Zipo habari za kutisha kwamba miongoni mwa klabu za Ligi Kuu ya England (EPL) huenda watakaohukumiwa, kutokana na kukabiliwa na mashtaka juu ya matumizi ya fedha yasiyoendana na kanuni zilizowekwa.
Hii inakuwa kana kwamba ni tishio kwa ligi na club Tick-tock. Wanadamu hupenda kufuatilia tukio au mfuluzo wa matukio unaotokana au kusababishwa na kitu fulani, yawe ya kidini au kwa maana nyingine yoyote, ikiashiria mwisho wa nyakati
Wamaya walipata kuuweka mwisho wa dunia kwamba ungekuwa Desemba 21, 2012, ambao tukirudi nyuma si ajabu ingekuwa ni ofa ambayo tulitakiwa kuikubali. Historia nzima ya kitamaduni ya miaka ya 80, kimsingi, ni Midge Ure akitembea kwenye wingi kubwa la Vienna akiwa na koti kubwa la Ngozi, akisubiri kifo kutoka mawinguni.
Hata hivyo, ni wazi, mambo0 huendelea kutokea. Dunia huendelea kukua, lakini watu hawaishi kutokea na kuuliza kiko wapi. Droo kwa ajili ya michuano ya Euro inakaribia kupangwa. Mfalme Charles anahofia methane. Midge Ure siku hizi anaishi Somerset.
Ni muhimu kutilia maanani kwamba kuhusu habari zile za kutisha, Manchester City na Bodi ya Ligi Kuu wamekubaliana juu ya tarehe kwa ajili ya mchakato wa kusikiliza mashtaka juu ya kwenda kinyume katika matumizi ya fedha, wakati unaoogofya, si tu kwa City, bali pia kwa hatma ya ligi yenyewe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na ‘Daily Mail’, baraza hilo maalumu kwa ajili ya mashitaka ya Man City litaanza kazi yake majira ya vuli na huenda hukumu ya mwisho ikatoka 2025. Hata kabla ya rufaa yoyote, hiyo itakuwa tayari ni miaka miwili tangu kuanzishwa kwa mashitaka hayo, na kusubiri huiko tayari kumetia baadhi hasira.
Ipo sababu nzuri ya kucheleweshwa huko, hasa ikizingatiwa Man City ni tofauti na Everton waliokiri kosa lao moja, wakaishia kupokwa pointi 10 za msimu huu. Man City wanakanusha mashitaka yote 115 dhidi yao na wanatarajia na wamejipanga kujitetea na wanasheria nguli.
Zaidi ya hapo, mashitaka hayo yanahusisha matukio ya misimu 14, wakiwa pia wamepata kuwa klabu yenye faida zaidi duniani. Kwa hiyo sasa kinachosubiriwa ni mishale ya saa kuendelea kutiki hadi zifike siku husika.