Menu
in ,

Ufunguzi wa mafunzo ya mpira wa kikapu kwa vijana chini ya miaka 17 na mkufunzi Greg Brittenham toka Marekani

Ndugu Mgeni rasmi Mhe. Shy-Rose Bhanji, Mbunge Afrika Mashariki,
Greg Brittenham kocha toka Marekani,
Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani Mhe. Dosset Tabari,
Mwakilishi wa serikali,
Ndugu wanamichezo,
Wanafunzi, wazazi, walimu na Makocha,
Wadau wote wa Michezo,

Awali ya yote nawashukuru wote mlioshirikiana nasi kufanikisha mafunzo haya.

Nawashukuru wazazi na walezi kwa kuwaruhusu watoto wao waje katika mafunzo haya, nawashukuru walimu wa mashule mbalimbali hapa Arusha na miji jirani kwa ushirikiano mkubwa kufanikisha vijana wao kufika katika mafunzo haya.

Mafunzo kwa vijana wadogo ni sehemu ya mpango mkakati wetu wa kuinua kiwango cha mchezo wa kikapu nchini.
Hivyo tunafanya kila jitihada ili mafunzo kama haya yawafikie vijana wengi nchi nzima, leo hii mji wa Arusha na miji jirani mnafaidika na mpango huu.

Mafunzo haya yamewezekana kwa msaada wa Mtanzania na Mwanamichezo aneishi Uingereza ndugu Israel Saria mmliliki wa www.tanzaniasports.com/new na mchamabuzi wa michezo BBC Idhaa ya kiswahili. Tunamshukuru sana Kocha Greg Brittenham kwa kukubali kuwndehsa mafunzo haya bila malipo yoyote.
Kocha Greg ni moja kati ya makocha bora sana duniani wa kikapu, hivyo vijana wa Arusha mmepata bahati ya kufundishwa na moja kati ya makocha bora kabisa duniani.
Mmoja wa wanafunzi wa Greg ni Patrick Ewing nadhani wengi mnafahamu ni mmoja kati ya wachezaji mahiri sana watano duniani na yukatika Hall of Fame.
Majuma machache yaliyopita nilipata bahati ya kukutana na mchezaji mwingine nyota wa zamani wa NBA Rolando Blackman ambaye naye tunapanga kuendesha mafunzo kama haya sehemu nyingine za nchi yetu nae alisema Tanzania tumebahatika kumpata Greg kwani ni kocha bora kabisa hivyo vijana mtafaidika sana.

Tunawashukuru sana watu wa Marekani kwa kuendelea kushirikiana nasi katika kuendeleza vijana wetu kupitia mchezo wa kikapu, mipira hii mnayotunia leo na gharama za uendeshaji zimetolewa na watu wa Marekani, idara ya mambo ya nje kupitia Ubalozi wao hapa Dar Es Salaam, tunawashukuru sana na leo wametuma mwakilishi wao tuko nae hapa Mhe. Tabari.

Tunawashukuru Cocacola kwa kutoa vinywaji vinavyotumika hapa na pia wadau wengine wote waliotusaidia.

Mhe. Mgeni rasmi na ndugu wanamichezo jana nilikuwa na mazungumzo na Kocha Greg na tumekubaliana kufanya mafunzo tena siku za baadae na kuendeleza ushirikano wetu na siku za mbele tutaangalia uwezekano wa kuwapelekea vijana wetu wa hapa waende USA kushiriki katika clinic kama hizi ili kupata uzoefu zaidi na pia vijana wa marekani waje Tanzania ili kushirikiana na vijana wetu katika mafunzo na pia kutembelea Tanzania.

Mhe. mgeni rasmi, mchezo wa kikapu kwa taarifa tu ni wa pili ukifuatia soka kwa kupendwa kuwa na wachezaji wengi na wafuasi wengi hapa Tanzania.
Hivyo tuna kila sababu ya kuwekeza zaidi katika kuendeleza mchezo huu katika miundombinu ya mchezo yaani viwanja, vifaa vya michezo na pia kuwekeza katika kuendeleza mafunzo kwa vijana wadogo ili tujenge msinhgi imara.
Tunawashukuru Cocacola wanafanya marekebisho kwenye baadhi ya viwanja ila lengo letu ni kuwa na viwanja katika kila wilaya na baadae kila kata nchini Tanzania na katika kila shule za msingi, sekondari na vyuo vyote nchini Tanzania.

Mwaka huu kwa kushirikiana na Cocacola tutaanza mashindano ya vyuo hii ni sehemu ya uendelezaji na uibuaji wa vipaji vyuoni.
Tunaomba wadau wengine wajitokeze kutusaidia kufikia malengo yetu.

Faida za mafunzo haya ni nyingi, moja ni kuwapatia vijana elimu ya mchezo kitaalamu hivyo kuwajengea msingi imara, pili tunawajenga kitabia na kimaadili kupitia mafunzo haya ili waweze kuwa raia bora na waweze kufanikiwa katika maisha yao, tatu wale wanaofanya vizuri huwa tunawaendeleza kwa kuwapatia mfunzo zaidi kulingana na mahitaji. Na ndio maanaleo hii tuko na kocha wa timu ya Taifa ya kikapu ya Tanzania ndugu Everist Mapunda na ndugu Bahati Mgunda ambaye ni mmoja wa makocha wetu mahiri na anaendeleza vijana kupitia taasisi yake ya Mambo Basketball.
Kwa kushirikiana na Mambo, TanSao na. NewFound Memorial University mwaka jana tulimpeleka kijana wetu mmoja kusoma Chuo Kikuu Canada kwa schorlaship iliyotokana na kikapu na kijana huyo ni matokeo ya clinic kama hizi.

Hivyo vijana mjitahidi na mfanikio yatapatikana kama mtajitahidi na kufanya vizuri katika mchezo wa kikapu na pia mfanye vizuri katika masomo yenu.

Mhe. Mgeni rasmi Licha ya mafanikio hayo bado tuna changamoto nyingi ikiwemo kukosekana kwa ufadhili katika mashindano mengi na pia kuna tatizo sugu la viwanja kama unavyoona manispaa ya Arusha na manispaa nyingi nchini hazina viwanja vya wazi vya wananchi yaani ” Public courts” ambapo kila mwanachi angepata fursa ya kucheza kirahisi. Ili kutumia uwanja kama huu tuliopo inabidi kuomba kibali kwa wahusika na wakati mwingine hatupati na wakati mwingine ni gharama kubwa kwani tunahitajika kulipa na vyama vyetu vingi vya mikoa na hata Taifa bado vinakabiliwa na tatizo sugu la uhaba wa vyanzo vya mapato.

Hivyo basi kupitia wewe kwa kuwa wewe ni mbunge mpenda michezo na mtaalamu wa mawasiliano tunaomba uhimize suala hili kama ni fursa ya uwekezaji. Na tuige mfano wa wenzetu nchi za nje ambapo makampuni makubwa yanajenga au kuwekeza katika viwanja na kuvipa majina yao mfano Staple Center Los Angels, American Airlines Arena Miami, Turkish Airline Arena Instabul, Toyota Center Houston, FEDEX Center Memphis n.k. Hii ni nia moja njia mbapo taasisi kubwa zinawekeza katika jamii.
Naamini jambo kama hilo linaweza kufanyika hapa Tanzania pia.

Hivyo nichuke nafasi hii kuomba wadau wote waone fursa hii ya uwekezaji.

Naomba mgeni rasmi kupitia wewe basi uweze kuishawishi taasisi mbalimbali ili zione umuhimu wa kuwekeza katika jamii kupitia mchezo wa kikapu.

Mhe. Mgeni rasmi naomba pia utumie nafsi yako kama Mbunge kuongea na wenzako ili mtusaidie katika kukabiliana na changamoto hizi na nyingine ili tuweze kutumia michezo kutatua changamoto mbalimbali katika jamii yetu ikiwemo suala la ajira kwa vijana.

Tunakushuru sana kwa kufika kwako na tunaomba uendelee kushirikiana nasi katika kuendeleza vijana wetu kupitia mchezo wa kikapu.

Ahsanteni kwa kunisikiliza,

Phares Magesa
Makamu wa Rais- TBF.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version