Menu
in , , , ,

Trent Arnold hakuna alichobakisha Liverpool

Tanzania Sports

DIRISHA la usajili barani Ulaya limeshika kasi kwenye vilabu mbalimbali. Timu zinafanya jitihada kuimarisha vikosi vyao, baadhi zinauza wachezaji ambao hawana nafasi ama kuhitaji fedha nyingi hivyo kulazimika kuuza mastaa wao. Miongoni mwao wapo nyota takribani 62 ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu. Nyota hao wanaruhusiwa kuingia kwenye majadiliano na timu nyingine pamoja na kusaini mkataba wa awali kabla ya kujiunga rasmi ama wanaweza kuondoka kwenye vilabu vyao. Trent Alexander Arnold ni miongoni mwa wachezaji nyota wanaowindwa na timu mbalimbali. Mkataba wake na Liverpool unaaelekea mwishowni sawa na wenzake Mohammed Salah na Virjil van Dyik. Liverpool wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kuwabakisha nyota hao kwenye kikosi chao, huku wakiwa na sababu nyepesi ya kuwashawishi kubaki.

Trent ni mchezaji wa aina gani kiufundi? 

Tangu alipoibuliwa kwenye kikosi cha kwanza na Jurgen Klopp, Trent amefanya kazi yake vizuri na ameonesha kipaji cha ziada katika uchezaji wake.l upo wakati kocha Klopp alikuwa akimtumia silaha yake ya kuongoza nguvu kwenye eneo la kiungo licha ya kumpanga kama beki wa kulia. Uchezaji wa Nyota huyo uliwatamanisha wengi kwani alipika mabao na kufunga baadhi hali ambayo wadau na mashabiki waliamini anafaa kuchezeshwa nafasi ya kiungo ili awe huru zaidi. 

Kwenye mashindano ya Euro alishindwa kumudu nafasi ya kiungo na kumalzimu kocha wake GaretH Southgate kumpumzisha kisha kumrudisha kwenye eneo lake la beki wa kulia. Nyota huyo pia anaweza kupiga mipira ya faulo,kutengeneza mabao na kupiga pasi ndefu ambazo zinaleta madhara lango la adui. Kiufundi ni mchezaji ambaye anataka kushambuliaji sana na mbunifu wa kuumba namna ya kusaka mabao.

Je kwanini Trent hana cha kupoteza Liverpool?

Trent ana umri wa miaka 26 tu, lakini anaelewa umuhimu na utamu wa makombe kwenye klabu yake. Liverpool wametwaa mataji 6 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo alifanikiwa kunyakua chini ya Jurgen Klopp. Kwa maana kwenye kazi yake suala la Ligi ya Mabingwa tayari anayo medali yake. Kwenye taji la Ligi Kuu England, tayari nyota huyo anayo medali yake. Mataji haya mawili muhimu yapomepita kwenye mafanikio ya nyota huyo. Hilo lina maana mbali ya mataji mengine, nyota huyo hana la kupoteza Liverpool. Hana deni lolote kwa klabu hiyo licha ya kumlea tangu akiwa kinda hadi kuingia kikosi cha wakubwa. Kama mataji ameshatwaa na Liverpoll hivyo si suala la kumfanya abakie tena klabuni hapo. 

Je ni wapi anakokwenda nyota huyo?

Klabu ya Real Madrid inakabiliwa na msimu mbaya wa majeruhi. Nafasi ya beki wa kulia ndiyo iliyoathirika zaidi kwani tegemeo kubwa ni Lucas Vazquez ambaye kimsingi ni winga na anapangwa nafasi hiyo kwa ajili ya kuziba pengo la beki wake Dani Carvajal. Katika baadhi ya mechi beki wa kulia amechezeshwa Federico Valverde au Eder Militao. Hata hivyo Federico ni kiungo ambaye anachakachuliwa kupangwa upande huo. Vilevile Militao ni beki wa kati na huwa anapangwa huko kama kuziba pengo ambalo si jukumu lake. 

Kuumia kwa Carvajal kumewalazimu Real Madrid kuingia sokoni huku wakiwa na matumaini kumrudisha Lucas Vazquez kwenye nafasi yake ya winga wa kulia ambayo aliitendea haki kwa muda mrefu klabuni hapo. Pia Real Madrid wameripotiwa kuwasilisha ofa ya pauni milioni 25 kutaka kumsajili Trent Arnold. 

Nyota wa zamani wa Liverpool na Real Madrid Michael Owen ameandika katika mtandao wake  “hatua zozote za  Real Madrid kuwasilisha ofay a usajili wa Trent desemba 30 na kuweka mezani kiasi cha puani milioni 20 maana yake wana uhakika wa kumpata mwishoni mwa msimu endapo Liverpool watakaa kiasi hicho cha fedha. Real Madrid wanaweka ofa mahali ambapo wanauhakika napo hasa kwa mchezaji anayelekea kumaliza mkataba wake. wanamaanisha klabu ichukue kiasi hicho au wakubali kumpoteza bure mwishoni mwa msimu. Ninajua jinsi wanavyoendesha mambo yao Madrid.”

Kana kwamba haitoshi Real Madrid wameongeza dau la pauni milioni 25 yaani tano za ziada baada ya ofay a awali kuwa pauni milioni 20. Katika thamani hiyo Trent kwakuwa anaelekea kumaliza mkataba wake ni wazi klabu yake inahaha kumshawishi asaini mkataba mpya ama wakubali ofa ya Real Madrid au kukosa fedha kabisa msimu ukimalizika.

Liverpool watapoteza mastaa wake wote?

Nahodha wao Van Dyik anaelekea kumaliza mkataba. Staa wao mwenye rekodi ya aina yake EPL, Mohammed Salah naye anayelekea kumaliza mkataba wake kama ilivyo kwa Trent Alexander Arnold. Nyota hao wamecheza kwa mafanikio katika klabu ya Liverpool na dhahiri walikuwa msingi wa mafanikio hayo. Lakini sasa mikataba yao inaelekea ukingoni. Huku Liverpool wakiwa wanaongoza Ligi na wanaelekea kutwaa taji hilo, kocha wa Arne Slots bila shaka atakuwa anapoteza wachezaji muhimu katika kikosi chake. Ni suala la muda tu.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version