Katika ligi kuu ya soka Tanzania bara toka ianzishwe kumekuwa kuna wafungaji wengi sana wa mabao ambao waliwahi kutokea. Wafungaji hao wamevuma katika vipindi tofauti. Umahiri huo umevisaidia vilabu vyao kupata ushindi katika mechi na halikadhalika baadhi mpaka kubeba vikombe vya ligi. Katika wafungaji wote Tanzania waliowahi kuwika katika kipindi cha hivi karibuni hakuna ambaye amefanikiwa kuivunja rekodi ya ufungaji mabao ambayo iliwekwa na mshambuliaji zamani wa Yanga bwana Mohammed Hussein maarufu kama Mmachinga ambayo aliiweka mnamo mwaka 1997 ambapo aliibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kwa kutikisa nyavu za vilabu pinzani mara 26. Mpaka hivi leo hakuna mmpachika mabao ambaye ameweza kuvunja rekodi hiyo licha ya kwamba miaka 26 imepita na hakuna ambaye aliyeivunja rekodi hiyo.
Tuzo maarufu katika ulimwengu wa soka ya ufungaji bora imepewa jina la “PUSKAS AWARD”. Jina hilo linatana mshambuliaji gwiji wa zamani wa klabu ya soka ya Real Madrid. Klabu ya Real Madrid ilimsajili gwiji wa soka kutoka taifa la Hungary bwana Ferenc Puskas wakati akiwa na umri wa miaka 31 na kwa wakati huo alikuwa amefungiwa kucheza soka kwa kwa mda wa miaka miwili na wakati alipokuwa amesajiliwa alikuwa ana uzito uliokuwa umezidi sana na alikuwa ana muonekano wa kitambi kikubwa ambacho kiliwafanya watu wengi waamini kwamba mchezaji huyo atavurunda na hatakuwa na mafanikio yoyote yale katika kikosi hicho.
Muono wao ulikuwa una makosa kwani katika misimu ambayo mchezaji huyo alikaa katika jiji la Madrid alikuwa kinara wa mabao kwa rekodi ambayo haijawahi kuvunjwa mpaka hii leo. Katika mechi 262 ambazo alifanikiwa kucheza alifanikiwa kutikisa nyavu za goli za klabu pinzani mara 242. Alifanikiwa kushinda aina yote ya mataji ya makombe ambayo alishiriki kwa nyakati hizo. Umahiri wake wa kufunga magoli hauna mfano mpaka hii leo. Mafanikio yake hayo yakapelekea tuzo hiyo ufungaji mabao mengi ipewe jina lake ambapo huiitwa .halikadhalika tuzo ya goli bora la msimu nayo kwa baadhi ya maeneo imebeba jina lake na hiyo inatokana na athari yake aliyoifanya ndani ya kipindi kifupi alichocheza soka la kulipwa.
Muhammed Hussein anastahili kuheshimishwa kwa kupewa tuzo ya mfungaji bora ibebe jina lake kwani rekodi yake imekaa mda mrefu sana haijavunjwa. Licha ya kwamba kumejitokeza washambuliaji wengi hatari katika ligi ya soka ya Tanzania bara lakini bado hawajaweza kuvunja rekodi yake. Wafungaji wengi waliokuja katika miaka ya hivi karibuni walikuwa wanauwezo wa kuivunja rekodi yake ukichukulia suala la kwamba walikuwa wana bajeti kubwa sana ya mishahara pamoja na posho za motisha(bonus) pindi wanapofanya vizuri uwanjani hususani wanapofunga magoli tofauti na namna ambavyo Muhammed Hussein alivyokuwa. Uwekezaji mkubwa katika soka la Tanzania ambao ulifanywa na wafanyabiashara wakubwa kama Bakhresa, Yusuf Manji, Mohammed Dewji, Ghalib Mohammed na wengineo bado haujawa chachu ya kuwafanya washambuliaji wapambane Zaidi kushinda magoli mengi Zaidi ili waweze kuivunja rekodi hiyo.
Alijaribu Abdallah Juma wa Mtibwa na akaishia kufunga magoli 25 na huyo ndiye aliyekuwa na nafasi klubwa ya kuvunja rekodi hiyo. Alijaribu mshambuliaji hatari wa Rwanda bwana Meddie Kagere na akaishia kufunga magoli 23 tu katika msimu wa mwaka 2018/2019. Alijaribu hamis Tamwe mara 2 na kashindwa kuivunja mara ya kwanza ilikuwa msimu wa mwaka 2015/2016 akiwa klabu ya Yanga na alifunga jumla ya magoli 21 na msimu wa mwaka 2013/2014 wakati akiwa Simba alifunga jumla ya magoli 19. Straika wa Uganda bwana Emannuel Okwi wakati akiwa Simba alifanikiwa kufunga jumla ya magoli 20 kwenye msimu wa mwaka 2017/2018.
Straika John Bocco wakati akiwa klabu ya Azam aliwahi kuwa mfungaji bora lakini aliishia kufunga jumla ya magoli 19 tu katika msimu wa mwaka 2011/2012. Straika kutoka nchi ya Kenya bwana Boniface Ambani alifanikiwa kuwa mfungaji bora na aliishia kufunga jumla ya magoli 18 na hiyo ilikuwa msimu wa mwaka 2008/2009. Mussa Mgosi wakati akiwa Simba kwenye msimu wa mwaka 2009/2010 alikuwa mfungaji bora na alifanikiwa kushinda jumla ya magoli 18. Mrisho Ngasa alifanikiwa kufunga jumla ya magoli 18 katika msimu wa mwaka 2010/2011 wakati akiwa Yanga. Kipre Tchetche alifanikiwa kuunga jumla ya magoli 17 katika msimu wa mwaka 2014/2015 wakati akiwa Azam.
Klabu ya Yanga wameamua kumkabidhi majukumu ya kuifundisha klabu hiyo katika upande wa wanawake ambayo hujulikana Zaidi kwa jina la Yanga Princess na hiyo ilikuwa baada ya kuachana na kocha wake Edna Lema ama maarufu kama Morinyo. Licha ya uwekezaji mkubwa ambao umefanyika katika klabu hiyo lakini bado imeshindwa kupata mshambuliaji ambaye atakayewahakikishia idadi hiyo ya magoli na hata mshambuliaji machachari kutoka Congo bwana Fiston Kalala Mayele ameshindwa kuivunja rekodi hiyo licha ya motisha mbalimbali ambazo alikuwa anazipata wakati anachezea klabu hiyo yenye maskani mitaa ya Jangwani Kariakoo.