Menu
in , , ,

Ubingwa Man City, Liverpool?

*Chelsea wanyemelea, Arsenal majanga

Siku za mwisho za Ligi Kuu ya England hazijafika, lakini kuna mwelekeo unaowapa Manchester City na Liverpool nafasi kubwa ya ubingwa, bila kuwasahau Chelsea.

Liverpool wamepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham leo na kurudia kwenye kiti cha uongozi baada ya kukaliwa kwa muda na Chelsea.

Liverpool hawakupata ushindi kirahisi, na labda ndiyo maana mabao yao yalitokana na penati kiasi cha baadhi ya wadau kuwabatiza jina la ‘wafalme wa penati.

Hata hivyo, kwa ujumla kwenye msimu huu Liverpool wameonesha uwezo kwenye mechi zao, wakiwaacha mbali wapinzani wao wa jadi nchini, Manchester United ambao sasa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo, wakiwa hawana uhakika wa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Nahodha wa Liverpool, Steven Gerard ndiye aliyewabeba tena Jumapili hii kwa mabao mawili ya penati katika kila kipindi wakati West Ham walipata bao lao kupitia kwa Guy Demel.

Liverpool waliocheza mechi 33 sawa na Chelsea na Arsenal, wamefikisha pointi 74 wakati Chelsea wakiwa na 72, Manchester City wenye pointi 70 kwa mechi 31 wakiwa katika nafasi ya tatu na Arsenal wakiwa nafasi ya nne kwa pointi 64.

Arsenal waliadhiriwa ugenini kwa Everton Jumapili hii, baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 ambacho hakikupata kutokea kwa muda mrefu, na kufufua matumaini ya Everton kupata nafasi kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Everton sasa wanawapumulia Arsenal baada ya kufikisha pointi 63 lakini wana mchezo mmoja mkononi. Hata hivyo, wana mechi ngumu dhidi ya Manchester City na Manchester United wanaoelekea kufufuka sasa.

Liverpool wenyewe bado wana mechi dhidi ya Manchester City na Chelsea, kwa hiyo suala la ubingwa linawezwa kuwa gumu bado kudhani timu ipi itatwaa.

Baada ya mechi za mwisho wa wiki hii, msimamo unabaki kwamba Liverpool wanaongoza wakifuatiwa na Chelsea, Man City, Arsenal na Everton, huku wakichomoza Manchester United na Tottenham Hotspur, na kama Spurs watashinda mechi ya Jumatatu dhidi ya Sunderland watawarudisha Man U kwenye nafasi ya saba waliyokaa kwa muda mrefu.

Nafasi tatu za mwisho ni Fulham wenye pointi 27, Cardiff pointi 26 wote wawili kwa mechi 33 wakati Sunderland wana pointi 25 kwa mechi zao 30, ambapo wakifanya vizuri kwa mechi za mkononi wanaweza kuepuka kikombe cha kushuka daraja

51.577966-0.130392

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version