Menu
in

Usajili Wa Kaze Watakata Yanga

Kocha Cedric Kaze ambaye anayetarajiwa kutua Yanga amewanyamazisha midomo wote waliokuwa wanauzungunzia vibaya  usajili wa timu hiyo  msimu huu.

Walio wengi walikuwa wanalaumu uongozi wa timu hiyo kuwa walisajili kwa kufuata mihemko bila ya kumshirikisha kocha. Kwa kauli thabiti ya kocha mtarajiwa wa timu hiyo inawaondoa mchezoni waliokuwa wanaubeza uongozi.

Kaze ameweka wazi kuwa katika sajili za Yanga walizofanya msimu huu amehusika kupendekeza baadhi ya wachezaji ambao wamesajiliwa.

Katika orodha hiyo yeye alipendekeza zaidi sehemu ya ushambuliaji, kuanzia kiungo hadi wafungaji.

Amesema kuwa usajili wa Mshambuliaji Michael  Sarpong, winga Tuisila Kisinda, mshambuliaji Yacouba Sogne, viungo Carlinhos pamoja na Mukoko Tonombe huku usajili mpya ambao umefanyika siku ya Jumatatu usiku wa Saidi Ntibazonkiza.

Hizo ni asilimia mia moja amehusika kutoa mapendekezo  kwa namna hiyo kocha huyo amewaziba midomo wachambuzi na mashabiki waliokuwa wanahoji juu ya usajili wa Yanga.

Ukiangalia sajili hizo ambazo zimetajwa hapo juu utaona dhahiri kuwa kwa kiwango kikubwa yeye ndiye kahusika kupendekeza usajili huku upande wa walinzi ukiwa umehusika zaidi na uongozi kushirikiana na  walimu wasaidizi.

Hadi sasa kila mmoja ameona kazi ya wachezaji hao ambao amependekeza kusajiliwa.

Carlinhos ambaye anaonekana bado hana nguvu ya kutosha amesaidia timu hiyo kupata alama 9 katika zile 13, kwani ametoa pasi za mwisho 2 ambazo zote zilikuwa za ushindi, zote alimpa Lamine Moro katika mchezo wa Mbeya City ambao Yanga ilishinda goli 1-0.

Nyingine ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo pia Yanga ilishinda 1-0 mfungaji akiwa Moro.

Pia alifunga goli 1 katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Coastal Union.

Michael Sarpong yeye amesaidia kukusanya alama moja baada ya kufunga goli la kukomboa dhidi ya Tanzanaia Prisons dakika ya 19 ambapo ilikuwa Yanga inaongozwa goli 1-0, mwisho wa mchezo timu hizo zilitoka 1-1.

Yacoub naye ameonesha uwezo wake kwani tayari anagoli moja alilofunga dhidi ya Coastal Union.

Tonombe naye amehusika na kupata alama tatu katika mchezo ambao Yanga walishinda goli 1-0 dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliopigwa mkoani Kagera.

Kisinda bado hajafunga lakini makali yake yameonekana na ni mmoja yawashambuliaji wakali sana wanaotokea pembeni, kasi yake inaonesha kabisa ni mtu wa aina gani.

Huu usajili mpya wa Saidi bado hatuja  uona vizuri japo video zake zinaonekana yote hayo kuhakikisha kuwa yupo makini na kile anachohitaji kukuifanya ndani ya timu hiyo.

Yote hayo ni matunda ya Kaze katika mapendekezo yake na hii inatuweka wazi kabisa kuwa tusiongee sana bali tuangalie maendeleo.

Hadi sasa kwa msemo wa vijiweni tunaweza kusema kuwa Kaze 3 walioubeza uongozi wa Yanga 0.

Kila mmoja anaweza kuongea na kutoa maoni ila kwa hili tuwapongeze Yanga kwa namna walivyokuwa wasiri na hawakutaka kusema kuwa nani yupo nyuma ya usajili.

Hii ndiyo hasa inayotakiwa hata kama unashambuliwa kiasi gani kinachotakiwa uwe na uvumilivu.

Tanzania Sports
Yanga

Kocha huyo anatarajiwa kutambulishwa muda wowote kuanzia sasa kwa taarifa za awali zinasema kocha huyo anatua siku ya Alhamisi.

Endapo kocha huyo atafanikiwa kujenga timu kwa kuiunganisha kwa pamoja itakuwa sababu ya kufanikiwa zaidi katika kazi yake.

KAZE ATAFAIDIKA AU YANGA ?

Kwa namna ilivyo endapo kocha huyo atafanikiwa kuleta kitu kipya na kuwaongoza wachezaji kuwa kitu kimoja na kuunganisha timu itakuwa sababu ya kufanikiwa zaidi kwake.

Kaze ndio atakayenufaika zaidi kuliko Yanga, klabu hiyo ni kongwe na kubwa hivyo kwa makocha ambao wamewahi kufika Afrika hakuna anayeweza kuchomoa endapo atahitajika.

Hivyo ni fursa kwa kocha huyo kunufaika na mpango huo akitusua hapo basi atakuwa amefanikiwa zaidi na huenda jina lake likakuwa kubwa zaidi ya lilivyo sasa hivi.

Ni kweli amefundisha sehemu mbalimbali lakini bado hajafundisha  timu kubwa ambazo anaweza kupata changamoto zaidi.

Ni wakati wake kuweza kufanikiwa kupitia ‘Brand’ ya Yanga itakuwa safari nzuri kwake.

Kwa upande wa Yanga watanufaika kama matokeo yatakuwa mazuri kwani kocha huyo hatoweza kudumu kwa miaka 10 au 15 hivyo watanufaika kwa kipindi hicho ambacho yeye yupo na akimaliza basi ataondoka wengine watakuja kufanya kazi.

Yanga inatatizo la kuunganisha timu kazi yake kubwa  kuanza kuunganisha kati ya eneo la kiungo na washambuliaji.

Akifauru hilo ahamie katika ufungaji jinsi atakavyo waweka washambuliaji katika sehemu ilio sahihi.

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version