao hilo la City.

Nilikiweka chini kiti kile cha jikoni kwa uangalifu, nikakikumbatia. Nilikuwa najua juu ya utata uliokuwapo, nikichanganya na unafuu niliopata kwa bao dhidi ya timu ya marafiki zangu kukataliwa, nikamaizi hakika kwamba zama hizi kuna kitu tofauti sana kwenye soka na namna inavyochezeshwa.

Ikawa kwamba yule shabiki wa City amefika nje kwenye eneo la maegesho ya magari, basi mtangazaji wa TV alipomwendea kutaka kupata mrejesho kwake juu ya habari zilizokuwa zinasambaa za bao kukataliwa, naye akasema bila kujua likichotokea.

“Kwa nini nichukie? Tumeshinda!” alisema kwa kujiamini. Haukupita muda, ile raha ikafutika baada ya habari kusambaa kwamba bao lilikataliwa, klip yake ikawa inasambaa kwenye mitandao ya jamii na wadau kuidaka kwenye simu zao za mkononi.

Ama kwa Sissoko, aliyekuwa mwenyewe kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, alisikia kutoka kwa jamaa yake akisema; “Ajabu, siamini!” Sissoko anasema kwamba akiisha kupata habari ya bao lile kufutwa na VAR alijisahau hata kwamba ameumia, akakimbilia uwanjani, akisema kwamba ulikuwa wakati wa kihistoria, akiwa na mshituko wa kihemko.

Hivi ndivyo VAR imekuwa ikibadilisha mambo, wa raha kuwa na uchungu na wa uchungu kuwa na raha kutokana na mabadiliko ya matokeo. Miaka karibu miwili sasa tangu hilo jambo la Spurs-City inaonekana kwamba kuna kukubaliana kwamba soka imepoteza kitu; ile soka yenyewe imepotea kidogo.

Karibu kila wikiendi sasa kuna maamuzi yanayotokana na VAR yanayowabadilisha watu, kuna mijadala mingi na mikubwa juu ya uendelea juu ya uthabiti na uendelevu wake. Kiangazi kilichopita, Kocha wa Sheffield United, Chris Wilder alisema alikuwa bado anaamua iwapo acheke au alie kutokana na matukio mengi ya kushangaza ya VAR.

Makocha wengine wa timu za Ligi Kuu ya England (EPL) nao walionekana kuchanganywa na VAR. Bosi wa Crystal Palace, Roy Hodgson, kwa mfano, alisema; “ni upuuzi unaoharibu mchezo”, Kocha wa West Ham, David Moyes akasema; “bado nina hasira kwamba hivi ndivyo jinsi soka imekwenda.” Yule wa Fulham, Scott Parker akisema; “jinai, fujo tu.”

Kocha wa Spurs, Jose Mourinho alikuwa ameahidi kuacha kuishambulia VAR kwa wasiwasi wa kuadhibiwa na vyombo husika kama kutozwa faini, akisema kwamba kuliko hivyo bora fedha husika azitoe kama msaada kwa wakfu.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anasikitika na kuchukizwa jinsi uamuzi unakuwa umeshachukuliwa na baaada ya muda mrefu unatenguliwa na VAR na kuvuruga mwenendo wa mechi. Kuna nyakati hadi dakika 10 watu wanakuwa wakisubiri tu kutazama video hizo na uamuzi. Vipi kwa wachezaji wanaofunga; je, wajifunze kushangilia nusu nusu hadi watakapopata uhakika wa mwisho kwamba mabao yao yamekubaliwa?

Palikuwapo mechi baina ya Leeds United na Crystal Palace Novemba mwaka jana, ambapo mshambuliaji wa Leeds, Patrick Bamford, alifunga bao zuri, lakini eti kumbe alipokuwa akimtazama mchezaji mwenzake na kuwaza wapi pa kumimina majalo, sehemu ya mkono wake ulikuwa umeotea. Kweli soka imepokonywa nyakati zile za mashangilio ya raha kubwa.

Wachambuzi kama Gary Lineker na Gary Neville nao wamekuwa wakilalamikia hali hiyo ya VAR kwamba haina maana sana na mechi zinaharibiwa mtiririko wake. Kwamba itafika mahali sasa kwapa limeotea, au vidole na hata beji ya jezi ya mchezaji. 

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version