Suala la afya ya wachezaji na ustawi wake ni mojawapo ya masuala yenye kuhitaji umakini wa hali ya juu.matokeo ya uwanjani ya wachezaji hutokana na maandalizi mazuri lakini pia na hali za afya ya akili na mwili. Mwili hautakiwi uwe na majeraha ambayo yatakayosababisha mwanamichezo asitekeleze majumu yake vizuri. Majeraha yanaweza kuwa ya nje yaliyo katika mfumo wa mchubuko na vidonda ama yanaweza yakawa ya ndani.
Majeraha ya ndani yanaweza yakawa kwenye mifupa, misuli ama kwenye viungo vyovyote vya mwili ambavyo hupatikana ndani ya mwili. Wanamichezo halikadhalika wanatakiwa kujitahisi kujizuia wasiwe na majeraha makubwa ambayo yanaweza kuwafanya watumie gharama kubwa katika matibabu na tahadhari wanatakiwa wawe nayo wanamichezo wote wale wanayocheza ya kulipwa na wanaocheza isiyo ya kulipwa.
Afya ya akili nayo katika ulimwengu wa sasa imekuwa ni jambo ambalo latakiwa litiliwe mkazo sana kwani matokeo mzuri kwa timu hutegemea namna wachezaji walivyo kaa sawa kihisia ambapo hisia zao huchangia katika utendaji wao ambao huchangia katika upatikanaji wa matokeo yao ya uwanjani. Masuala ya mahusiano ya wanamichezo na jamii nayo halikadhalika huchangia kwa kiwango kikubwa katika utendaji wao wa kila siku.
Umuhimu wa afya ya mchezo uko wazi na ndio maana vilabu vikubwa navyo vimewekeza kwa wataalamu wa fani hiyo kwa ajili ya kuzungumza na wachezaji ili wawaaandae vizuri wachezaji hao kwa ajili ya mashindano yenye ushindani. wanamichezo wengi wa kulipwa wamewahi kulalamika kushindwa kufanya vizuri katika mashindano kutokana na kwamba akili zao hazikuwa vizuri. mfano mwanasoka maarufu kutoka nchi ya Brazil bwana Adriano hudai kwamba kushindwa kwake kuendelea na kucheza soka la kiwango kulitokana na taarifa alizozipata za kifo cha baba yake mzazi na taarifa hizi zilimfanya akashindwa kucheza michezo kadhaa ya klabu yake ya wakati huo ya Inter Milan na kurudi nchini kwao. pindi aliporudi nchini kwao alikaa kwa mda kadhaa na alishindwa kuendelea na kucheza soka la ushindani.
Elimu ya afya ya michezo inapaswa ianze kutolewa kuanzia ngazi za chini na hivyo kuwasaidia wanamichezo kuanza kujiweka sawa na fani hii adhimu ambayo inaweza kuwasaidia wanamichezo kwenye mambo yafuatayo:moja ni Kuwafanya wachezaji wacheze mda mrefu. maendeleo ya sayansi ya tiba ya mifupa yanaonyesha kwamba wanamichezo wengi katika dunia ya sasa wanaweza kucheza katika kiwango cha juu kwa mda mrefu.
Katika miaka ya huko nyuma wanamichezo wengi walikuwa wanashindwa kuendelea na michezo ya ushindani pindi wanapokuwa wameingia umri wa miaka 30 lakini kwa sasa tunaona wanamichezo wanaweza kucheza hata hadi umri wa miaka 40 kama wakifuatilia vizuri kanuni za afya michezoni.
Pili ni Kupunguza hatari ya majeraha. wanamichezo na watu wanaowasimamia hao wanamichezo kama wakisimamia vizuri kanuni za afya michezoni basi hatari ya majeraha makubwa inawezekana kuyapunguza kwa wanamichezo husika. kama wanamichezo watakuwa na elimu ya afya michezoni basi wataweza hata kuyatibu majeraha watakayokuwa wanayapata kwa uangalifu mkubwa.
Tatu ni Kuwafanya wachezaji wacheze vizuri. wanamichezo ambao watakuwa wana elimu ya afya michezo ama katika vilabu vyao vya michezo kutakuwa na mtaalamu aliyebobea huwa wanajipanga vizuri zaidi kimichezo na hili huwasaidia kufanya vizuri.
Nne ni Kuwajengea wachezaji uwezo wa kujiamini. wanamichezo ambao wana elimu ya afya ya michezo huwa wanajiamini zaidi kuliko wale wasio na elimu hiyo. kujiamini huko huwasaidia kuwa na matokeo mazuri katika mashindano mbalimbali
Mwisho niseme elimu ya afya michezo sio jambo dogo bali ni jambo ambalo linahitaji uwekezaji kwa hiyo kwa kuwa lina manufaa makubwa basi taasisi za michezo zisione gharama katika kuwekeza katika hilo kwani lina faida kubwa sana.