Menu
in , , ,

Ukiacha joto, vipi kitisho cha ugaidi Qatar?


MALUMBANO yanaendelea iwapo michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022.

itafanyika nchini Qatar. Fainali za mwaka huu zilifanyika nchini Brazil, ambapo Ujerumani waliibuka mabingwa.

Michuano ya mwaka 2018 itafanyika nchini Urusi, ambako kunadaiwa kuwa na baridi kali. Wajumbe wa Shirikisho la Soka la Kimataifa ( Fifa) walizichagua nchi hizokuwa wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia, lakini kuna ubishani mkubwa kuhusiana na Qatar.

Kwa Urusi, mambo yalibadilika na inaonekana mgogoro wake si mkubwa. Wamejipanga vilivyo, lakini masuala ya kisiasa yamekuwa magumu kwa upande wao kutoka kwa mahasimu wake, Georgia na Ukraine kwa upande mmoja, kisha nchi za Magharibi na Ulaya kwa ujumla wamekuwa mahasimu wa taifa hilo linaloongozwa na Vladimir Putin.

Bahati mbaya sana, Qatar ni taifa la kwanza katika ulimwengu wa Kiarabu kupewa nafasi ya kuandaa michuano hiyo na wamejipanga kwa namna nyingi kuanzia viwanja na masuala ya utalii.

Hata hivyo, taifa hilo huwa kwenye kipindi cha joto kali ifikapo Juni na Julai, ambapo michuano ya Kombe la Dunia hufanyika. Kampeni kubwa ya kuwapiga vita Qatar washindwe kuandaa fainali hizo imezidi kushika kasi.

Lakini pia kampeni ya pili haijaanza rasmi, ingawaje mapema mwaka jana kulidokezwa tishio la ugaidi. Suala la ugaidi na mapigano yanayoendelea nchini Irak na Syria dhidi ya Marekani na washirika wake, ni dhahiri linaweza kuathiri taswira yaQatar.
Kwenye fainali za 2010 ziliyofanyika nchiniAfrika Kusini kulizuka tishio kama hilo. Sababu ni kwamba nchi jirani ya Angola ilikuwa imekumbwa na mkasa wa waasi wa jimbo la Cabinda.

waliokishambulia kikosi cha Timu ya Taifa ya Togo.
Kikosi cha Togo kilishambuliwa wakati kikitoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye mechi za maandalizi. Angola ni taifa jirani na Afrika Kusini, hivyo suala hilo likadaiwa kuiathiri Afrika Kusini.

Hata hivyo, michuano hiyo ilifanikiwa kufanyika na mambo yakaenda vizuri. Kwa sasa Qatar ndiyo gumzo zaidi, ambapo wajumbe mbalimbali waFifa wamekuwa wakitofautiana wanapokuwa nje ya ofisi za shirikisho hilo.

Ukweli ninaoona hapa kwamba kutakuja kampeni nyingine ya kitisho cha ugaidi. Kitisho hiki kitatumika kama nyenzo ambayo itawaondoelea nafasi Qatar kuandaa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022.

Qatar inapakana na Saudi Arabia na Bahrain kwa upande wa magharibi na kaskazini. Qatar inapakana na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa upande wa mashariki. Vile vile ukisoma ripoti za nchi zenye kuhifadhi magaidi kwa mujibu wa Marekani, inaelezwa kuwa Qatar ni eneo hatari ambalo linahatarisha usalama wa ukanda huo.

Pengine zinaweza kuwa tetesi lakini bado haiondoi ukweli kwamba Qatar watakumabana na kampeni kali dhidi yake kwa kigezo cha vitisho vya ugaidi.

Soka ni mchezo wa burudani.
Soka ni mchezo wa furaha na upendo. Lakini vitisho vyovyote vinavyosababisha kuondoka hayo yote, basi hakuna ulazima wa kufanyika kwa michuano hiyo katika eneo husika. Inawezekana Qatar imeweka ulinzi mzuri sana. Huenda Qatar inaweza kukabiliana na vitisho vya ugaidi, lakini ni wazi suala hilo la ugaidi linaweza kusababisha kuporwa uenyeji.

Ingawa Fifa inasisitiza hakuna mabadiliko, kinachoendelea nchini Irak, Syria, na Saudi Arabia kuungana na Marekani kupambana na magaidi wa ISIS ni dhahiri itakuwa shida nyingine.

Hofu yangu ni namna gani Qatar wataepuka kampeni dhidi yao. Ni namna gani wataepuka kikombe cha vitisho vya ugaidi. Hapo ndipo penye swali gumu. Itakuwaje

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version