Menu
in , , ,

TUMEJIANDAA KUIKABILI UGANDA- KIM

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema kikosi chake kimejiandaa
kuikabili Uganda kwenye mechi ya marudiano ya mchujo kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN)
itakayochezwa Jumamosi jijini Kampala.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Kim amesema tangu
kikosi chake kimeingia kambini Julai 14 mwaka huu, wachezaji wamekuwa
wakifanya vizuri kwenye mazoezi na wako tayari kwa ajili ya mechi hiyo.

“Uganda ni timu bora kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Mechi
itakuwa ngumu, tunaamini tunakwenda kufanya vizuri. Tayari tunayo mikakati
kwa ajili ya mechi hiyo, tunakwenda kuikamilisha Kampala,” amesema Kim.

Hata hivyo, Kim amesema licha ya mwitikio mzuri wa wachezaji kwenye mazoezi
lakini wanakabiliwa na changamoto ya wengi wa wachezaji kuwa wamefunga
wakati wachezaji wanapokuwa kambini wanatakiwa kula, kunywa na kupumzika.

“Hiki ni kipindi kigumu kwa mpira wa miguu, na suala la kufunga ni la
kiimani ambapo hatuwezi kuwazuia wachezaji kufunga. Karibu nusu ya
wachezaji wanafunga, hii ni changamoto ambayo tunaiheshimu,” amesema Kim na
kuongeza kuwa ni wazi kikosi chake cha kwanza kitakuwa na mabadiliko baada
ya beki Shomari Kapombe kwenda kwenye majaribio nchini Uholanzi.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaondoka Mwanza
kesho (Julai 24 mwaka huu) saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir na
kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 8.15 mchana.

Wachezaji waliomo kwenye msafara huo ni makipa Juma Kaseja, Mwadini Ali na
Ali Mustafa. Mabeki ni Aggrey Morris, David Luhende, Erasto Nyoni, Kelvin
Yondani, Nadir Haroub na Vincent Barnabas.

Viungo ni Amri Kiemba, Athuman Idd, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Khamis
Mcha, Mudhathir Yahya, Salum Abubakar na Simon Msuva. Washambuliaji ni John
Boko, Juma Luizio na Mrisho Ngasa.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version