Menu
in , ,

Ubora wa refa katika vita ya Yanga na Azam

MECHI nzuri, ufundi mwingi na umahiri wa wachezaji na makocha ulioneshwa kwenye mchezo wa Liugi kuu kati ya wenyeji Yanga na wageni wao Azam fc. Ulikuwa mchezo ambao uliwapa burudani mashabiki huku mwamuzi akionesha sababu zote kuwa bora kati ya wengi waliopo nchini. Mara baada ya mwamuzi Ahmed Aragija kupuliza filimbi ya kuashiria kumalizika kwa mchezo kati ya mabingwa watetezi na Azam FC kamera za Televisheni zilielekezwa zaidi kwa kiungo mshambuliaji Feisal Salum. Kiungo huyo wa Azam fc hakuonesha makeke kama ilivyokuwa mchezo uliopita ambapo alipachika bao moja. 

Tanzania Sports

Katika mchezo huo Fei Toto alikuwa akiongoza jahazi la Azam fc akishirikiana na wachezaji wenzake hakuwa yule ambaye alipania kila mechi aliyokutana na wanajangwani hao. Katika mchezo huo w a Ligi Kuu Tanzania Bara ulishuhudia beki wa kati wa Yanga Ibrahim Bacca akitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi mshambuliaji Nassoro Saadun wa Azam. Je ni mambo gani yaliyotokea kwenye mchezo huo?

Uwezo wa mwamuzi Aragija

Mara nyingi amekuwa akilaumiwa kwa maamuzi yenye utata, lakini Ahmed Aragija mwamuzi wa CAF na FIFA alionensha uwezo mkubwa na kumudu mchezo huo. Mwamuzi huyu anasifika kwa uwezo wa kusimamia sheria za mchezo wa soka na ndiye bora zaidi. Licha ya mechi kuwa na presha kubwa lakini refa huyo hakuonekana kuyumba kimaamuzi. Aragija alitoa kadi sahihi kwa wakati sahihi, alikemea na kuonya wachezaji. Aliwakumbusha ‘Fair Play’ kiasi kwamba aliwafanya wachezaji hao kuishiwa hoja pale walipokuwa wanamlalamikia. Kwa mfano wakati Ibrahim Bacca akimshika mabega mshambuliaji wa Azam, Saadun alikuwa mchezaji wa mwisho ambapo sheria ilikuwa upande wa mwamuzi na hakufanya ajizi kwa kumwonesha kazi nyekundu. 

Ubingwa bado mbichi

Hii ilikuwa mechi ya 9 kwa upande wa Yanga wakati Azam wao ilikuwa ya 10. Yanga wamejikusanyia pointi  24 wakiwa kileleni, wakati Azam wanashikilia nafasi ya nne wakiwa na pointi 21. Tofauti ya kinara wa Ligi na anayeshika nafasi ya nne ni pointi 3 sawa na mchezo mmoja. Nafasi ya pili imeshikiliwa na Simba wenye pointi 22 kutokana na michezo 9. Singida Black Stars wao wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 22 sawa na Simba. 

Timu hizo nnje unaweza kusema mojawapo ndiyo itakuwa bingwa wa Ligi Kuu. Fountaine Gate waowanashikilia nafasi ya tano wakiwa na pointi 17, sawa na kusema wako nyuma kwa pointi 6 na kinara wa Ligi. Tofauti finyu ya pointi kutoka nafasi ya kwanza,pili,tatu nan ne ni mechi moja. Kwamba anayeshinda mchezo unaofuata kati ya timu hizo nne anaweza kuongoza Ligi Kuu. Hata hivyo uwezo wa timu zote unaonesha kuwa Ligi bado mbichi na ubingwa hauna mwenyewe. Matokeo ya alama tatu waliyopata Azam inamaanisha kuwa yeyote anaweza kufungwa na mbio za ubingwa ni ndefu hadi mwakani.

Goli la video

Kwenye mpira wa miguu kuna magoli ya video. Haya ni magoli yenye mvuto wa kipekee. Goli lililofungwa na winga wa Azam fc, Sillah katika dakika ya 33 ya mchezo lilikuwa na mvuto wa aina yake. Alipokea pasi kutoka katikati ya 18 akitokea winga wa kulia kisha akaupeleka mpira kwenye mguu wa kushoto na kuachia shuti kali lililomwacha hoi golikipa wa Yanga, Djigui Diarra

Ugumu wa Yanga kufungika

Ingawaje mchezo huo wamepoteza lakini Yanga wameonesha ni timu tishio ili kuwafunga unapatakiwa kufanya kazi mara mbili zaidi yao. Azam fc walifanya kazi kubwa kucheza dhidi ya timu pungufu ya Yanga. Mashambulizi ya mara kwa mara kutokea pande zote yalionesha timu hiyo ilivyo hatari. Azam walilazimika kujilinda kwa muda mwingi ili kuhakikisha ushindi wao unamalizika kwa alama tatu. Ni dhahiri shahiri kuwa ili kuwafunga Yanga inabidi uhakikisha wanakuwa pungufu kiwanjani, kwa maana ya kuwatafutia kadi za njano na nyekundu ili watolewe nje au kuwa na hofu ya kutolewa hivyo uwezo wao unashuka.

Uenyeji wa Azam Complex 

Yanga na Simba hazina viwanja wote kwa pamoja wanakodi uwanja wa Azam Complex katika baadhi ya mechi zao za Ligi Kuu. Katika mechi ambazo wamekuwa wenyeji kwenye uwanja wa Azam Complex kumeshuhudiwa matokeo ya kushangaza. Yanga wamepoteza 1-0 wakiwa wenyeji wa mchezo huo kwenye dimba la Azam Complex. Kwenye michezo iliyopita Azam fc wakiwa wenyeji walichapwa mabao 2-0 na Simba, Simba wakiwa wenyeji kwenye uwanja huo huo walichapwa 1-0 na Yanga. Sasa imekuwa zamu ya Yanga kuambulia kipigo.

Rekodi ya Taousi

Kocha mkuu wa Azam ni Rachid Taousi ameweka rekodi ya kukiongoza kikosi chake na kuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga. Katika mchezo huo Azam fc walimtumia Nassoro Saaduni kiwenye safu ya ushambuliaji na mara nyingi alikuwa peke yake huku mawinga wa kulia na kushoto warudi nyuma katika mbinu za kujilinda. Mpango wa kwanza wa Azam ulikuwa kucheza 4-5-1 ambapo nusu ya eneo lao walikuwa wamejipanga kujihami na walipopata nafasi ya kushambulia walipiga pasi ndefu au kupenyeza ndefu kisha wachezaji wa mbele kukimbizana na mabeki wa Yanga. Katika mchezo huo Taousi alionesha furaha kubwa mara baad aya filimbi ya mwisho kwani ilikuwa inamaanisha yeye ndiye kinara na ameweka rekodi ya kuwafunga mabingwa watetezi.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version