FAINALI za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) na Ligi ya Europa zinakutanisha timu nne zote za England, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia kwa nchi moja ya Ulaya kufikisha humo timu nne.
Liverpool watakutana na Tottenham Hotspur kwenye fainali ya UCL jijini Madrid hapo Juni mosi wakati Arsenal watapepetana na Chelsea huko Baku Mei 29 katika fainali ya Ligi ya Europa.
Huku washindi wa mashindano yote hayo wakiingia kwenye UCL kwa ajili ya msimu ujao, inamaanisha nini kwa Ligi Kuu ya England (EPL) na watu wake kufuzu? Timu nne za juu EPL zinafuzu kwa UCL wakati mabingwa wa Kombe la FA na watakaoshika nafasi ya tano wanakwenda kwenye Ligi ya Europa.
Ikiwa mabingwa wa makombe haya mawili watamaliza katika nafasi nne za juu, itamaanisha kwamba nafasi zao zitakwenda kwa Ulaya zitakwenda kwa timu zitakazoshika nafasi ya sita nay a saba kwenye EPL.
England watapata timu ya tano kwenye UCL ikiwa timu itakayomaliza nje ya nne bora itapata ushindi kwenye moja ya mashindano hayo. Arsenal wanaelekea kumaliza katika nafasi ya tano ikiwa Manchester United hawatawavuka katika siku ya mwisho ya ligi hiyo, wakiwa nyuma ya Spurs kwa alama tatu na mabao manane huku ikiwa imesalia mechi moja.
Hii inamaanisha kwamba watatakiwa kushinda Kombe la Europa ili kufuzu kwa UCL mwakani kwa sababu kufunga idadi hiyo ya mabao takikana ni ngumu. Nafasi nne za juu kimsingi zinakwenda kwa Manchester City, Liverpool, Spurs na Chelsea kwa hiyo Arsenal watamaliza nje, lakini wanatakiwa kuchukua Kombe la Europa.