Menu
in , , ,

Usajili EPL £1.165bn

Joe Hart

Matumizi makubwa ya fedha yamefanywa na klabu za Ligi Kuu ya England (EPL) na hadi kufungwa kwa dirisha la usajili la msimu wa kiangazi, zimetumiwa pauni bilioni 1.165.

Kiasi hicho kikubwa cha fedha kimevunja rekodi ya kilichotumika msimu uliopita, ambacho kilikuwa pauni milioni 870. Usajili pia umeshuhudia klabu zikirejesha nyota wao lakini pia zikiwatoa kwa mkopo nyota wengine pasipo kutarajiwa.

Klabu 13 za juu zimevunja rekodi zao wenyewe, pengine kwa sababu ya kila klabu kuanza kufaidika na mgawo wa pauni bilioni 5.1 za dili la matangazo ya televisheni lililoanza msimu huu.
Kwa wastani klabu za EPL zimetumia pauni milioni 60, ambapo kiasi cha pauni milioni 155 zimetumiwa katika siku ya jana, iliyokuwa ya mwisho kabla ya dirisha kufungwa, tofauti na mwaka jana ambapo zilitumiwa pauni milioni 140.

Klabu nne zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) msimu huu – Arsenal, Leicester City, Manchester City na Tottenham Hotspur – kwa pamoja wametumia pauni milioni 385 – ikiwa ni karibu theluthi ya kiasi chote kilichotumiwa na klabu 20 za EPL.

Tangu kuanzishwa mfumo wa dirisha la usajili, jumla ya matumizi ya kusajili wachezaji yamezidi pauni bilioni 8.6, ambapo zaidi ya asilimia 80 yake imetumika kwenye dirisha la kiangazi, nyingine ikiwa lile la 3000
Klabu zilizovunja rekodi zao, majina ya wachezaji na kiasi cha mamilioni ya pauni za Uingereza kilichotumika kununua wachezaji husika ni kama ifuatavyo:

Manchester United: Paul Pogba (£89m), Bournemouth: Jordon Ibe (£15m), Liverpool: Sadio Mane (£34m na yaweza kupanda hadi £36m), Sunderland: Didier N’Dong (£13.6m), Crystal Palace: Christian Benteke (£32m),​Hull: Ryan Mason (£13m), West Ham: Andre Ayew (£20.5m), West Brom: Nacer Chadli (£13m), Leicester: Islam Slimani (£29m), Watford: Roberto Pereyra (£13m), Southampton: Sofiane Boufal (£16m), Burnley: Jeff Hendrick (£10.5m) naSwansea: Borja Baston (£15.5m)​

Klabu mbili za Manchester pekee zimetumia zaidi ya pauni milioni 150 kwenye dirisha hili. Wachezaji waliorejeshwa kwenye klabu zao ni Pogba kwa Man United na David Luiz aliyerejea Chelsea baada ya mabadiliko ya makocha ambao hawakuwapenda wakawauza.

Lakini pia kuna nyota walioondolewa, Arsenal wakimweka kando kiungo Jack Wilshere anayeenda Bournemouth kwa mkopo wa msimu mzima huku Man City wakiwatoa Samir Nasri, Joe Hart, Wilfried Bonny na Eliaquim Mangala wameondoka Etihad, wote wakikadiriwa kuwa na thamani ya soko ya paunimilioni 62.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version