*LVG asema hakutarajia Welbeck acheze Old Trafford
*Watu wanamtishia kifo shujaa Danny Welbeck
Robo fainali ya Kombe la FA imemalizika, lakini si yatokanayo nayo, ambapo mfungaji wa bao la ushindi kwa Arsenal dhidi ya Manchester United anartishiwa.
Welbeck aliyeuzwa Arsenal msimu uliopita wa kiangazi na koch mpya wa man United, Louis van Gaal, alirudi Old Trafford na kufunga bao, akimzodoa bosi aliyemuuza kwa madai kwamba si mtamu kwenye kufunga mabao.
Welbeck ni Mwingereza aliyekulia tangu mapema kwenye Akademia ya Old Trafford lakini Van Gaal akaamua kumuuza kwa pauni milioni 16 kwa Arsenal Septemba mwaka jana.
Kocha huyo, maarufu zaidi kama LVG alisema alimuuza kwa sababu hakuwa na uwezo wa kupachika mabao kama akina Robin van Persie na WayneRooney. Alimsajili pia Radamel Falcao amabye hajaonesha makubwa hapo,
“Manchester United wanamaanisha makubwa kwangu, mie ni shabiki na ni ngumu kuchukua ukweli kwamba nimeshiriki kuwang’oa mashindanoni,” anasema Welbeck.
Mtu aliyesajiliwa badala yake, Radamel Falcao hakuwa kwenye kikosi hicho amekuwa akichezeshwa kwa nadra, huku LVG akinukuliwa kusema kwamba hawezi kucheza zaidi ya dakika 20.
Katika hatua nyingine, askari polisi wa Greater Manchester wanasema kwamba wanachunguza juu ya watu wanaodaiwa ama kutoa lugha za kashf dhidi ya Welbeck au kutishia kumuua.
Ushindi huu wa Arsenal katika dimba laOld Trafford umekuja kw amara ya kwanza tangu 2006, na ni angalizo kwa wenyeji juu ya kujichunga, kujiangalia ili kuona wanafuzu kwa Kombe la Mabingwa wa Ulaya.